Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mambo manne kumbeba Amorim

AMORIM Pict

Muktasari:

  • Man United itakwenda Marekani wiki hii kucheza mechi tatu za kirafiki ikiwa ni maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu England.

SOLNA, SWEDEN: RUBEN Amorim atakuwa na muda wake wa kwanza kuwa na pre-season nzima kwenye kikosi cha Manchester United tangu alipokuwa kocha wa timu hiyo ya Old Trafford.

Man United itakwenda Marekani wiki hii kucheza mechi tatu za kirafiki ikiwa ni maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu England.

Mchezo wa kwanza, Man United itakipiga na West Ham uwanjani MetLife, kisha Bournemouth huko Chicago kabla ya kumaliza na Everton huko Atlanta. Itakipiga na Fiorentina uwanjani Old Trafford kabla ya msimu kuanza.

Man United tayari imeshaanza mechi zake za pre-season, ilipotoka sare ya 0-0 na Leeds United huko Stockholm, Sweden Jumamosi iliyopita. Katika mechi hiyo, mashabiki waliona matatizo kadhaa, ambayo kocha Amorim anapaswa kuyapatia ufumbuzi kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa 2025-26.

Wakati kikosi hicho kikijiandaa na mechi tatu za huko Marekani, kuna mambo manne ambayo kocha Amorim anapaswa kuyapatia ufumbuzi mapema.

AM 01

1. Kufunga mabao; Man United ilimaliza msimu uliopita kwa kufunga mabao 44 tu kwenye Ligi Kuu England. Kuna timu nne tu ndizo zilizofunga mabao machache kuzidiwa na Man United, lakini suala la kufunga ndilo linalopaswa kumalizwa.

Mastaa wapya Matheus Cunha na Bryan Mbeumo watakuwa na kazi kubwa ya kufunga mabao, huku Amorim akitambua wazi anapaswa kusajili Namba 9 mpya kuja kuboresha fowadi yake baada ya Rasmus Hojlund na Joshua Zirkzee kushindwa kufanya kweli.


AM 02

2. Kupata ubora wa Cunha; Licha ya Man United kutoka kapa dhidi ya Leeds wikiendi iliyopita ikiwa na huduma ya Cunha uwanjani, kocha Amorim alifurahishwa na kiwango cha Mbrazili huyo kuwa na muunganiko mzuri na kiungo Bruno Fernandes.

Amorim alifurahishwa na namna Cunha alivyocheza kwenye mechi hiyo, akidai ndicho kitu ambacho Man United ilikuwa inakikosa na sasa kazi yake ni kuhakikisha mkali huyo ubora wake unazidi kuwa juu kwenye kikosi chake ili kumpungumzia mzigo Fernandes.


AM 03

3. Kuboresha safu ya ulinzi; Safu ya ulinzi ni eneo la ndani ya uwanja ambalo Man United inahitaji kuliimarisha zaidi, hasa kutokana na kocha Amorim kupendelea kutumia mfumo wa mabeki watatu wa kati, akitaka wasaidiwe na wing-back wawili.

Kitu kingine ambacho Amorim ataomba ni kuona mabeki wake wakikaa mbali na majeraha msimu huu, lakini ujio wa Diego Leon, kurejea kwa Lisandro Martinez na Luke Shaw kutampa machaguo mengi tofauti kocha Amorim akiwa na mabeki watano wa kati.


AM 04

4. Kuimarisha safu ya kiungo; Wapinzani wamekuwa wakipata wepesi sana kwenye safu ya kiungo ya Man United inapocheza na timu hiyo hasa kwa msimu uliopita na hilo kocha Amorim analifahamu wazi. Casemiro alirejea kwenye ubora wake msimu uliopita, lakini umri wake ni miaka 33, hivyo huwezi kumtegemea kwenye kila mechi.

Manuel Ugarte hakuwa na msimu mzuri, Kobbie Mainoo naye hakuwa vizuri na Mason Mount naye alisumbuliwa sana na majeraha ya mara kwa mara. Usajili wa Cunha na Mbeumo hiyo ina maana Casemiro na Fernandes watacheza kwenye kiungo ya chini, lakini hakuna ubishi, Amorim anahitaji kiungo mwingine kwenye eneo hilo.