Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Martinez kuikacha Villa, kutua Chelsea

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Martinez amekuwa nje ya mipango ya Aston Villa tangu klabu hiyo ilipomsajili kipa Zion Suzuki kutoka Parma mapema mwezi huu.

KIPA wa Argentina, Emiliano Martinez anakaribia kujiunga na Chelsea akitokea Aston Villa kwa ada ya pauni7.5 milioni, katika dili ambalo litakuwa la nne kuhusisha klabu hizo mbili katika dirisha hili la usajili.

Martinez amekuwa nje ya mipango ya Aston Villa tangu klabu hiyo ilipomsajili kipa Zion Suzuki kutoka Parma mapema mwezi huu.

Hivyo, Martinez, Lucas Digne, Ollie Watkins na Youri Tielemans  wote kuondoka Villa kabla ya dirisha la usajili kufungwa. Wachezaji hao wanne walikuwa miongoni mwa wanaolipwa mishahara mikubwa zaidi katika kikosi.

Kuondoka kwao kutapunguza mzigo wa mishahara Villa na kuipa nafasi kuingia kwenye usajili wa Nicolas Jackson, Leon Goretzka na, huenda, Rafael Leao.

Villa imetoa ofa ya mshahara kwa Leao ambayo ni ndogo kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na ile ya Galatasaray, lakini klabu hiyo inaamini nafasi ya mshambuliaji huyo wa AC Milan kucheza Ligi Kuu England inaweza kumshawishi kujiunga nayo.

Martinez awali alikaribia kujiunga na Juventus mapema mwezi huu, lakini uhamisho huo ukakwama licha ya Juventus kuwasilisha ofa ya awali ya pauni milioni sita. Kocha wa Villa, Unai Emery alikuwa tayari kuendelea na makipa wake wawili, Suzuki na Marco Bizot, baada ya uhamisho wa Martinez.


RAFAEL LEAO

ASTON Villa imeanza mawasiliano ya moja kwa moja na AC Milan kuhusu mshambuliaji wa pembeni wa Ureno, Rafael Leao, 27, katika harakati za kuipiku Galatasaray kwenye mbio za kumsajili. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 anaendelea kuwa mmoja wa  wanaowindwa katika dirisha hili la usajili.


ROBINIO VAZ

HULL City iko katika hatua za mwisho za kufikia makubaliano na AS Roma kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa, Robinio Vaz, mwenye umri wa miaka 19.


MOISE KEAN

COMO inakaribia kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Fiorentina na timu ya taifa ya Italia, Moise Kean katika dili linaloweza kufikia takriban Pauni 35 milioni. Mazungumzo yanaendelea vizuri, huku Kean akionekana kuwa karibu zaidi kuhamia Como katika dirisha hili la usajili.


ENZO FERNANDEZ

KIUNGO wa Chelsea na timu ya taifa ya Argentina, Enzo Fernandez, 25, bado ana matumaini ya kukamilisha uhamisho wa kujiunga na Manchester City. Fernandez anaendelea kusubiri kuona kama mpango huo utafanikiwa, huku Manchester City ikiwa miongoni mwa klabu zinazohusishwa na uwezekano wa kumsajili.


NICK WOLTEMADE

NAPOLI inafikiria kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Newcastle United na timu ya taifa ya Ujerumani, Nick Woltemade, 24. Klabu hiyo ya Italia imeanza kutathmini uwezekano wa kumchukua Woltemade kwa mfumo wa mkopo katika dirisha hili la usajili.


DANIEL MUNOZ

NOTTINGHAM Forest imewasilisha ofa yenye thamani ya hadi pauni22 milioni kwa ajili ya kumsajili beki wa pembeni wa Crystal Palace na timu ya taifa ya Colombia, Daniel Munoz, 30. Forest imechukua hatua hiyo katika jitihada za kuimarisha kikosi chake kabla ya dirisha la usajili kufungwa.


IGOR JESUS

ATLETICO Madrid inafikiria kumsajili mmoja au wote kati ya washambuliaji wa Brazil, Igor Jesus, 25, wa Nottingham Forest na Gabriel Jesus, 29, wa Arsenal ili kuimarisha safu yake ya ushambuliaji.


ILIMAN NDIAYE

MANCHESTER City imemtaja kiungo mshambuliaji wa Everton, Iliman Ndiaye, 26, kuwa mmoja wa wachezaji wanaolengwa katika usajili, lakini klabu hiyo imemuweka kwenye thamani ya takribani pauni80 milioni. Ndiaye, raia wa Senegal, amekuwa akifuatiliwa na City kutokana na uwezo wake wa kucheza kiungo mshambuliaji.


EXEQUIEL PALACIOS

IPSWICH Town imetangaza kumsajili kiungo wa kimataifa wa Argentina, Exequiel Palacios kutoka Bayer Leverkusen kwa ada ambayo haijawekwa wazi. Palacios, 27, amesaini mkataba wa kuichezea Ipswich Town hadi 2030 na atavaa jezi ya klabu hiyo kuanzia msimu huu.