Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Liverpool yafikia patamu kwa Hugo Ekitike

TETESI Pict

Muktasari:

  • Liverpool imehamia kwa Ekitike na inapambana kumsajili baada ya kushindwa kuipata saini ya straika wa Newcastle United, Alexander Isak ambaye  ndio ilikuwa lengo lao la kwanza.

MABOSI wa Liverpool wamewasilisha ofa ya Pauni 69 milioni pamoja na nyongeza itakayofikia Pauni 78 milioni kwenda Eintracht Frankfurt kwa ajili ya kumsajili straika wa klabu hiyo na timu ya taifa ya Ufaransa, Hugo Ekitike mwenye umri wa miaka 23.

Liverpool imehamia kwa Ekitike na inapambana kumsajili baada ya kushindwa kuipata saini ya straika wa Newcastle United, Alexander Isak ambaye  ndio ilikuwa lengo lao la kwanza.

Kwa mujibu wa ripoti, Frankfurt inahitaji takribani Euro 100 milioni kama ada ya uhamisho wa Ekitike na Liverpool inaonekana kuwa tayari kutoa kiasi hicho cha pesa.

Ripoti zinaeleza Ekitike pia alikuwa katika mipango ya kocha wa Newcastle, Eddie Howe aliyehitaji kuipata saini yake katika dirisha hili ili akamchezeshe pamoja na Isak na Anthony Elanga.

Mambo yaliharibika baada ya kugoma kumuuza Isak kwenda Liverpool na kwa sababu hiyo, majogoo hao wakaamua kumgeukia Ekitike na ushawishi wao unaonekana kuwa mkubwa zaidi.

Mkataba wa Ekitike unatarajiwa kumalizika mwaka 2029, na msimu uliopita alicheza mechi 48 za michuano yote na kufunga mabao 22.

Mbali ya kiasi hicho cha pesa cha ada ya uhamisho, mabosi wa Liverpool pia wamempa Ekitike ofa ya mshahara wa karibia Pauni 200,000 kwa wiki.


Pierre-Emerick Aubameyang

AL-Ettifaq ya Saudi Arabia inadaiwa kuwasilisha ofa kwa wawakilishi wa mshambuliaji wa kimataifa wa Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang, 36, mara baada ya kuona ameachana na Al-Qadsiah. Hata hivyo, licha ya ofa hiyo nono iliyowekwa mezani, Aubameyang inadaiwa kukataa na kusisitiza anahitaji kurudi Ulaya na kujiunga na Marseille  ili kucheza soka la kiushindani. Msimu uliopita alicheza mechi 36 za michuano yote na kufunga mabao 21.


Raheem Sterling

CHELSEA inataka kumuuza winga wao raia wa England Raheem Sterling kwa takribani Pauni 20 milioni, dirisha hili baada ya kocha Enzo Maresca kumjumuisha katika orodha ya wachezaji ambao hana mpango wa kuwatumia kwa msimu ujao. Staa huyu ambaye alinunuliwa kwa Pauni 47.5 milioni na Chelsea akitokea Man City miaka mitatu iliyopita, mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2027. Msimu uliopita alicheza kwa mkopo Arsenal.


Conor Gallagher

ATLETICO Madrid inaweza kulazimika kumuuza kiungo wao wa kati, Conor Gallagher, 25, dirisha hili baada ya kuzidi kwa idadi ya wachezaji wasio wa Umoja wa Ulaya wanaoruhusiwa kusajiliwa chini ya kanuni za La Liga. Conor ambaye anatokea England iliyojitoa katika umoja wa Ulaya, tangu kuanza kwa dirisha hili amekuwa akihusishwa na timu za England ikiwemo Newcastle United.

Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2029.


Joao Palhinha

TOTTENHAM ipo kwenye hatua nzuri katika mazungumzo yao na Bayern Munich ili kumnunua kiungo wa klabu hiyo, Joao Palhinha, 30, dirisha hili. Mabosi wa Bayern wapo tayari kumuuza fundi huyu, 30, lakini inahitaji kiasi kisichopungua Pauni 26 milioni kama ada yake ya uhamisho. Kiungo huyu anatamani sana kuondoka kwa sababu hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha Bayern kwa sasa.


Armand Lauriente

WINGA wa Sassuolo na Ufaransa, Armand Lauriente, 25,  anatarajiwa kuwasili England leo kwa ajili ya kufanya vipimo vya afya kabla ya kukamilisha uhamisho wake wa kujiunga na Sunderland dirisha hili. Taarifa za uhakika kutoka Sky Sports zinaeleza Sunderlandimekubali kutoa Pauni 17.5 milioni kwenda Sassuolo kama ada ya uhamisho wa fundi huyu.

Lauriente alishafanya makubaliano binafsi na Sunderland na kilichokuwa kinasubiriwa ni makubaliano juu ya ada ya uhamisho.


Xavi Simons

KIUNGO wa kati wa RB Leipzig, Xavi Simons, 22, amewaambia watu wake wa karibu anapendelea kwenda kucheza Ligi Kuu England kwa msimu ujao ambako Chelsea na Arsenal wanaripotiwa kuifuatilia saini yake. Simons ambaye alionyesha kiwango bora msimu uliopita, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2027, msimu uliopita alicheza mechi 33.


Ederson

MABOSI wa Manchester City wanadaiwa kukataa ofa ya Euro 3 milioni kutoka Galatasaray iliyowasilisha kuipata saini ya kipa wa klabu hiyo, Ederson, 31, dirisha hili. Ederson ambaye mkataba wake wa sasa unamalizika mwaka 2026, msimu uliopita alicheza mechi 40 za michuano yote.