Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man United inakuja... inakataa!

MAN UTD Pict

Muktasari:

  • Hatua hiyo inatokana na namna inavyofanya usajili, ambapo hadi sasa imeshapigwa bao katika usajili wa mastaa kadhaa waliong'ara msimu uliopita katika timu mbalimbali kwenye Ligi Kuu England akiwamo Elliot Anderson aliyetua Manchester City akitokea Nottingham Forest, Morgan Rogers aliyetokea Aston Villa akitua Chelsea na Jeremy Jacquet aliyetua Man City akitokea Stade Rennais.

MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER United inatarajia kurejea katika Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, sambamba na kupigania mataji mbalimbali ya ndani ya England, lakini kuna jambo ambalo mashabiki wake wanaweza kuanza kufikiria upya itakuwaje?

Hatua hiyo inatokana na namna inavyofanya usajili, ambapo hadi sasa imeshapigwa bao katika usajili wa mastaa kadhaa waliong'ara msimu uliopita katika timu mbalimbali kwenye Ligi Kuu England akiwamo Elliot Anderson aliyetua Manchester City akitokea Nottingham Forest, Morgan Rogers aliyetokea Aston Villa akitua Chelsea na Jeremy Jacquet aliyetua Man City akitokea Stade Rennais.

Kwa ujumla, nyota wengi ambao ingali imekuwa ikiwafukuzia ni ama itakumbana na wakati mgumu au kuwakosa kabisa kutokana na ushindani pamoja na mtindo ilionao kujivutavuta kumaliza dili haraka.

Hadi jana, kikosi hicho chini ya Michael Carrick kilikuwa kimekamisha usajili wa kipa Kit Margetson kutoka Swansea City, Tynan Thompson kutoka Tottenham Hotspur pamoja na viungo Youri Tielemans (Aston Villa) na Andrey Santos (Chelsea).

Hata hivyo, kinachoelezwa ni kwamba wachezaji hao wote hawakuwa katika machaguo yote muhimu ambayo Carrick aliyapendekeza kwa uongozi mara tu baada ya Ligi Kuu England kumalizika msimu uliopita.

MAN 01

Carrick aliyechukua nafasi ya Ruben Amorim mwezi Januari, aliiongoza United kumaliza nafasi ya tatu katika Ligi Kuu England, ikiwa ni mara ya tano tu tangu Sir Alex Ferguson astaafu 2013 kumaliza ndani ya tatu bora.

Pamoja na mafanikio hayo kocha huyo anakabiliana na shida katika utoaji wa fedha za usajili. Lakini, ni maeneo gani ambayo yana ukakasi na ni wapi ambapo wanaweza kutoboa?

Kabla ya dirisha la usajili kufunguliwa, safu ya ulinzi ilionekana kuwa eneo ambalo halikuhitaji maboresho makubwa, na United ina wachezaji wengi wa beki wa kati pamoja na mabeki wa pembeni wenye uwezo wa kucheza nafasi mbalimbali. Hata hivyo, kuna hisia kwamba timu inahitaji kuongeza beki mwingine wa kati.

Sababu kubwa ni kwamba mabeki wawili wanaotegemewa zaidi, Matthijs de Ligt na Lisandro Martinez, wamekuwa wakikumbwa mara kwa mara na majeraha.

De Ligt hajacheza tangu Novemba kutokana na tatizo sugu la mgongo ambalo klabu inaendelea kulisimamia kwa tahadhari kubwa. United imethibitisha tu kwamba atakosa mwanzo wa msimu, bila kutoa muda rasmi wa kurejea kwake.

Kwa upande wa Martinez, naye alipata majeraha katika fainali ya Kombe la Dunia 2026. Ingawa hakuna taarifa rasmi kuhusu ukubwa wa tatizo hilo, historia yake inaonyesha pia amewahi kukaa nje kwa muda mrefu mara kadhaa tangu ajiunge na timu hiyo. Kwa sasa itawategemea zaidi Harry Maguire, Leny Yoro na Ayden Heaven.

Kwa beki wa kushoto, Luke Shaw alikuwa tegemeo kubwa msimu uliopita ndilo tegemeo pekee na iwapo Harry Amass ataondoka kwa mkopo tena, Patrick Dorgu anaweza kuziba nafasi hiyo, ingawa wengi wanaamini anafaa zaidi kucheza mbele.

MAN 02
MAN 02

Diogo Dalot na Noussair Mazraoui pia wana uwezo wa kucheza kushoto inapobidi. Hata hivyo, kama kuna nafasi moja ya beki inayohitaji kuongeza mchezaji, basi ni kushoto hasa kutokana na ratiba ngumu ya msimu mpya ambayo itahusisha pia Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Upande wa viungo United imewasajili Santos na Tielemans, lakini Santos anaonekana kuwa na uwezo mkubwa wa baadaye, huku Tielemans akiwa mmoja wa viungo bora zaidi wa Ligi Kuu England katika miaka ya karibuni, ingawa kwa hadhi ya Man United bado hafikii ubora unaotakiwa, hivyo bado kuna kazi ya kufanya kwani  wengi wanaamini United inahitaji angalau viungo watatu wapya wa kati wenye viwango vikubwa. Ukiondoa wapya waliotua, kwa sasa machaguo mengine yaliyopo ni Kobbie Mainoo na Manuel Ugarte ambaye ni majeruhi.

Kwa viungo washambuliaji ndilo eneo ambalo United inaonekana kuwa na wingi wa vipaji kukiwa na Bruno Fernandes, Bryan Mbeumo, Matheus Cunha na Amad Diallo.

Dorgu pia anaweza kucheza. Zaidi ya hapo, Cunha na Mbeumo wana uwezo wa kucheza pia kama washambuliaji wa kati na pia Marcus Rashford iwapo hataondoka sambamba na Mason Mount kama hataendelea kusumbuliwa na majeraha.

Kwa upande wa mshambuliaji wa kati, inaonekana haiwezekani United kutumia fedha nyingi tena kusajili straika kwani Benjamin Sesko  ameonyesha uwezo wa kutosha katika msimu wake wa kwanza na ataendelea kuaminiwa kuiongoza safu ya ushambuliaji msimu ujao.

Hata hivyo, iwapo hatapata mtu wa kusaidiana naye shida inaweza kuwa kubwa ikizingatiwa kwamba Joshua Zirkzee, ambaye ndiye mbadala wake, bado hajashawishi wengi katika misimu yake miwili Old Trafford, licha ya kuonyesha kiwango kizuri katika ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Rosenborg katika mchezo wa kirafiki majuzi.

Iwapo Zirkzee ataondoka, inaweza kuwa busara kwa United kusajili mshambuliaji mwenye uzoefu zaidi ili kumpa ushindani na msaada Sesko.

Hata hivyo, klabu inaweza pia kuwaamini kina Cunha, Mbeumo na hata Rashford kucheza kama washambuliaji wa kati pale Sesko atakapokosekana, lakini shida inabakia kwa matajiri je watatoa mkwanja kuwezesha chama hilo kuwa na kikosi cha kutisha zaidi msimu ujao? Ni suala la kusubiri na kuona!