Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Enzo akoleza moto kutua Manchester City

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Mchezaji huyo amekuwa katika rada za timu mbalimbali wakati huu wa dirisha kubwa la usajili, lakini Manchester City imeonekana kuwa mbali zaidi kuitaka saini yake.

MANCHESTER CITY wako tayari kufikia bei ya Pauni 120 milioni inayotakiwa na Chelsea kwa ajili ya kumsajili kiungo wa Argentina mwenye umri wa miaka 25, Enzo Fernández ambaye inadaiwa kwamba hana furaha kikosini.

Mchezaji huyo amekuwa katika rada za timu mbalimbali wakati huu wa dirisha kubwa la usajili, lakini Manchester City imeonekana kuwa mbali zaidi kuitaka saini yake.

Awali, Enzo alikuwa karibu zaidi kutua Real Madrid pamoja na beki wa zamani wa Chelsea, Marc Cucullera aliyehamia Madrid mwezi mmoja uliopita.

Kwa sasa kinachoelezwa ni kwamba kiungo huyo anasisitiza suala la kuondoka kwake Stanford Bridge lifanyiwe kazi hasa baada ya kumalizika kwa fainali za Kombe la Dunia 2026 ambako kuna nyakati alionekana kuwa na mazungumzo na mawakala wa wachezaji mbalimbali ikielezwa kwamba alikuwa anasuka mipango ya kusepa.

Na katikati ya mjadala juu ya kuondoka kwake inadaiwa kwamba kuna ofa mpya nyingi za fedha, lakini Man City ndiyo inayopambana kutaka kumng’oa ikipanda dau kila uchao. Kwa upande wake Enzo anataka kwenda kuungana na kocha wake wa zamani Chelsea, Enzo Maresca anayeinoa Man City.



Willy Kambwala

BEKI wa kati wa DR Congo, Willy Kambwala, mwenye miaka 21, yuko mbioni kujiunga na Como akitokea Villarreal. Klabu yake ya zamani, Manchester United, inatarajiwa kunufaika kupitia kipengele cha asilimia ya mauzo ya baadaye kilichowekwa kwenye mkataba wake.


Nkunku

NEWCASTLE United na RB Leipzig zinaendelea na mazungumzo na AC Milan kuhusu uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa, Christopher Nkunku, mwenye miaka 28. Timu hizo mbili zinaweza kufanikiwa ikiwa tu Milan itaamua kuachana na mpango wa kumnga’ang’ania mchezaji huyo.


Julian Alvarez

ATLETICO Madrid imekubali kumuuza mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina, Julian Alvarez, kwenda Arsenal, lakini mchezaji huyo mwenye miaka 26 ameendelea kusisitiza anataka kujiunga na Barcelona. Juzi, Alvarez alikumbana na zomeazomea kutoka kwa mashabiki wa Atletico kutokana na suala hilo.


Jules Ahoka

SUNDELAND inadaiwa kufikia makubaliano ya Pauni 4 milioni ili kumsajili kiungo wa timu ya taifa ya DR Congo chini ya miaka 23, Jules Ahoka, mwenye miaka 20, kutoka Royal Antwerp. Nyota huyo ambaye hajawahi kucheza timu yoyote nchini kwao anaweza kutua Englanda wakati wowote.


Victor Osimhen

ARSENAL bado ina nia ya kumsajili mshambuliaji wa Galatasaray, Victor Osimhen, mwenye miaka 27, lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Nigeria atalazimika kupunguza madai yake ya mshahara ili dili hilo litimie. Inaelezwa dai la mshahara mkubwa zaidi ya ule anaoupokea Uturuki linaweza kuwa kikwazo.atakomaa.


Daniel Munoz

NYOTA wa Colombia anayecheza kama beki wa pembeni anayekipiga Crystal Palace, Daniel Munoz, mwenye miaka 30, anahusishwa na uhamisho kwenda Tottenham Hotspur, lakini ripoti zinaeleza kuwa mchezaji huyo ameanza kuwa na shaka kuhusu kujiunga na Spurs.


Wilfried Gnonto

WINGA wa Leeds na timu ya taifa ya Italia, Wilfried Gnonto anaweza kuuzwa katika dirisha hili la usajili ili timu hiyo ipate fedha kwa ajili ya kusajili nyota ambao amekuwa ikipambana kuhakikisha wanatua kikosini.


Nicolas Jackson

CHELSEA inatarajia Aston Villa itawasilisha ofa kwa ajili ya mshambuliaji wake wa kimataifa wa Senegal, Nicolas Jackson, mwenye miaka 25, ambaye imepanga kumuuza kwa Pauni milioni 65. Hata hivyo, mkwanja unaohitajika huenda usikubaliwe na Villa inayomthaminisha kwa bei ya nusu ya hiyo.


Di Gregorio

BOURNEMOUTH iko katika hatua za mwisho za kumsajili kipa wa Juventus, Michele Di Gregorio, mwenye miaka 29, kwa mkopo wenye kipengele cha kumnunua moja kwa moja baadaye. Hata hivyo, iwapo dili litakamilika itabidi Bournemouth ishukuru kwani kumekuwapo na ushindani mkubwa kuinasa saidi ya kipa huyo.