Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bradley Barcola awapa moto Liverpool

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Liverpool imeongeza kasi ya mazungumzo na PSG, huku muda wa dirisha la usajili ukielekea ukingoni. Klabu hiyo ya England imeelekeza nguvu zake kwa Barcola baada ya kushindwa kukamilisha dili la Yan Diomande.

BRADLEY Barcola ameendelea kuipa Liverpool matumaini ya kukamilisha usajili wake baada ya Paris Saint-Germain (PSG) kushusha bei ya mshambuliaji huyo kutoka euro 170 milioni hadi karibu pauni 115 milioni.

Liverpool imeongeza kasi ya mazungumzo na PSG, huku muda wa dirisha la usajili ukielekea ukingoni. Klabu hiyo ya England imeelekeza nguvu zake kwa Barcola baada ya kushindwa kukamilisha dili la Yan Diomande.

Kupunguzwa kwa bei hiyo kunatajwa kuwa hatua kubwa katika mazungumzo, kwani PSG awali ilikuwa imeshikilia dau lake la juu. Liverpool sasa inaamini kuna uwezekano mkubwa wa kufikia makubaliano kabla ya dirisha kufungwa.

Endapo usajili huo utakamilika kwa pauni 115 milioni, Barcola atakuwa mchezaji wa pili ghali zaidi katika historia ya Liverpool, nyuma ya Alexander Isak aliyesajiliwa kwa pauni 125 milioni.

Kwa upande wa mchezaji, masharti binafsi hayatarajiwi kuwa tatizo kubwa, huku maelezo ya awali ya mkataba wa muda mrefu yakiwa tayari yameandaliwa. Barcola pia anaripotiwa kuweka kipaumbele kwenye uwezekano wa kuhamia Anfield.

Liverpool bado inaendelea kutafuta winga wa kulia, lakini Barcola ndiye anayeshikilia nafasi ya juu katika mipango yao kwa sasa. viongozi wa klabu hiyo wanafanya kila linalowezekana kukamilisha dili hilo kabla ya muda wa mwisho.


NICOLAS JACKSON

ASTON Villa imekubaliana na Chelsea kumsajili mshambuliaji wa Senegal, Nicolas Jackson, kwa jumla ya Pauni 65 milioni. Villa italipa Pauni 47.5 milioni mwanzoni, huku makubaliano binafsi yakikamilishwa. Jackson, 25, ataungana tena na Kocha Unai Emery, aliyewahi kumfundisha Villarreal. Usajili huo unatarajiwa kukamilisha safari yake Chelsea na kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji ya Villa.


HONEST AHANOR

CHELSEA inakaribia kumsajili beki wa Atalanta, Honest Ahanor, kwa dau la Euro 40 milioni. Mazungumzo yamepiga hatua na makubaliano binafsi yakitarajiwa kukamilishwa. Ahanor, 18, alicheza mechi 28 za Serie A msimu uliopita na akashiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya. Chelsea inaamini kinda huyo ataongeza nguvu kwenye safu yake ya ulinzi.


OLLIE WATKINS

AL-Hilal ya Saudi Arabia inakaribia kumsajili mshambuliaji wa Aston Villa, Ollie Watkins, kwa dau la zaidi ya Pauni 50 milioni. Watkins anatarajiwa kwenda Saudi Arabia kwa vipimo vya afya kabla ya kusaini mkataba wa miaka mitatu. Villa iko tayari kumuuza baada ya kumpata Nicolas Jackson. Watkins amecheza mechi 278, akifunga mabao 108 na kutoa asisti 47.


LUCA REGGIANI

AC Milan imeingia kwenye mbio na Inter kumsajili beki wa Borussia Dortmund, Luca Reggiani. Beki huyo wa Italia, aliyezaliwa 2008, amepewa Milan kama chaguo la kuimarisha safu yao ya ulinzi. Reggiani alijiunga Dortmund akitokea Sassuolo mwaka 2024 na tayari amecheza mechi tisa za kikosi cha kwanza, akifunga bao moja. Inter pia imekuwa ikimfuatilia.


RAFAEL LEÃO

RAFAEL Leao anakaribia kuondoka AC Milan na kujiunga Galatasaray baada ya klabu hizo kufikia hatua nzuri ya makubaliano ya uhamisho wa Euro 45 milioni. Mazungumzo ya masharti binafsi bado yanaendelea. Leão ameichezea Milan tangu 2019, aliponunuliwa kutoka Lille kwa Euro 49.5 milioni. Tangu wakati huo, amefanya mechi 291, akifunga mabao 80 na kutoa asisti 65.


EDUARDO CAMAVINGA

MANCHESTER United imepanga kuwasilisha ofa ya Pauni 43 milioni kwa Real Madrid kumnasa kiungo Eduardo Camavinga kabla ya dirisha la usajili kufungwa. Camavinga, 23, alijiunga Madrid akitokea Rennes mwaka 2021 na mkataba wake unaendelea hadi 2029. United inataka kuongeza ubora kiungo, huku nafasi ya Camavinga ikiwa finyu chini ya kocha mpya Jose Mourinho.


CHIDO OBI

FEYENOORD haina mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Manchester United, Chido Obi, licha ya kuhusishwa na dili hilo. Mfuatiliaji wa klabu hiyo, Mikos Gouka, amesema Feyenoord tayari ina washambuliaji wa kutosha, hivyo kuongeza kinda mwingine hakutakuwa na maana. Obi, mwenye asili ya Nigeria, aliwahi kuwa Arsenal kabla ya kujiunga Manchester United mwaka 2024. Feyenoord ina Ayase Ueda na Ferri.


ISMAILA SARR

ISMAILA Sarr anaendelea kuhusishwa na uhamisho wa Liverpool, lakini Crystal Palace imeweka wazi kuwa mchezaji huyo hajagoma kufanya mazoezi. Kocha Pierre Sage amesema Sarr ana maumivu ya kinena na kwa sasa anafanya mazoezi binafsi. Liverpool imeonyesha nia ya kumsajili baada ya dili la Yankuba Minteh kuvunjika. Hata hivyo, Sage anatarajia Sarr kubaki Selhurst Park licha ya presha ya uhamisho.


JACK GREALISH

JACK Grealish anaweza kuondoka tena Manchester City baada ya Sunderland kuanza mazungumzo ya kumsajili kwa mkopo. Sunderland inajadili pia uwezekano wa kumnunua moja kwa moja mwakani, huku ikiomba City iendelee kugharamia sehemu ya mshahara wake. Grealish, 30, alicheza kwa mkopo Everton msimu uliopita, akifunga mabao mawili na kutoa assists sita katika mechi 22.