Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kwa mziki huu wa Man United! Kaa mbali

MZIKI Pict

Muktasari:

  • Jumamosi iliyopita, Man United ilitangaza usajili wa straika wa Pauni 70 milioni, Benjamin Sesko, ambaye ataongoza safu ya ushambuliaji ya miamba hiyo. Straika huyo wa zamani wa RB Leipzig anatajwa kama mmoja wa washambuliaji matata kabisa Ulaya kwa sasa na atakuwa kwenye safu mpya ya wakali watatu kwenye fowadi ya Man United mdimu huu.

MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER United imeamua kufungua pochi kufanya usajili wa kuboresha safu ya ushambuliaji kumaliza tatizo la mabao ambalo lilimkabili kocha Ruben Amorim msimu uliopita, huku ikielezwa kujenga kikosi cha kutisha wapinzani.

Jumamosi iliyopita, Man United ilitangaza usajili wa straika wa Pauni 70 milioni, Benjamin Sesko, ambaye ataongoza safu ya ushambuliaji ya miamba hiyo. Straika huyo wa zamani wa RB Leipzig anatajwa kama mmoja wa washambuliaji matata kabisa Ulaya kwa sasa na atakuwa kwenye safu mpya ya wakali watatu kwenye fowadi ya Man United mdimu huu.

Na straika Sesko alisema kwa msisitizo kwamba ni suala la muda kabla hajaanza kuirudisha Man United kwenye anga za juu ambako ndiko inakopaswa kuwa.

Matheus Cunha alikuwa usajili wa kwanza wa Amorim kwenye dirisha hili, alipojiunga akitokea Wolves, kisha ikafanikiwa kunasa saini ya Bryan Mbeumo kutoka Brentford. Mastaa hao watatu wapya ndiyo watakaoongoza safu ya ushambuliaji ya Man United kwenye Ligi Kuu England msimu huu.

Cunha na Mbeumo walikuwa matata kwenye Ligi Kuu England msimu uliopita, wakufunga zaidi ya mabao 30 ya ligi, huku Sesko naye alikuwa bora Ujerumani.

Hao ndio watakaoongoza fowadi ya Man United kwa msimu huu, ambapo itakuwa na kasheshe la kuhakikisha timu inarudi kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na kukamatia nafasi za juu kwenye msimamo wa Ligi Ku England.

Na sasa jina linalohusishwa sana na mpango wa kujiunga na Man United ni kiungo, Carlos Baleba kutoka Brighton. Mawasiliano yameshafanyika baina ya pande zinazohusika kwenye dili hilo huku dhamira ya Man United ikiwa ni kunasa saini ya kiungo huyo Mcamerooni aende Old Trafford.

Man United inamtaka Baleba aende akacheze na Bruno Fernandes kwenye safu ya kiungo, nyuma ya wale washambuliaji watatu. Ujio wa Baleba utakwenda kuwapa changamoto kubwa viungo Kobbie Mainoo, Casemiro, Mason Mount na Manuel Ugarte.

Eneo jingine ambalo Man United inalotaka kuboresha ni kipa kutokana na Andre Onana kuwa na makosa mengi ndani ya uwanja. Kutokana na hilo, Man United imekuwa ikihusishwa na kipa wa Paris Saint-Germain, Gianluigi Donnarumma, ambaye amewekwa kando na timu yake hiyo ya Paris wakati ikijiandaa na mechi ya Uefa Super Cup dhidi ya Tottenham.

Kusajili kipa mpya Namba 1 si kipaumbele sana kwa Man United kwenye dirisha hili, lakini kama Donnarumma anapatikana sokoni mabosi watafanya jambo. Kipa mwingine ambaye amekuwa akihusishwa na Man United ni Emi Martinez.

Kwenye safu ya ulinzi, Man United bado ina watu wa kuleta ushindani mkali, ikiwa na Diogo Dalot, Noussair Mazraoui, Matthijs de Ligt, Harry Maguire, Lisandro Martinez, Patrick Dorgu, Leny Yoro, Luke Shaw, Ayden Heaven na Diego Leon. Kwenye fowadi pia kuna mastaa wengine kama Rasmus Højlund, Joshua Zirkzee, Amad Diallo na Chido Obi.