Lamine Yamal azua utata Barcelona
Muktasari:
- Yamal alicheza dakika 65 katika ushindi huo wa Barcelona wa kuanza kutetea taji la LaLiga, lakini alionekana kutofurahishwa wakati kocha Hansi Flick alipomtoa uwanjani.
BARCELONA, HISPANIA: NYOTA wa Barcelona, Lamine Yamal amezua mjadala nchini Hispania baada ya kuonekana mwenye huzuni wakati akitolewa katika mchezo ambao Barcelona iliichapa Elche mabao 5-0.
Yamal alicheza dakika 65 katika ushindi huo wa Barcelona wa kuanza kutetea taji la LaLiga, lakini alionekana kutofurahishwa wakati kocha Hansi Flick alipomtoa uwanjani.
Katika kipindi cha televisheni cha michezo, El Chiringuito, mtangazaji Josep Pedrerol amesema Barcelona imepokea picha za Yamal ambazo hazikuwa zimezoeleka kwake na ilipanga kumuuliza moja kwa moja kama kila kitu kilikuwa sawa.
Hata hivyo, mchambuzi Jota Jordi anaamini hali hiyo inaweza kuwa na uhusiano na uwezekano wa Barcelona kuwapoteza marafiki wa karibu wa Yamal ndani ya klabu hiyo.
Ripoti zinaeleza kuwa Alejandro Balde, Marc Casado na Hector Fort wanaweza kuuzwa katika dirisha hili la usajili.
Wachezaji hao watatu wamepitia akademi ya Barcelona pamoja na Yamal na wamekuwa na uhusiano wa karibu tangu wakiwa vijana.
Balde amehusishwa na uwezekano wa kuhamia Manchester Uni ted, huku Jordi akisema wachezaji hao ni kama ndugu kwa Yamal.
“Wao ni kama ndugu zake, na nimeambiwa kwamba jambo hilo linamuumiza Lamine,” amesema Jordi.
FLICK ATOA MAELEZO
Kocha Flick, hata hivyo, alikanusha kuwa kuna tatizo kubwa kwa Yamal na kueleza kuwa alia mua kumtoa kutokana na hali yake ya mwili.
“Alikuwa na tatizo dogo, maumivu ya kichwa. Lamine ni kipaji kikubwa, lakini amekuwa na mapum ziko ya wiki tatu na amefanya mazoezi kwa siku chache tu. Ni kawaida kutokuwa katika kiwango chake cha juu
Huyu ni mchezaji muhimu kwenye timu yetu wakati mwingine ni bora pia kuzingatia kuhusu afya yake na maisha yake kwa ujumla,” amesema Flick.
Kocha huyo amesema ameridhishwa na kiwango alichoonyesha Yamal katika dakika 60 alizocheza.
“Aliweka presha vizuri kwenye bao la kwanza na kwenye bao la pili alimpa Raphinha pasi. Anatupa chaguo zaidi kutokana na kiwango ambacho amekuwa akik ionyesha kila kukicha. Alitusaidia sana na anaendelea vizuri,” aliongeza.
Flick pia amesema ni kawaida kwa mchezaji mwenye ushindani mkubwa kama Yamal kutofurahia kutolewa uwanjani kwa sababu anatamani kucheza muda wote.
“Ni kawaida kwamba anataka kucheza. Unapokuwa bingwa wa kweli, daima unatamani kushinda taji linalofuata,” amesema.
Barcelona sasa inalenga kuendeleza mbio zake za kutetea taji la LaLiga, huku Flick akisisitiza kuwa kikosi chake kina kiu ya kutwaa ubingwa wa tatu mfululizo.