Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ligi Kuu England imefikia patamu, sasa ni ‘weka, niweke’

EPL Pict

Muktasari:

  • Kwa maana hiyo, miamba hiyo miwili hakuna anayekubali kuangusha pointi kwenye mechi zake. Atakayefanya hivyo, imekula kwake.

LONDON, ENGLAND: HUKO kwenye Ligi Kuu England msako wa ubingwa wa taji hilo ni jino kwa jino. Weka niweke.

Msimamo unavyosoma, Arsenal inashikilia usukani wa ligi hiyo kwa tofauti ya pointi mbili tu dhidi ya Manchester City.

Kwa maana hiyo, miamba hiyo miwili hakuna anayekubali kuangusha pointi kwenye mechi zake. Atakayefanya hivyo, imekula kwake.

Baada ya kupisha Krismasi na Boxing Day, mchakamchaka wa miamba hiyo unarudi tena Jumamosi hii, ambapo Man City itatangulia kucheza ikiwa huko ugenini, The City Ground kukipiga na Nottingham Forest.

EP 01

Ushindi kwa Man City katika mechi hiyo utawafanya wababe hao wa kocha Pep Guardiola kuchukua usukani wa ligi kwa muda, hadi hapo Arsenal itakapocheza dhidi ya Brighton uwanjani Emirates. Mambo ni bandika, bandua.

Takwimu zinaonyesha kwamba Man City na Forest zimekutana mara 12 kwenye Ligi Ku England, ambapo mechi nne zilimalizika kwa sare, huku Man City ikishinda tano, tatu nyumbani na mbili ugenini, wakati Forest imeshinda tatu na zote ilipocheza nyumbani. Kwa maana hiyo, Forest itashuka uwanjani kusaka ushindi wake wa nne nyumbani dhidi ya Man City, ambayo itakwenda ugenini kusaka ushindi wake wa tatu dhidi ya wapinzani hao. Mambo ni moto.

EP 02

Kuhusu wapinzani wao kwenye mbio za ubingwa, Arsenal wao watakuwa Emirates kuwakabili Brighton, ambapo kwenye rekodi zao katika mechi za Ligi Kuu England, miamba hiyo imekutana mara 16, ambapo mechi tano zilimalizika kwa sare, huku Arsenal ikishinda sita, tatu nyumbani na tatu nyingine ugenini, huku Brighton ikishinda tano, mbili nyumbani na tatu ugenini. Kwa maana hiyo, Brighton itakwenda uwanjani Emirates ikiwa haina rekodi za kinyonge, ikiwa imeshinda mara tatu uwanjani hapo sawa na ilivyo kwa wenyeji. Itakuwaje?

Mechi nyingine za Ligi Kuu England zitakazopigwa Jumamosi, Brentford itakuwa nyumbani kukabiliana na Bournemouth, huku Everton ikienda ugenini kukipiga na Burnley na Liverpool itakuwa nyumbani Anfield kukabiliana na Wolves, iliyo kwenye hali mbaya zaidi kwenye ligi hiyo msimu huu.

EP 03

Kasheshe jingine litakuwa huko Stamford Bridge, wakati Chelsea itakapokuwa na kibarua kizito cha kuwakabili Aston Villa.

Kwa kipindi cha hivi karibuni, Aston Villa imekuwa ikiitesa sana Chelsea, ambapo katika mechi tano zilizopita, kikosi hicho cha Unai Emery, kimeshinda mechi tatu, sare moja na kupoteza mara moja.

Lakini, kwenye rekodi za jumla, Chelsea imeichapa Aston Villa mara nyingi, ambapo mara 60 walizokutana kwenye Ligi Kuu England, The Blues imeshinda 30, mara 17 nyumbani na 13 ugenini, huku Aston Villa ikishinda 16, mara tisa nyumbani na saba ugenini, wakati mechi 14 zilimalizika kwa sare.

Jumapili kutakuwa na mechi mbili tu kwenye mchakamchaka wa ligi hiyo, Sunderland itakipiga na Leeds United, wakati Crystal Palace itakuwa na nafasi ya kuulizana maswali magumu na Tottenham Hotspur uwanjani Selhurst Park.