Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mayele ana dakika 180 za kibabe

MAYELE Pict

Muktasari:

  • Mechi hiyo inapigwa kuanzia saa 10:00 jioni kabla ya kurudiana tena Juni Mosi jijini Cairo, Misri ili kupata bingwa mpya wa msimu huu wa michuano hiyo kutokana na taji kutemwa mapema na waliokuwa watetezi, Al Ahly ya Misri iliyong'olewa nusu fainali na Mamelodi kwa bao 1-0.

KESHO Jumamosi inapigwa mechi ya kwanza ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye Uwanja wa Loftus Versfeld, Pretoria, Afrika Kusini kwa kuzikutanisha Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini na Pyramids ya Misri, huku nyota wa zamani wa Yanga, Fiston Mayele akiwa na dakika 180 za kibabe.

Mechi hiyo inapigwa kuanzia saa 10:00 jioni kabla ya kurudiana tena Juni Mosi jijini Cairo, Misri ili kupata bingwa mpya wa msimu huu wa michuano hiyo kutokana na taji kutemwa mapema na waliokuwa watetezi, Al Ahly ya Misri iliyong'olewa nusu fainali na Mamelodi kwa bao 1-0.

Hata hivyo, mechi hiyo ya kesho na ile ya marudiano wikiendi ijayo ni kama njia ya Mayele kuandika historia nyingine, sio ya kubeba ubingwa wa Afrika, lakini kunyakua tuzo ya Kiatu cha Dhahabu kwa mara nyingine ikiwa ni misimu miwili tu alivyofanya hivyo akiwa na Yanga ilifika fainali ya Shirikisho.

Katika fainali hizo za msimu wa 2022-2023, Mayele alimaliza kama kinara wa mabao akifunga mabao saba, mbali na saba mengine aliyofunga katika mechi za awali za michuano ya CAF, japo Yanga ilikwama kubeba taji kwa kanuni ya faida ya bao la ugenini mbele ya USM Alger ya Algeria.

Matokeo ya jumla ya mechi hiyo yalikuwa ni sare ya 2-2, Yanga ikipoteza nyumbani kwa mabao 2-1, bao la kufutia machozi likifungwa na Mayele na ndilo lililokuwa la saba na kumzidi straika wa Marumo Galants, Ranga Chivaviro aliyekuwa wanalingana naye kila mmoja akifunga mabao sita.

Kwa sasa Pyramids anayehusishwa kutakiwa na Kaizer Chiefs inayonolewa na kocha wa zamani wa Yanga aliyefanya kazi na straika huyo, Nasreddine Nabi ana mabao matano, akiwa ndiye kinara sambamba na wachezaji wengine wawili akiwemo anayecheza naye Pyramids, Ibrahim Adel na Emam Ashour wa Al Ahly iliyolewa katika michuano hiyo.

Mabao hayo matano yanayomfanya Mayele kuongoza orodha hiyo, ni kati ya manane aliyofunga msimu huu kupitia mechi 11 za michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa Afrika, hivyo kama atazitumia mechi hizo mbili za fainali kwa kutupia kambani huenda akarudia kile cha 2022-2023.

Mayele alianza kufunga bao moja katika mechi ya raundi ya kwanza ya michuano hiyo Pyramids ilipoing'oa JKU ya Zanzibar kwa mabao 9-1, kisha akafunga mawili walipoinyoosha APR ya Rwanda kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-2 kisha timu hiyo ikatinga makundi ya michuano hiyo.

Katika makundi alifunga bao moja tu katika mechi ya kwanza ya Kundi D dhidi ya GD Sagrada Esperança ya Angola walioilaza kwa mabao 5-1, kisha kuja kufunga mawili katika mechi ya robo fainali dhidi ya FA Rabat ya Morocco walioing'oa kwa jumla ya mabao 4-3.

Kisha akafunga mabao mengine mawili katika nusu fainali dhidi ya Orlando Pirates ya Afrik Kusini waliong'oa kwa ushindi wa 3-2, akifunga bao la kusawazisha la kwanza na lile la ushindi lililoipeleka Pyramds kwa mara ya kwanza fainali ya Ligi ya Mabingwa.

Mayele ana nafasi kubwa ya kuandika historia kutokana na wachezaji wengine waliona na mabao manne timu zao kutolewa mapema, huku Peter Shalulile wa Mamelodi Sundowns aliyefunga matatu, akiwa ndiye mchezaji wa kumpa presha ukiondoa Adel anayechuana naye kileleni kwa sasa.


ORODHA YA WAFUNGAJI

5 Fiston Mayele (Pyramids)

   Ibrahim Adel    (Pyramids)

   Emam Ashour (Al Ahly)


4 Relebohile Mofokeng(Orlando Pirates)

   Mahau Nkota  (Orlando Pirates)


3 Peter Shalulile (Mamelodi Sundowns)

   Hussein El Shahat     (Al Ahly)

   Wessam Abou Ali      (Al Ahly)

   Elias Mokwana          (Esperance)

   Achref Jabri      (Esperance)

   Aymen Mahious        (CR Belouizdad)