Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ndoa ya Aziz KI, Hamisa Mobetto shakani, usaliti watajwa

NDOA Pict


BUNDI ameanza kuganda kwenye ndoa ya mwanamitindo na mwanamuziki Hamisa Mobetto na mumewe kiungo wa Yanga, Stephane Aziz KI, huku sintofahamu ikizua maswali kama wawili hao bado wako kwenye ukurasa mmoja.


Ingawa hakuna maelezo rasmi kutoka kwa Hamisa au Aziz KI kwamba ndoa yao ina shida, kumekuwa na madai yanayozunguka mitandaoni kuhusu wawili hao kupishana na kutokuwa karibu kama ilivyokuwa awali.


Mwanaspoti limezungumza na Hamisa ambaye hakukubali wala kukataa moja kwa moja madai hayo, lakini alikiri kuwa katika ndoa kuna wakati wanandoa wanaweza kupishana.

“Inawezekana watu kupishana, sisi ni binadamu na tumefanikiwa kufunga ndoa, tofauti zipo ndio, lakini sio kweli kama ambavyo mambo yanaelezwa huko mitandaoni sisi bado tupo,”  amesema Hamisa.

NDO 01

Kauli hiyo imezidi kuacha gumzo likiendelea, hasa kutokana na madai kwamba wawili hao wamekuwa na maisha tofauti kwa kipindi hiki.

Hata hivyo, vyanzo vinasema kuwa kiungo huyo mahiri yupo kwenye mchakato wa kuoa mke mwingine hapa hapa jijini Dar es Salaam na tayari ameshazungumza na watu wake wa karibu kuhusu jambo hilo na amepewa baraka zote.

NDO 02

TUHUMA ZA KUSALITIANA

Taarifa kutoka kwa watu wa karibu na wawili hao zinaeleza kuwa moja ya mambo yanayowakabili ni kutuhumiana kuhusu uaminifu, huku kila mmoja akiwa na malalamiko yake.

“Kila mmoja anamtuhumu mwenzake. Ukikutana na Hamisa anakwambia kuna mambo Aziz anayafanya, lakini ukirudi kwa Aziz naye ana madai yake kama hayo na hawako tayari kupata suluhu. Hali sio nzuri,” kilisema chanzo.

Pia kumekuwapo na madai kwamba Hamisa haonekani mara kwa mara kwenye nyumba yao ya Mbezi Beach kama ilivyokuwa awali wakati staa huyo akiwa nje ya nchi, huku Aziz akiendelea kuonekana hapo mara kwa mara kama hayupo mazoezini Yanga.

NDO 03

GUMZO LILIANZA LINI?

Kwa upande wa historia, gumzo kuhusu ndoa yao halikuanza leo wala jana.

Kabla hata hawajafunga ndoa, uhusiano wao ulikuwa umezungukwa na maswali mengi. Februari 10, 2025, Mwanaspoti liliandika kuhusu utata uliokuwepo wakati taarifa za ndoa yao zilipoanza kusambaa, huku baadhi ya watu wakishindwa kuamini kama kweli walikuwa wakielekea kwenye ndoa.

Lakini Februari 16, 2025, mambo yakawa rasmi baada ya wawili hao kufunga Nikah katika Msikiti wa Nnuur, Mbweni, Dar es Salaam.

Siku moja kabla, Februari 15, Aziz KI alitoa mahari iliyotajwa kuwa ng’ombe 30 na Sh30 milioni, kabla ya sherehe kubwa kufanyika Februari 19 katika Ukumbi wa SuperDome, Masaki.

NDO 04

MWANZO WA NDOA

Baada ya ndoa, wawili hao waliendelea kuonyesha ukaribu wao hadharani. Mei 2025, Hamisa alimuunga mkono Aziz KI wakati akihamia Morocco kujiunga na Wydad, akimueleza kama mume wake, rafiki yake mkubwa na shabiki wake namba moja.

Hata hivyo, baadaye zilianza kujitokeza tafsiri mbalimbali kuhusu ukaribu wao.

Desemba 2025, tayari kulikuwa na gumzo la mita ndaoni kuhusu uwezekano wa kutengana, lakini Hamisa alionekana tena akiwa na Aziz KI, jambo lililopunguza kwa muda hofu za mashabiki.

Februari 2026, wawili hao pia walisherehekea mwaka mmoja wa ndoa yao, huku Aziz KI akimfanyia Hamisa ‘surprise’ ya zawadi kubwa.

NDO 05

SASA NINI KINAENDELEA?

Licha ya historia hiyo, Juni 2026 zilianza kusambaa zaidi video zilizodai kuwa wawili hao wameachana. Hata hivyo, madai hayo hayakuambatana na tangazo rasmi kutoka kwa wanandoa hao. Ndiyo maana kauli ya sasa ya Hamisa inakuwa muhimu zaidi.

Akiwa hakubali simulizi kwamba mambo yao yamefika mwisho, lakini pia akikiri kuwa kuna tofauti, amewaacha mashabiki wakisubiri kama hali hiyo itamalizika kwa suluhu au itazaa uamuzi mwingine. Kwa sasa, hakuna uthibitisho rasmi kwamba ndoa hiyo imevunjika.

Kinachobaki ni sintofahamu, madai ya watu wa karibu na mabadiliko yanayoonekana kwenye maisha yao ya hadharani.

Na kwa ndoa iliyotikisa nchi kwa ukubwa wa sherehe yake mwaka 2025, macho ya mashabiki sasa yameelekezwa kwa Hamisa na Aziz KI kuona kama wataumaliza mgogoro huo kwa suluhu au huu utakuwa mwanzo wa sura nyingine katika ndoa yao.