Man United haijakata tamaa dili la Myles Lewis-Skelly
Muktasari:
- Lewis-Skelly, mwenye umri wa miaka 19, amekuwa akivutia Manchester United na Chelsea, lakini ameanza katika ushindi wa Arsenal wa mabao 3-0 dhidi ya Manchester City katika Community Shield, pamoja na ushindi wao wa Ligi Kuu dhidi ya Coventry.
MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER United bado ina matumaini ya kushawishi Arsenal kumuuza Myles Lewis-Skelly licha ya kinda huyo kuanza kwenye mechi zake za hivi karibuni.
Lewis-Skelly, mwenye umri wa miaka 19, amekuwa akivutia Manchester United na Chelsea, lakini ameanza katika ushindi wa Arsenal wa mabao 3-0 dhidi ya Manchester City katika Community Shield, pamoja na ushindi wao wa Ligi Kuu dhidi ya Coventry.
Vyanzo vinavyoaminika vimesema nafasi ya Lewis-Skelly kwenye kikosi cha kwanza kwa kiasi fulani imetokana na kusuasua kwa Martin Zubimendi pamoja na kurejea kwa kuchelewa kwa Mikel Merino, ambaye alishiriki kwenye fainali ya Kombe la Dunia ambayo Hispania ilishinda.
Arsenal inamtathmini Lewis-Skelly kwa thamani inayozidi pauni 50 milioni na uwezekano mdogo wa klabu yoyote kufikia bei hiyo umeongeza imani ya Mikel Arteta kwamba ataweza kumbakiza kinda huyo aliyezalishwa katika akademi ya klabu hiyo.
Arteta amesema alikuwa na uhakika wa “asilimia 100” kwamba Lewis-Skelly angebaki Arsenal.
Lewis-Skelly alianza katika mechi mbili pekee za Ligi Kuu kabla ya mwezi wa mwisho wa msimu uliopita, huku Arteta akiwa na mashaka kuhusu ukomavu wake.
Hata hivyo, aliishia kuanza katika mchezo wa mkondo wa pili wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Atletico Madrid, ambao Arsenal ilishinda, kabla ya kuanza pia katika fainali ambayo Arsenal ilipoteza dhidi ya Paris Saint-Germain.
Manchester United inataka kumsajili beki wa kushoto kabla ya muda wa mwisho wa usajili wa saa 11 jioni, Septemba 1, lakini inaona bei ya Lewis-Skelly kuwa kubwa kupita kiasi.
Kinda huyo wa Arsenal mwenye uwezo wa kucheza nafasi mbalimbali anaweza kucheza kama beki wa kushoto na pia kiungo wa kati, nafasi ambayo ameanza msimu huu akiwa na Gunners.
Beki wa kushoto wa Newcastle, Lewis Hall, alikuwa mlengwa mkuu wa Manchester United, lakini Magpies wamechukua hatua za kupunguza tetesi za uwezekano wa uhamisho huo.
Hall, mwenye miaka 21, angependa kuhamia Manchester United, lakini Newcastle tayari imewauza Anthony Gordon, Sandro Tonali na Bruno Guimaraes kwa jumla ya karibu pauni 250 milioni.
Manchester United iliamua kuchelewa kuingia sokoni kumsaka beki wa kushoto baada ya Barcelona kuamua kutotumia chaguo lao la kumnunua Marcus Rashford.
Luke Shaw anaingia katika msimu wake wa 13 akiwa Manchester United na sasa ameingia kwenye mwaka wa mwisho wa mkataba wake, ambao hauna kipengele cha kuongeza mwaka mwingine.
United iko tayari kumuuza beki wake wa kushoto mwenye miaka 19, Harry Amass, ambaye alishiriki katika maandalizi ya msimu mpya, lakini hakufanikiwa hata kuwa kwenye benchi katika kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya Hull City Jumamosi.
Patrick Dorgu, ambaye awali alisajiliwa kama wing back wa kushoto, anaweza pia kucheza kama beki wa kushoto, huku mabeki wa kulia Diogo Dalot na Noussair Mazraoui nao wote wakiwa wamewahi kucheza upande wa kushoto.
United ilifungwa kupitia mipira miwili iliyokufa katika kipigo chake cha kwanza cha Ligi Kuu dhidi ya Hull. Kocha wa Hull, Sergej Jakirović, alifichua kwamba walilenga mfumo wa United katika mipira ya adhabu wakati wa mazoezi yao ya mwisho kabla ya mchezo, Ijumaa.