Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man City wamvizia Pedro Neto

PEDRO Pict

Muktasari:

  • Kocha mpya wa City, Enzo Maresca, ambaye aliwahi kufanya kazi na Neto akiwa Chelsea, anaaminika kumkubali sana mchezaji huyo kutokana na kiwango na uwezo wake wa kushambulia.

MANCHESTER, ENGLAND: LICHA ya dirisha la usajili kuendelea kupamba moto, mabingwa wa England, Manchester City, wameanza kupanga maisha baada ya kuondoka kwa baadhi ya wachezaji wao wa pembeni kwa kumweka nyota wa Chelsea, Pedro Neto, kwenye rada zao.

Ripoti zinaeleza kuwa City wanamwona Neto, mwenye umri wa miaka 26, kama mmoja wa winga wanaoweza kuziba nafasi endapo Savinho ataondoka kuelekea Tottenham. Kabla ya Neto kujiunga na Chelsea akitokea Wolves kwa pauni 51 milioni, City walikuwa tayari wakimfuatilia.

Kocha mpya wa City, Enzo Maresca, ambaye aliwahi kufanya kazi na Neto akiwa Chelsea, anaaminika kumkubali sana mchezaji huyo kutokana na kiwango na uwezo wake wa kushambulia.

PED 01

Mbali na Neto, City pia wanawafuatilia vijana Ibrahim Mbaye wa Paris Saint-Germain na Yan Diomande wa RB Leipzig kama sehemu ya mipango yao ya kuimarisha kikosi.

Hata hivyo, City wameonyesha pia kuvutiwa na beki wa kulia wa Chelsea, Malo Gusto, lakini wanaona thamani ya pauni 75 milioni inayotajwa na Chelsea kuwa kubwa mno.

Kwa upande wa Chelsea, tayari wamemuuza Alejandro Garnacho kwenda Aston Villa, huku klabu hiyo pia ikionesha nia ya kumsajili mshambuliaji Nicolas Jackson. Aidha, Chelsea wanaendelea kufanya kazi ya kumsajili winga Kerim Alajbegovic kutoka Bayer Leverkusen.

PED 02

Akizungumza baada ya kutambulishwa rasmi kama kocha wa Manchester City, Maresca amesema anaamini mafanikio aliyoyapata Leicester City na Chelsea yanampa msingi mzuri wa kuiongoza City.

"Nimekuwa na bahati kufanya kazi katika klabu zenye utambulisho mzuri wa soka kama Leicester na Chelsea. Tulifanya kazi nzuri katika timu zote mbili na ninafurahia kuwa sehemu ya historia hiyo," amesema Maresca.