Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man United iko siriazi kwa Lewis-Skelly

Muktasari:

  • Lewis-Skelly ambaye ni zao la akademi ya Arsenal amekuwa na kiwango bora katika kikosi hicho cha Washika Mitutu wa London, ambapo msimu uliopita alikuwa akiingia kwenye kikosi cha kwanza kila mara na hivyo kutishia uhakika wa mastaa wakongwe wa timu hiyo.

MANCHESTER United ina imani ya kuishawishi Arsenal ili kuiuza mchezaji wake wa kiungo, Myles Lewis-Skelly, 19, licha ya bei ya zaidi ya Pauni 50 milioni kuonekana kuwa kikwazo katika dili la mchezaji huyo wa England anayeweza kucheza pia kama beki wa kushoto.

Lewis-Skelly ambaye ni zao la akademi ya Arsenal amekuwa na kiwango bora katika kikosi hicho cha Washika Mitutu wa London, ambapo msimu uliopita alikuwa akiingia kwenye kikosi cha kwanza kila mara na hivyo kutishia uhakika wa mastaa wakongwe wa timu hiyo.

Hata hivyo, tangu kuanza kwa dirisha la usajili msimu huu, mchezaji huyo amekuwa akitajwa mara kwa mara kuwa katikati ya mijadala ya timu mbalimbali Ulaya, akihusishwa na vigogo vya Italia, AC Milan pamoja na Inter Milan ambavyo vinadaiwa kwamba vimekuwa vikimmezea mate ili kumsajili.

Lakini, watu wa karibu na Lewis-Skelly wanadaiwa wamekuwa wakisukuma taarifa za kutakiwa kwake na timu kubwa ili kutengeneza mazingira ya kuboreshewa maslahi na pia mkataba ambao unamalizika ifikapo Juni 30, 2030.

Wakati Manchester United ikiwa ni miongoni mwa timu kubwa ya karibuni kujitosa kumtaka mchezaji huyo, taarifa kutoka Hispania zinadai pia Barcelona na Real Mallorca zimeulizia juu ya upatikanaji wake katika dirisha hili, na zinasikilizia iwapo zitaweza kumpata.


Matias Fernandez-Pardo

NEWCASTLE United imewasilisha ofa ya Pauni 34.2milioni bila kujumuisha bonasi kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Lille na timu ya taifa ya Ubelgiji, Matias Fernandez-Pardo, 21 katika dirisha hili la usajili. Fernandez-Pardo anaitamanisha Newcastle akaongeze nguvu katika eneo la mbele lililopo chini ya Mkongomani Yoane Wissa.


Alex Scott

CHELSEA inadaiwa kukataliwa ofa zake tatu katika dirisha hili za kumsajili kiungo wa Bournemouth na timu ya taifa ya England, Alex Scott, 23. Scott anadaiwa kuwa tayari kuondoka katika timu yake kutokana na vita ya namba iliyopo kwa sasa.


Ilyas Ansah

HULL City imewasilisha ofa ya Pauni 17.9 milioni kwa mshambuliaji wa Union Berlin na timu ya Ujerumani ya vijana chini ya miaka 21, Ilyas Ansah, huku mazungumzo kuhusu mkataba wa muda mrefu yakiwa yamefikia hatua za juu.


Noussair Mazraoui

AC Milan inafikiria kupambana ili kufanya uhamisho wa dakika za mwisho kabla ya dirisha kufungwa kumsajili beki wa Manchester United na timu ya taifa ya Morocco, Noussair Mazraoui, 28. Beki huyo ni miongoni mwa mastaa walio na uhakika wa namba United.


Dele Alli

MONZA inadaiwa kuwa katika hatua za mwisho za kumpa mkataba wa mwaka mmoja kiungo wa zamani wa Tottenham Hotspur na timu ya taifa ya England, Dele Alli, 30. Mchezaji huyo hana timu kwa sasa tangu alipoondoka Como, Septemba 2025.


Edson Alvarez

OLYMPIACOS inadaiwa kuwasilisha ofa ya kumchukua kwa mkopo kiungo wa West Ham United, Edson Alvarez. Hammers tayari inadaiwa kuwa imefikia makubaliano na Real Sociedad kuhusu mchezaji huyo mwenye wa miaka 28, lakini klabu hiyo ya Ugiriki inamtaka nahodha huyo wa Mexico.


Sorba Thomas

STOKE City imekataa ofa kutoka Hull City kwa ajili ya kumsajili winga Sorba Thomas. Potters wamekataa ofa ya karibu Pauni 7 milioni kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Wales mwenye umri wa miaka 27 ambaye amekuwa na panda shuka kikosini kwake.


Pavel Sulc

WREXHAM iko tayari kuvunja rekodi yake ya usajili katika harakati za kumsajili kiungo wa Lyon, Pavel Sulc. Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Czech alifunga mabao 11 katika Ligi Kuu Ufaransa msimu uliopita.


Zach Abbott

PRESTON North End inavutiwa na uwezekano wa kumsajili kwa mkopo beki wa Nottingham Forest, Zach Abbott, ambapo mchezaji huyo mwenye miaka 20 amecheza mechi 11 za kikosi cha kwanza cha Forest na pia anaripotiwa kuwa kwenye orodha ya wachezaji wanaolengwa na Watford.