Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Casemiro azua janga Inter Miami 

CASEMIRO Pict

Muktasari:

  • Siku ya Jumatano, Inter Miami ilitangaza rasmi kumsajili nyota huyo mwenye umri wa miaka 34, ambaye aliondoka Manchester United mwishoni mwa msimu uliopita, kwa mkataba utakaomalizika mwishoni mwa msimu wa 2027 wa MLS, ukiwa na kipengele cha kuongeza hadi Juni 2029.

NEW YORK, MAREKANI: UONGOZI wa Ligi Kuu ya Soka Marekani (MLS) imeanzisha uchunguzi dhidi ya Inter Miami kufuatia madai ya kukiuka taratibu za usajili baada ya kumsajili kiungo wa Brazil, Casemiro.

Siku ya Jumatano, Inter Miami ilitangaza rasmi kumsajili nyota huyo mwenye umri wa miaka 34, ambaye aliondoka Manchester United mwishoni mwa msimu uliopita, kwa mkataba utakaomalizika mwishoni mwa msimu wa 2027 wa MLS, ukiwa na kipengele cha kuongeza hadi Juni 2029.

Hata hivyo, dakika chache baada ya tangazo hilo, MLS ilitoa taarifa ikithibitisha kuwa inachunguza madai ya kuingilia taratibu za usajili.

"Ligi inaendelea kukusanya taarifa zote muhimu na haitatoa maoni zaidi hadi uchunguzi utakapokamilika," ilisema MLS.

CASE 03

Tatizo ni haki za kumsajili Casemiro

Uchunguzi unahusu mfumo wa haki za kumsajili, sheria ya MLS inayotoa haki ya kwanza kwa klabu fulani kufanya mazungumzo na mchezaji wa kimataifa anayetarajiwa kujiunga na ligi hiyo.

Kwa mujibu wa kanuni za MLS, kila klabu inaweza kuwa na hadi wachezaji watano kwenye orodha yake kwa wakati mmoja.

Kabla ya Casemiro kutua Inter Miami, LA Galaxy ndiyo iliyokuwa inamiliki haki hizo.

Inter Miami ilisema ilinunua haki hizo kutoka Galaxy, huku klabu hiyo ya Los Angeles ikithibitisha kuwa makubaliano yalifikiwa, lakini masharti yake yatatangazwa baada ya uchunguzi wa MLS kukamilika.

CASE 04

Casemiro aanza maisha mapya Marekani

Casemiro alitangaza Januari kuwa angeondoka Manchester United mwishoni mwa msimu wa 2026/27 baada ya pande zote mbili kukubaliana kutoongeza mkataba wake.

Kiungo huyo alitwaa mataji matano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa Real Madrid kabla ya kujiunga na Manchester United mwaka 2022.

Akiwa Old Trafford, alicheza mechi 160, akifunga mabao 26 na kutoa asisti 14, huku akisaidia klabu kutwaa Kombe la FA na Kombe la Ligi.

Baada ya kuondoka kwake, Manchester United ilijaza pengo hilo kwa kuwasajili Andrey Santos kutoka Chelsea kwa pauni50 milioni na Youri Tielemans kutoka Aston Villa kwa pauni35 milioni.

CASE 02

Beckham afurahishwa na usajili

Kabla ya uchunguzi kutangazwa, mmiliki mwenza wa Inter Miami, David Beckham, alimkaribisha Casemiro kwa furaha.

"Casemiro ni mshindi aliyefanikisha mengi katika soka. Baada ya mafanikio yake makubwa akiwa Real Madrid na Manchester United, ninafurahi ameamua kuifanya Miami kuwa nyumbani kwake," amesema Beckham.

Inter Miami sasa itakuwa na kikosi chenye nyota kadhaa akiwemo Lionel Messi, Rodrigo De Paul na Sergio Reguilon, ambaye aliwahi pia kucheza na Casemiro Real Madrid na Manchester United.

CASE 01

Hii si mara ya kwanza Inter Miami kukumbwa na matatizo ya usajili.

Mwaka 2021, klabu hiyo ilitozwa faini ya dola milioni mbili baada ya kukiuka kanuni za MLS katika usajili wa kiungo wa Ufaransa, Blaise Matuidi kutoka Juventus.

MLS ilibaini kuwa Matuidi alikuwa analipwa zaidi ya kiwango kilichoruhusiwa, hali iliyofanya Inter Miami kuwa na wachezaji wanne wa hadhi ya juu, badala ya watatu wanaoruhusiwa chini ya kanuni maarufu kama "Beckham Rule."