Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mashtaka 115 ya Man City, hukumu kusubiri mwisho wa msimu

MAN CITY Pict

Muktasari:

  • Takribani mwaka mmoja na nusu uliopita kulifanyika usikilizwaji wa mashtaka hayo 115 yanayoikabili Man City kwa muda wa wiki 12 kati ya mawakili wa Man City na wale wa Ligi Kuu England. Man City ilishitakiwa kwa kuvunja kanuni za kifedha mara 115 lakini ilikanusha vikali makosa yote na kusisitiza kwamba hawana hatia.

MANCHESTER, ENGLAND: Hivi karibuni kumekuwa na taarifa zinazokinzana kuhusu lini uamuzi wa mwisho juu ya mashtaka 115 yanayoikabili Manchester City ambapo baadhi ya ripoti zinadai hukumu huenda ikatokea wakati wa Pasaka au mwisho wa msimu.

Adhabu mbalimbali zinadaiwa huenda zikatolewa kwa Man City ambapo hivi karibuni inaelezwa kuwa huenda ikapokwa pointi 60.

Takribani mwaka mmoja na nusu uliopita kulifanyika usikilizwaji wa mashtaka hayo 115 yanayoikabili Man City kwa muda wa wiki 12 kati ya mawakili wa Man City na wale wa Ligi Kuu England. Man City ilishitakiwa kwa kuvunja kanuni za kifedha mara 115 lakini ilikanusha vikali makosa yote na kusisitiza kwamba hawana hatia.

Katikati ya Machi, mwaka huu, The Athletic iliripoti kuwa vyanzo kutoka pande zote mbili havikuwa vimepokea taarifa yoyote kutoka kwa mamlaka kuhusu ni lini uamuzi utafanyika.

Hata hivyo, mwandishi wa tovuti ya Independent, Miguel Delaney, alifichua mapema wiki hii kupitia podikasti yake ya Libero kuwa awali aliambiwa uamuzi unaweza kutolewa kabla ya Pasaka lakini sasa itabidi kusubiri hadi mwisho wa msimu.

Beki wa zamani wa Man City Richard Dunne amesema ikiwa mamlaka zinataka kutoa uamuzi inabidi zitoe mapema tena wakati ligi imemalizika au inaanza kwani uamuzi ukifanyika katikati ya msimu muda ambao mbio za ubingwa zitakuwa zimechachamaa inaweza kuleta shida kwani watu watadhani kuna upangaji wa matokeo.

“Wataharibu ushindani wao wenyewe kama wataanza kutoa maamuzi muda ambao ligi imechanganya. Ni bora kusubiri hadi mwisho wa msimu ndio wafanye uamuzi.”