Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Celtic yamsajili nyota aliyetesa Argentina Kombe la Dunia 2026

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Hassan, mwenye umri wa miaka 24, ni mchezaji anayepiga kwa mguu wa kushoto lakini mara nyingi hutumika upande wa kulia. Amesaini mkataba wa miaka minne na Celtic, huku klabu hiyo ikiwa na chaguo la kuongeza mwaka mwingine.

GLASGOW, SCOTLAND: Celtic imemsajili winga wa Real Oviedo, Haissem Hassan, aliyeng'ara katika mchezo dhidi ya Argentina na kuisaidia Misri kusogea karibu na kuiondoa timu hiyo iliyokuwa ikiongozwa na Lionel Messi katika Kombe la Dunia la mwaka huu.

Hassan, mwenye umri wa miaka 24, ni mchezaji anayepiga kwa mguu wa kushoto lakini mara nyingi hutumika upande wa kulia. Amesaini mkataba wa miaka minne na Celtic, huku klabu hiyo ikiwa na chaguo la kuongeza mwaka mwingine.

Hassan alicheza jumla ya dakika 126 pekee katika Kombe la Dunia kutokana na kuchelewa kwa usajili wake, hali iliyomfanya akose hatua ya makundi licha ya kuwa alikuwa amewahi kuichezea timu za vijana za Ufaransa.

Hata hivyo, jina lake lilianza kuzungumzwa zaidi baada ya kupata nafasi ya kucheza katika hatua ya mtoano.

Alianza kama mchezaji wa akiba katika ushindi wa Misri dhidi ya Australia kwa mikwaju ya penalti kwenye hatua ya 32 bora, kabla ya kutoa kiwango bora dhidi ya Argentina.

Katika mchezo huo, Hassan aliwasumbua mabeki wa Argentina kwa kasi na uwezo wake wa kucheza mmoja kwa mmoja, huku Misri ikikaribia kupata ushindi mkubwa kabla ya kunyimwa ushindi huo katika mazingira yaliyoibua mabishano.

Mshambuliaji huyo aliyezaliwa jijini Paris amekuwa Real Oviedo kwa miaka miwili, baada ya kujiunga na klabu hiyo akitokea katika mfululizo wa timu nyingine tatu za Hispania tangu alipoondoka klabu yake ya utotoni, Chateauroux, mwaka 2020.

Ujio wake Celtic unaongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo, huku Hassan akitarajiwa kuleta kasi, ubunifu na uwezo wa kupenya kwenye safu za ulinzi.


Memphis Depay

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Memphis Depay, ameukosoa uamuzi wa Corinthians wa kutomwongezea mkataba, akidai klabu hiyo ya Brazil imekiuka makubaliano waliyofikia ya kuongeza mkataba wake kwa miaka miwili.

Corinthians imethibitisha kuwa haitamuongezea mkataba Depay, mwenye umri wa miaka 32, ikisema uamuzi huo umechukuliwa kwa lengo la kulinda “hali ya kifedha” ya klabu.


Martin Zubimendi

Real Madrid imeendelea kuonyesha nia ya kumsajili kiungo wa Arsenal, Martin Zubimendi, licha ya kushindwa kumnasa katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi mwaka jana.

Los Blancos ilipoteza mbio za kumsajili Zubimendi baada ya Arsenal kukamilisha dili la kumnunua kiungo huyo wa Hispania kwa ada ya pauni milioni 51.

Hata hivyo, Real Madrid haijaondoa kabisa uwezekano wa kumrudisha kwenye rada zake, huku Zubimendi akiendelea kuwa mmoja wa viungo wanaovutiwa nao kwa ajili ya kuimarisha kikosi hicho.


Paul Pogba

Klabu ya Monaco iko kwenye mazungumzo na kiungo Paul Pogba kuhusu kuvunja mkataba wake, ikiwa ni mwaka mmoja kabla ya kumalizika kwa mkataba huo.

Pogba, mwenye umri wa miaka 33 na aliyewahi kuichezea Manchester United, alipewa nafasi ya kurejesha makali ya soka lake na Monaco msimu uliopita baada ya kumaliza kutumikia adhabu ya kusimamishwa kutokana na kosa la matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku.

Hata hivyo, mambo hayakwenda kama ilivyotarajiwa baada ya Pogba kucheza jumla ya dakika 115 pekee katika mechi sita tangu alipojiunga na klabu hiyo.


Cristian Romero

Tottenham Hotspur imefikia makubaliano ya awali ya kumuuza beki wake Cristian Romero kwa Atletico Madrid, kwa mujibu wa taarifa za Sky Sports.

Dili hilo lina thamani ya takribani pauni milioni 34.2, ikiwemo bonasi zitakazotokana na utendaji wa mchezaji na mafanikio ya klabu.

Katika makubaliano hayo pia kuna kipengele kitakachoipa Tottenham asilimia 15 ya fedha endapo Romero atauzwa tena na Atletico Madrid hapo baadaye.


Lamine Camara

Crystal Palace imekumbana na pigo katika harakati zake za kuimarisha kikosi baada ya Monaco kukataa ofa ya mdomo kwa ajili ya kiungo Lamine Camara.

Palace ilitoa ofa inayodaiwa kuwa na thamani ya zaidi ya pauni milioni 35 kwa ajili ya kumsajili Camara, kiasi ambacho kingemfanya kuwa mmoja wa wachezaji wenye gharama kubwa zaidi katika historia ya usajili wa klabu hiyo.

Camara, mwenye umri wa miaka 22, ni raia wa Senegal na tayari ameichezea timu yake ya taifa mara 49. Pia alishiriki katika Kombe la Dunia lililofanyika msimu huu.



Ferran Torres

Paris Saint-Germain (PSG) iko katika hatua za mwisho za kukamilisha dili la kumsajili mshambuliaji wa Barcelona, Ferran Torres, kwa mujibu wa The Athletic.

PSG na Barcelona zinaendelea na mazungumzo kuhusu ada ya uhamisho wa Torres, mwenye umri wa miaka 26, huku mchezaji huyo akitarajiwa kutorejea mazoezini na kikosi cha kocha Hansi Flick wakati mazungumzo hayo yakiendelea.


Mykhailo Mudryk

Winga wa Chelsea, Mykhailo Mudryk, anaweza kuondoka klabuni hapo kwa mkopo baada ya Chelsea kuwa tayari kusikiliza ofa za kumpeleka katika klabu nyingine kwa mfumo huo.

Mudryk, mwenye umri wa miaka 25, tayari amevutia klabu kadhaa, huku taarifa zikieleza kuwa angalau timu tatu za Ligi Kuu England zimeonyesha nia ya kumsajili kwa mkopo.

Kwa mujibu wa football.london, Coventry City inayofundishwa na Frank Lampard ni miongoni mwa klabu zinazofikiria kumsajili winga huyo.


Curtis Jones

Mabingwa wa Serie A, Inter Milan, wameendelea kusukuma dili la kumsajili kiungo wa Liverpool, Curtis Jones, huku wakiamini wanaweza kukamilisha usajili huo kwa ada ya takribani euro milioni 35, sawa na pauni milioni 30.

Jones, ambaye ni raia wa England, amekuwa akivutia Inter katika dirisha hili la usajili, huku mabingwa hao wa Italia wakiamini dili hilo linaweza kukamilika iwapo Liverpool itakubali ofa hiyo.


Nobel Mendy

Hull City imethibitisha kumsajili beki wa Senegal, Nobel Mendy, kutoka Rayo Vallecano kwa ada ya rekodi ya klabu hiyo, huku pia ikimsajili beki wa kati Lucas Herrington kutoka Colorado Rapids.

Mendy, mwenye umri wa miaka 21, amesaini mkataba wa miaka mitano na Hull City, huku klabu hiyo ikiwa na chaguo la kuongeza mwaka mwingine.