Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mashabiki wamgeukia Mbappe, wataka aondoke

MBAPPE Pict

Muktasari:

  • Madrid imekuwa na msimu mbovu ulioshuhudia kocha mpya Xabi Alonso akifutwa kazi Januari mwaka huu baada ya kudumu kwa miezi michache tu tangu aajiriwe akitokea Bayer Leverkusen.

MADRID, HISPANIA: STAA wa Real Madrid, Kylian Mbappe anakabiliwa na presha kubwa kutoka kwa mashabiki wa klabu hiyo ambao wamepiga kura ya kutaka auzwe.

Madrid imekuwa na msimu mbovu ulioshuhudia kocha mpya Xabi Alonso akifutwa kazi Januari mwaka huu baada ya kudumu kwa miezi michache tu tangu aajiriwe akitokea Bayer Leverkusen.

Kwa sasa Madrid inashika nafasi ya pili katika LaLiga ikiwa nyuma kwa pointi 11 dhidi ya wapinzani wao wakubwa Barcelona, ambao wanaweza kuthibitisha ubingwa wao wa ligi kwa ushindi katika mechi ya El Clasico Jumapili.

Wakati Madrid, inaendelea kupitia hali ngumu, Mbappe, 27, naye  anaonekana kupitia wakati mgumu kutokana na mitazamo ya mashabiki ambao wanaona hajaisaidia timu kama walivyotarajiwa.

MBAP 01

Mbappe alionekana katika visiwa vya Sardinia huko Italia akiwa na mchunmba wake Ester Exposito ikiwa ni sehemu ya mapumziko kutokana majeraha ya msuli wa nyuma ya paja  aliyopata.

Safari hiyo ilipingwa vikali na mashabiki ambao wanamwona Mbappe hajali chochote wakati huu klabu ikiwa inapitia nyakati ngumu.

Timu binafsi ya Mbappe ilijibu lawama hizo kupitia taarifa iliyosema kuwa sio kweli kwamba Mbappe haumii kutokana na hali ya timu na kila siku amekuwa akipambana kuhakikisha anarudi mapema na kuisaidia.

Mvutano huo uliongezeka zaidi baada ya ripoti kuibuka zikidai Mbappe aliwahi kuingia katika mabishano na mmoja wa makocha wa timu hiyo.

Gazeti la The Athletic liliripoti kuwa nyota huyo wa Ufaransa “alimzungumzia kwa hasira na kwa lugha ya matusi” na mmoja wa wafanyakazi wa benchi la ufundi wakati wa mazoezi.

MBAP 02

Inaelezwa kuwa tukio hilo limeathiri morali ya wachezaji wengine kwani hajachukuliwa hatua yoyote, pia baadhi ya mastaa nao wamechukizwa na kitendo cha Mbappe kwenda mapumzikoni katika wakati kama huu timu inazama.

Inaelezwa kutokana na mambo hayo, mashabiki wa Madrid wamendaa kampuni rasmi wakichukua saini za mashabiki wanaounga mkono Mbappe kuuzwa na hadi sasa kuna saini za watu wapatao milioni nne waliosaini kutaka fundi huyo apigwe bei.

Mambo yanaweza kuwa mabaya zaidi kwa Mbappe ikiwa matokeo ya El Clasico ya Jumapili yatakuwa ya kupoteza kwani hasira za mashabiki zinaonekana kuwa zote zitahamia kwake.