Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Manchester City yamtaka Pedro Neto wa Chelsea

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Neto, mwenye umri wa miaka 26, amekuwa akihusishwa na kuondoka Stamford Bridge dirisha hili la usajili, huku City ikionekana kuwa miongoni mwa klabu zinavyoonyesha nia ya dhati ya kumsajili.

MANCHESTER CITY imeingia katika mbio za kumsajili winga wa Chelsea, Pedro Neto, ambaye thamani yake imewekwa Pauni milioni 70, huku kocha mpya Enzo Maresca akitamani kufanya kazi naye kwa mara nyingine.

Neto, mwenye umri wa miaka 26, amekuwa akihusishwa na kuondoka Stamford Bridge dirisha hili la usajili, huku City ikionekana kuwa miongoni mwa klabu zinavyoonyesha nia ya dhati ya kumsajili.

Endapo dili hilo litakamilika, litamkutanisha tena Neto na Maresca, ambaye amepewa jukumu la kuinoa Manchester City baada ya kurithi mikoba ya Pep Guardiola.

Tayari City imefanya usajili mkubwa kwa kumchukua kiungo Elliot Anderson kutoka Nottingham Forest kwa ada iliyoweka rekodi mpya ya Uingereza ya Pauni milioni 116. Pia imemsajili chipukizi Jeremy Monga kutoka Leicester City.

Hata hivyo, Maresca anaonekana kutoridhika na usajili huo pekee, akimtaja Neto kuwa mmoja wa wachezaji wanaoweza kutekeleza kwa ufanisi mfumo wake wa uchezaji.

Mbali na Manchester City, AC Milan nayo imeonyesha nia kubwa ya kumchukua nyota huyo wa kimataifa wa Ureno.

Mabingwa hao wa Italia wanamwona Neto kama mrithi sahihi wa Rafael Leao, ambaye mustakabali wake ndani ya klabu hiyo unaendelea kuzua maswali.

Hata hivyo, Milan italazimika kwanza kumuuza Leao ili kupata fedha za kukamilisha usajili wa Neto.



Mohamed Salah

Nahodha wa Misri, Mohamed Salah anakaribia kujiunga na Trabzonspor ya Uturuki, huku taarifa zikieleza amebadili uamuzi wake licha ya kuwa awali alikuwa amefikia makubaliano ya mdomo kujiunga na Besiktas. Kwa mujibu wa Foot Mercato, mshambuliaji huyo, 34, sasa anaelekea kuichezea Trabzonspor, hatua inayoweza kuhitimisha sakata la mustakabali wake lililodumu kwa muda mrefu.


Benjamin Sesko

Bayern Munich bado haijaondoa nia yake ya kumsajili mshambuliaji wa Manchester United, Benjamin Sesko, huku ikifuatilia kwa karibu maendeleo ya nyota huyo. Hata hivyo, mabingwa hao wa Bundesliga wanaendelea kumchukulia Harry Kane kama mshambuliaji wao namba moja, huku wakiamini atatia saini mkataba mpya ndani ya mwaka huu.


Ezri Konsa

BEKI wa Aston Villa, Ezri Konsa ameripotiwa kuwa tayari kujiunga na Arsenal endapo miamba hiyo ya London itawasilisha ofa rasmi dirisha hili la usajili. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 anaamini hatua hiyo itampa nafasi ya kupambana katika mashindano makubwa zaidi. Arsenal inaendelea kumfuatilia kwa karibu huku ikitafuta kuimarisha safu yake ya ulinzi kabla ya msimu mpya kuanza.


Franjo Ivanovic

HULL City ipo hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Benfica, Franjo Ivanovic, baada ya mazungumzo kati ya klabu hizo kuingia hatua nzuri. Ripoti zinaeleza mchezaji huyo anatarajiwa kujiunga kwa mkopo, huku kipengele cha usajili wa kudumu kikijadiliwa. Hull inaamini Ivanovic ataongeza nguvu katika safu yao ya ushambuliaji kuelekea msimu mpya.


Mika Godts

PARIS Saint-Germain imeongeza kasi ya harakati za kumsajili winga wa Ajax, Mika Godts, huku Arsenal, Liverpool, Manchester United na Tottenham zikiendelea Mbelgiji mwenye umri wa miaka 21 anathaminiwa kwa Pauni 52 milioni. PSG inaamini inaweza kuwazidi wapinzani wake kwa kuwasilisha ofa itakayoridhisha Ajax kabla ya dirisha la usajili kufungwa.


Giorgio Scalvini

MBIO za kuwania saini ya beki wa Atalanta, Giorgio Scalvini, zimepamba moto baada ya Chelsea na Tottenham kuingia kwenye kinyang’anyiro pamoja na Newcastle United. Hata hivyo, Newcastle ndiyo inayoongoza mbio hizo na inajiandaa kuwasilisha ofa ya Pauni 34 milioni. Atalanta inamthaminisha beki huyo wa Italia, 22, kwa Pauni 42 milioni, hivyo mazungumzo yanatarajiwa kuwa magumu.


Emiliano Martinez

JUVENTUS imepunguza rasmi nia ya kumsajili kipa wa Aston Villa, Emiliano Martinez, baada ya mazungumzo kati ya klabu hizo kushindwa kufikia makubaliano kuhusu ada ya usajili. Tofauti ya thamani iliyowekwa na kila upande imefanya dili hilo kusimama. Kutokana na hali hiyo, Juventus imeamua kujiondoa kwa sasa na kuanza kutafuta chaguo jingine la kuimarisha nafasi ya kipa.



Freddie Potts

CLUB Brugge ipo katika hatua nzuri za mazungumzo ya kumsajili kiungo wa West Ham United, Freddie Potts, kwa ada inayokadiriwa kufikia pauni milioni 10. Kiungo huyo mwenye miaka 22 ni mtoto wa nyota wa zamani wa West Ham, Steve Potts. Pande zote zinaendelea kujadiliana kwa matumaini ya kukamilisha makubaliano kabla ya dirisha la usajili kufungwa rasmi.


Cody Gakpo

TOTTENHAM Hotspur imemweka mshambuliaji wa Liverpool, Cody Gakpo, kwenye orodha ya vipaumbele vyake vya usajili katika dirisha hili. Hatua hiyo imekuja wakati mustakabali wa Mholanzi huyo ukiendelea kuzua maswali baada ya Liverpool kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji. Spurs zinaamini zinaweza kutumia mazingira hayo kumshawishi Gakpo kuhamia London kabla ya msimu mpya kuanza.