Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Madrid, Liverpool yafungua mazungumzo dili la Rodrygo

FUNUNU Pict

LIVERPOOL wamefanya mazungumzo ya awali na Real Madrid kuhusu winga wa klabu hiyo na timu ya taifa ya Brazil Rodrygo, mwenye umri wa miaka 24.

Mabosi wa Liverpool wanamwangalia fundi huyu kama mbadala wa Luis Diaz ambaye kuna uwezekano mkubwa akaondoka katika dirisha hili.

Rodrygo inadaiwa kutaka kuondoka katika dirisha hili kwa sababu haoni kama yupo kwenye mipango ya kocha mpya Xabi Alonso ambaye amempa muda mchache wa kucheza katika michuano ya Kombe la Dunia la Klabu.

Inaelezwa Madrid ipo tayari kumuuza staa huyu lakini kwa ada ya uhamisho isiyopungua Pauni 70 milioni kiasi ambacho Liverpool imeomba kipunguzwe.

Mabingwa hao wa Ligi Kuu England tayari wameshafanikisha usajili wa Florian Wirtz ambaye amewagharimu takriban Pauni 120 milioni, hivyo hawataki kutumia kiasi kikubwa cha pesa kwake kwani bado ina mahitaji mengine ikiwemo kusajili straika.

Mbali ya Liverpool saini ya Rodrygo pia inahitajika sana na Bayern Munich, pia wababe hao wa Ujerumani wamerudi nyuma kutokana na kiasi cha pesa kinachohitajika kama ada yake ya uhamisho.


Ademola Lookman

INTER Milan imetuma maombi ya kutaka kumchukua mshambuliaji wa Atlanta na timu ya taifa ya Nigeria, Ademola Lookman kwa mkopo ambao utakuwa na kipengele ambacho kitawawezesha  kumnunua mazima kwa Pauni 36 milioni mwisho wa msimu ikiwa itaridhishwa na kiwango chake. Hata hivyo, ofa hiyo inaripotiwa kukataliwa na Atalanta ambayo imesisitiza inataka kumuuza mazima staa huyo mwenye umri wa miaka 27 na ada yake ya uhamishi ni Pauni 43 milioni.


Josh Keeley

LUTON Town iko mbioni kumsajili kipa wa Tottenham na Jamhuri ya Ireland, Josh Keeley dirisha hili baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 kushindwa kukubaliana na Spurs kuhusu mkataba mpya. Staa huyu ambaye mara kadhaa alionekana katika kikosi cha wakubwa licha yakuwa alisajiliwa katika kikosi cha vijana, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2027. Anataka kuondoka ili kupata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza.


Evan Ferguson

AS Roma inadaiwa kuwa katika hatua nzuri kwenye mazungumzo yao na Brighton kwa ajili ya kuipata saini ya na mshambuliaji wa klabu hiyo na timu ya taifa ya Jamhuri ya Ireland, Evan Ferguson mwenye umri wa miaka 20. Evan ambaye awali aliwahi kuhusishwa na Man United ameonyesha nia ya kutaka kuondoka kwenda Roma kwa ajili ya kupata changamoto mpya. Mkataba wake unamalizika mwaka 2028.


Giorgio Scalvini

NEWCASTLE imeweka mikakati ya kusuka upya safu yao ya ulinzi na tayari Kocha Eddie Howe amewasilisha majina ya mabeki ambao anaona wataongeza nguvu, beki wa Juventus, Nicolo Savona, 22, na wa Atalanta, Giorgio Scalvini, 21, dirisha hili. Howe anataka kujihakikishia wanafanya vizuri michuano ya kimataifa msimu ujao na sasa anaona ameshafanikisha maboresho kwenye eneo la ushambuliaji.


Rasmus Hojlund

AC Milan bado inapambana kutaka kumsajili mshambuliaji wa Manchester United, Rasmus Hojlund, dirisha hili. Milan imekuwa ikiimezea mate saini ya Hojlund tangu dirisha la majira ya baridi mwaka huu. Staa huyu pia ni miongoni mwa wachezaji ambao kocha Ruben Amorim haridhishwi sana na utendaji kazi wao na ndiyo maana amependekeza asajiliwe straika mwingine katika dirisha hili kwa ajili ya kuboresha zaidi eneo hilo.


Jack Grealish

WEST Ham ni miongoni mwa klabu zilizowasiliana na Manchester City kutaka kumsajili winga wa timu hiyo, Jack Grealish, dirisha hili. Grealish pia inawindwa na Everton ambayo inataka kumchukua kwa mkopo. Man City inataka kumuuza Grealish na tayari kocha Pep Guardiola ameshamwambia kuwa hana nafasi katika kikosi chake hivyo atafute timu.


Bafode Diakite

INAELEZWA Lille imekataa ofa kutoka Sunderland na Bournemouth zinazohitaji saini ya beki wao, Bafode Diakite, 24, dirisha hili. Ofa hizo zilizowasilishwa hivi karibuni na inadaiwa timu zote zinaripotiwa kuwasilisha ofa Pauni 23 milioni. Lille imeziambia timu hizi ipo tayari kumuuza Diakite lakini inahitaji kiasi kisichopungua Pauni 34 milioni kama ada yake ya uhamisho.