Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

LeBron, Doncic kugeuza kibao Lakers?

NBA Pict

Muktasari:

  • Lakini tangu LeBron James kujiunga na timu hiyo mwaka 2018, swali lililokuwa kila msimu ni kama timu imeimarika vya kutosha kumpa nafasi ya kushinda taji lingine.

TEXAS, MAREKANI: KWA miongo sita iliyopita, Los Angeles Lakers wamekuwa moja ya timu za hadhi ya juu katika Ligi ya NBA, wakijivunia historia ya mataji 17 na mastaa wa enzi za dhahabu kama Kareem Abdul-Jabbar, Magic Johnson, na Kobe Bryant.

Lakini tangu LeBron James kujiunga na timu hiyo mwaka 2018, swali lililokuwa kila msimu ni kama timu imeimarika vya kutosha kumpa nafasi ya kushinda taji lingine.

LeBron, licha ya umri wake unaokaribia miaka 41, bado anachangia kwa kiasi kikubwa timu yake na kuonyesha ubora wa hali ya juu.

Hata hivyo, baada ya miaka ya changamoto, kuachwa raundi ya kwanza mara nyingi, na msimu mmoja wa kutoshiriki mchujo 'playoffs', Lakers wanakutana na sura mpya ya matumaini kwa kuja kwa Luka Dončić.

Dončić ni mchezaji mzuri wa kizazi kipya ambaye kwa sasa anachukua jukumu kubwa zaidi ndani ya timu. Akionekana kuwa na afya na nguvu mpya, msimu huu ni wa kuangalia ikiwa Lakers wataweza kuungana kwa nguvu za LeBron na Dončić na kurejea katika nafasi ya kuwania ubingwa.

NB 01

LeBron bado ni nguzo

LeBron bado anacheza kwa kiwango cha juu. Msimu uliopita, alifunga wastani wa pointi 24.4 huku akitoa usaidizi wa pasi za mwisho 8.2 kwa mchezo. Alishika nafasi ya 21 kwenye All-Star akimaliza nafasi ya siya kwenye kura za MVP na kuisaidia Lakers kufikisha ushindi wa 50. Takwimu hizo zinaonyesha kuwa gwiji huyo bado ni mkali.

NB 02

Doncic: Sura mpya Lakers

Doncic ndiye nembo ya baadaye ya Lakers. Uhamisho wake kutoka Dallas Mavericks ulikuwa wa kushtua. Dallas ilikuwa timu pekee aliyowahi kuchezea, na alihamishwa akiwa na umri wa miaka 25, akiwa tayari ameshinda tuzo nyingi na kuongoza ligi kwa pointi msimu wa 2023-24. Kuna wanaodai sababu za kuuzwa kwake zilihusiana na mazoezi na kiwango cha utimamu wa mwili. Lakini wakati huu wa likizo amewanyamazisha wakosoaji. Ameonekana akiwa amepunguza uzito na mwenye nguvu zaidi za ushindani.

NB 03

Changamoto Mbele

Pamoja na mabadiliko hayo, ukanda wa Magharibi unabaki kuwa moto wa kuotea mbali. Timu kama Denver Nuggets, Golden State Warriors na Minnesota Timberwolves zinabaki na vikosi imara. Kwa Lakers, changamoto kubwa itakuwa afya ya nyota wao wawili. Msimu uliopita walicheza mechi 23 tu pamoja kama washambuliaji wa kwanza. Wakiwa wote kwenye hali nzuri ya mwili kwa msimu mzima, Lakers wanaweza kufikia ushindi wa 55+ na nafasi ya juu kwenye msimamo.

Pia, kuna suala la muda wa kuzoeana. Dončić na LeBron ni wachezaji wenye tabia ya kutawala mpira. Itahitaji nidhamu na mikakati sahihi kuhakikisha wanaendana bila kuingiliana, huku kila mmoja akitumia nguvu zake vizuri.

NB 04

Hitimisho

Kwa mara ya kwanza katika muda mrefu, Lakers wanaonekana kuwa na mipango ya muda mrefu zaidi ya “kumsaidia LeBron tu.” Sasa wana mipango ya baadaye na sasa kupitia Doncic. Ikiwa Doncic ataendelea na kasi aliyo nayo na LeBron akibaki kwenye kiwango cha juu Lakers inaweza kuwa miongoni mwa timu zinazowania ubingwa msimu ujao.