Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal, Man City waweka historia fainali Carabao Cup

Muktasari:

  • Arsenal na Man City zilifanikiwa kuziondoa Chelsea na Newcastle United katika hatua ya nusu fainali na kukutana zenyewe kwenye fainali.

LONDON, ENGLAND: ARSENAL na Manchester City tayari zilikuwa zimeweka historia katika michuano ya Carabao kabla hata ya fainali ya Jumapili iliyopigwa kwenye dimba la Wembley.

Arsenal na Man City zilifanikiwa kuziondoa Chelsea na Newcastle United katika hatua ya nusu fainali na kukutana zenyewe kwenye fainali.

Kabla ya mechi hiyo mara ya mwisho kwa timu hizo kukutana katika Kombe la Ligi ilikuwa mwaka 2018 ambapo kikosi cha Pep Guardiola kilishinda kwa mabao 3-0.

Mechi ya jana ilikuwa na rekodi kibao kabla hata ya kuanza kuchezwa kwani ilikuwa ni mara ya kwanza kwa timu iliyo nafasi ya kwanza kwenye Ligi Kuu England kukutana na timu iliyo nafasi ya pili katika fainali ya Kombe la Ligi.

Arsenal na City kila moja ilipangiwa tiketi 32,000 kwa ajili ya fainali hiyo lakini mchezo huo ulikuwa wa kwanza tangu sheria mpya ya serikali dhidi ya “tailgating” (kuingia uwanjani bila tiketi halali kwa kumfuata mtu mwingine kwa karibu kwenye geti yaani akifungua tu nawe unapita) ianze kutumika.

Sheria hiyo mpya inaelezwa kuwa kufanya hivyo ni kosa kisheria na waliobainika wanaweza kufungiwa kuhudhuria mechi kwa miaka mitano na kutozwa faini hadi pauni 1,000.

Hatua hiyo imechukuliwa kufuatia vurugu zilizotokea Wembley wakati wa fainali ya UEFA Euro 2020 ambapo maelfu ya mashabiki wa England waliingia uwanjani bila tiketi.