Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mabosi Bayern Munich watua kwa Luis Diaz

TETESI Pict

Muktasari:

  • Ripoti zinaeleza Bayern imehamia kwa staa huyu wa kimataifa wa Colombia baada ya kuikosa huduma ya Nico Williams ambaye amesaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia Athletic Bilbao.

IMEFICHUKA Bayern Munich imewasilisha ombi kwenda Liverpool ili kumnunua winga wao Luis Diaz, mwenye umri wa miaka 28, katika dirisha hili.

Ripoti zinaeleza Bayern imehamia kwa staa huyu wa kimataifa wa Colombia baada ya kuikosa huduma ya Nico Williams ambaye amesaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia Athletic Bilbao.

Kwa mujibu wa tovuti ya Bild, Bayern imewasilisha ofa inayofikia Euro 52 milioni mapema wiki hii lakini hadi sasa bado haijapata majibu kutoka Liverpool.

Hata hivyo, ofa hiyo haionekani inaweza kuishawishi Liverpool kumuuza kwani ni ndogo tofauti na ile inayodaiwa kuhitaji ya kuanzia Euro 70 milioni.

Luiz ambaye ni mmoja wa wachezaji tegemeo katika kikosi cha Liverpool, amekuwa akihusishwa kuondoka tangu mwaka jana na Barcelona ndiyo iliripotiwa kuwa karibu zaidi.

Kwa sasa Barca haionekani kuwa na mpango wa kumsajili licha ya kwamba hiyo ndiyo ilikuwa ni timu ya ndoto yake.

Mkataba wa sasa wa staa huyu unatarajiwa kumalizika mwaka 2027.


Yoane Wissa

MABOSI wa Brentford wameitupilia mbali ofa nyingine ya Nottingham Forest waliyoiwasilisha kwa ajili ya kumnunua mshambuliaji wao  Yoane Wissa mwenye umri wa miaka 28, katika dirisha hili. Taarifa zinaeleza ofa hiyo ipo chini ya Pauni 25 milioni. Brentford ipo tayari kumuuza fundi huyu lakini kwa kiasi cha pesa kisichopungua Pauni 50 milioni.


Hugo Ekitike

Liverpool iko tayari kuanza mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt na timu ya taifa ya Ufaransa, Hugo Ekitike, mwenye umri wa miaka 23, dirisha hili. Hata hivyo, kabla ya kumsajili Ekitike, majogoo hawa watalazimika kwanza kumuuza  mshambuliaji wao wa kimataifa wa Uruguay Darwin Nunez, 26, ambaye anawindwa na Napoli.


Viktor Gyokeres

DILI la Arsenal kumsajili straika wa Sporting Lisbon, Viktor Gyokeres linaonekana kwenda kufeli baada ya ripoti kufichua timu hizo mbili hazijawasiliana kwa siku ya tatu sasa tangu wawakilishi wa timu zote wakutane Ureno kujadili ada ya uhamisho na kutofikia mwafaka. Staa huyu wa kimataifa wa Sweden mwenye umri wa miaka 27, anatamani sana kuondoka na ameshawaambia vigogo wa Sporting juu ya hilo.


Alejandro  Garnacho

NAPOLI ipo tayari kulipa karibia Pauni 45 milioni kwenda Manchester United kwa ajili ya kuipata saini ya mshambuliaji wa mashetani hao na timu ya taifa ya Argentina, Alejandro  Garnacho dirisha hili. Garnacho ni miongoni mwa wachezaji ambao Man United ipo tayari kuwauza dirisha hili kwa sababu hawapo kwenye mipango ya kocha Ruben Amorim.


Rodrygo

MABOSI wa Real Madrid wako tayari kumruhusu winga wa timu hiyo, Rodrygo aondoke dirisha hili lakini itamwacha mwenyewe afanye uamuzi wa timu gani anataka kujiunga nayo katika dirisha hili. Rodrygo mwenye umri wa miaka 24, bado anatamani kuendelea kusalia Ulaya licha ya uwepo wa ofa za Saudi Arabia. Liverpool ni miongoni mwa timu zinazohitaji huduma yake.


Dani Ceballos

KATIKA dirisha hili, Real Madrid imewaweka sokoni mastaa wake wawili ambao ni pamoja na kiungo wao wa kimataifa wa  Hispania Dani Ceballos, 28, na kiungo wa timu ya taifa ya Morocco, Brahim Diaz, 25, ambao kocha wao mpya, Xabi Alonso inadaiwa hawapo katika mipango yake. Madrid inahitaji kiasi kisichopungua Pauni 40 milioni kwa kila mmoja wao na hadi sasa bado haijapokea ofa yoyote.


Ousmane Diomande

CRYSTAL Palace ipo katika mazungumzo na Sporting Lisbon kwa ajili ya kumsaji beki wa kati wa timu hiyo na Ivory Coast, Ousmane Diomande, mwenye umri wa miaka 21, dirisha hili. Sporting ipo tayari kumuuza Diomande ambaye pia anahusishwa na vigogo mbalimbali Ulaya lakini inahitaji kiasi kisichopungua Pauni 45 milioni kama ada ya uhamisho.