Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mambo magumu FIFA, Infantino akalia kuti kavu!

FIFA Pict

Muktasari:

  • Jambo lililomuumiza zaidi Infantino ni kuona hata baadhi ya nchi zilizokuwa washirika wake wakubwa ndani ya Shirikisho la Soka Asia (AFC) zikianza kujitenga naye.

LONDON, ENGLAND: Katika siasa za mpira wa miguu, wiki moja inaweza kubadilisha kila kitu.

Jumanne asubuhi, Gianni Infantino alikuwa katika nafasi salama kama rais wa FIFA, akiwa ndiye mtu mwenye nguvu zaidi katika uongozi wa soka duniani.

Lakini sasa, baada ya jaribio lake la kutafuta wawekezaji binafsi watakaomiliki sehemu ya mashindano ya FIFA, mpango ambao inaelezwa ulifanyika bila uelewa wa baadhi ya viongozi wakuu wa taasisi hiyo, nafasi yake imeanza kuyumba.

Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA), ambalo limekuwa mkosoaji mkubwa wa Infantino, lilitoa pigo kubwa Alhamisi baada ya kutishia kususia mashindano yote ya FIFA, ikiwemo Kombe la Dunia.

Sasa UEFA inaona kuna nafasi ya kipekee ya kumuondoa Infantino madarakani, na huenda hii ikawa fursa bora zaidi ambayo imewahi kupata.

FIFA01

LAKINI UEFA SI TAASISI PEKEE YENYE MALALAMIKO.

CONCACAF, shirikisho ambalo Infantino alishirikiana nalo kwa karibu katika maandalizi ya Kombe la Dunia 2026, limetaka kufanyika kwa "mapitio kamili" ya uongozi wa FIFA kutokana na mpango huo wa uwekezaji.

Jambo lililomuumiza zaidi Infantino ni kuona hata baadhi ya nchi zilizokuwa washirika wake wakubwa ndani ya Shirikisho la Soka Asia (AFC) zikianza kujitenga naye.

Baadaye alipoteza pia uungwaji mkono kutoka kwa baadhi ya wasaidizi wake wa karibu, akiwemo mshauri mkuu Carlos Cordeiro na afisa mkuu wa uendeshaji Kevin Lamour.

Baada ya Infantino kubadili msimamo wake katika saa za mwanzo za Jumamosi, UEFA ilitoa taarifa nyingine nzito ikisema imepoteza imani na uongozi wake.

Sasa mistari ya vita imechorwa. Swali kubwa ni: nini kinaweza kutokea baadaye?

FIFA02

INFANTINO ANAWEZA KUONDOLEWA VIPI?

Njia rahisi na ya haraka zaidi kwa Infantino kuondoka madarakani ni kujiuzulu mwenyewe, kama alivyofanya mtangulizi wake Sepp Blatter mwaka 2015.

Hata hivyo, Infantino bado ana uungwaji mkono kutoka baadhi ya maeneo na anaweza kuamua kusimama hadi Machi, ambapo anatarajiwa kugombea muhula wake wa nne na wa mwisho kama rais wa FIFA.

Njia nyingine ni Baraza la FIFA kujaribu kumlazimisha kuchukua hatua kupitia kikao cha dharura.

Kikao hicho kinaweza kuitishwa endapo wajumbe 19 kati ya 37 wa Baraza la FIFA wataomba kufanyika kwake.

UEFA ina wajumbe tisa, AFC saba, CONCACAF watano, Afrika sita, CONMEBOL watano na Oceania watatu, huku wajumbe wengine wakiwa Infantino mwenyewe na katibu mkuu Mattias Grafstrom.

Hata hivyo, kuna shaka kama idadi hiyo ya kura 19 inaweza kufikiwa.

Iwapo itafikiwa, kikao hicho lazima kifanyike ndani ya wiki mbili, na Baraza la FIFA linaweza kumtaka Infantino kuwasilisha barua ya kujiuzulu. Lakini kisheria anaweza kukataa.

Pamoja na hilo, hatua hiyo ingeongeza presha kubwa zaidi juu yake.

Hatua inayofuata ingekuwa kuitisha kongamano maalumu la wanachama wote 211 wa FIFA.

FIFA03

Kongamano hilo linaweza kuitishwa ikiwa vyama 43 vya soka (moja ya tano ya wanachama wote) vitaomba rasmi kwa maandishi.

UEFA, ikiwa na vyama 55, inaweza kuanzisha mchakato huo wakati wowote.

Mchakato huo ungechukua angalau miezi miwili hadi mitatu, na bado hakuna uhakika wa mafanikio.

Kwa vitendo, ingekuwa kama uchaguzi mpya bila kuwa na mgombea mwingine, kwani kura 106 zingehitajika kupitisha kura ya kutokuwa na imani na rais.

UEFA ina kura 55, Afrika 54, Asia 46, CONCACAF 35, Oceania 11 na CONMEBOL 10.

Hadi sasa, Afrika, CONMEBOL na Oceania hazijakosoa mpango wa Infantino.

Hivyo swali kubwa linabaki: Je, UEFA inaweza kufikisha kura 106?

Ingawa nchi 136 zilikataa rasmi mpango wa uwekezaji huo, kupinga wazo fulani si sawa na kupiga kura ya kumuondoa rais.

Kwa mfano, Qatar tayari imesema inamuunga mkono Infantino, huku Mexico ikijitenga na taarifa ya pamoja ya CONCACAF.

Nani anaweza kumpinga Infantino?

Hatua nyingine muhimu ni kumpata mgombea mwenye uwezo wa kushindana naye katika uchaguzi wa Machi.

Infantino alichaguliwa bila mpinzani mwaka 2019 na 2023, lakini safari hii hali inaweza kuwa tofauti.

Mtu yeyote anayetaka kupambana naye katika uchaguzi wa urais wa FIFA lazima atangaze nia yake kabla ya tarehe 18 Novemba.

Kwa sasa, vita vya madaraka ndani ya FIFA vimeanza rasmi, na miezi ijayo inaweza kuamua hatma ya mmoja wa viongozi wenye ushawishi mkubwa zaidi katika historia ya soka duniani.