Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kwa Arsenal hii, mtakimbiana!

MTAKIMBIANA Pict

Muktasari:

  • Chama hilo linaloandaa kikosi chake ili kibebe taji la Ligi Kuu England msimu ujao, hadi sasa tayari limeshatumia Pauni 70.8 milioni kunasa huduma za viungo wawili, Martin Zubimendi na Christian Norgaard na kipa Kepa Arrizabalaga.

LONDON, ENGLAND: MIKEL Arteta anakaribia kufanya matumizi ya Pauni 200 milioni dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi wakati Arsenal ikijiandaa kukamilisha usajili wa wachezaji watatu kwa mpigo ndani ya wiki hii. Patamu hapo.

Chama hilo linaloandaa kikosi chake ili kibebe taji la Ligi Kuu England msimu ujao, hadi sasa tayari limeshatumia Pauni 70.8 milioni kunasa huduma za viungo wawili, Martin Zubimendi na Christian Norgaard na kipa Kepa Arrizabalaga.

Hata hivyo, baada ya kumaliza nafasi ya pili kwenye ligi kwa misimu mitatu mfululizo, kocha huyo Mhispaniola sasa ameamua kufunga busta kwa kunasa mastaa wa kuleta mataji.

Kwa msaada wa mkurugenzi wa michezo mpya wa timu hiyo, Andrea Berta, Arteta anatarajia kupata sura nyingine tatu mpya kwenye kikosi chake cha Arsenal wiki hii – jambo litakalofanya matumizi yao kwenye usajili wa dirisha hili kukaribia Pauni 200 milioni.

Kwa mujibu wa Times, Arsenal imekubali kulipa dau la awali la Pauni 54.5 milioni kwa ajili ya kunasa huduma ya straika Viktor Gyokeres kutoka Sporting Lisbon.

Straika huyo wa kimataifa wa Sweden alifunga mabao 54 katika mechi 52 msimu uliopita, hivyo huduma yake inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa Arsenal baada ya timu yao kushindwa kufanya vizuri kwenye safu ya ushambuliaji msimu uliopita.

Kocha Arteta pia yupo kwenye hatua za mwisho kunasa huduma ya winga wa Chelsea, Noni Madueke, ambaye atagharimu timu hiyo Pauni 48 milioni za awali na kisha itaongezwa Pauni 4 milioni baadaye.

Winga huyo ambaye alikosa mechi ya fainali ya Kombe la Dunia la Klabu wakati Chelsea ilipoichapa Paris Saint-Germain mabao 3-0, Jumapili iliyopita, anaripotiwa ameshafanya vipimo vya kwanza vya afya kwa ajili ya kujiunga na Arsenal.

Na jembe la tatu linalotarajiwa kunaswa na Arsenal ndani ya wiki hii ni staa Cristhian Mosquera. Beki huyo wa kati wa Valencia ataigharimu miamba hiyo ya Emirates, Pauni 13 milioni, akija kuongeza nguvu kwenye safu ya ulinzi yenye mabeki hodari, William Saliba na Gabriel Magalhaes.

Kwa hesabu hizo za wachezaji watatu watakaonaswa ndani ya wiki hii, yatafikisha matumizi ya Arteta kwenye dirisha hili kufikia Pauni 186 milioni.

Kusajili wachezaji wengi hivi kwenye dirisha la majira ya kiangazi halijawahi kutokea tangu mfumo mpya wa usajili ulipoanza mwaka 2002. Lakini, Arsenal inaweza isiishie hapo, kwa sababu Arsenal bado anataka kusajili winga wa kushoto. Na kwenye hilo, staa wa Newcastle United, Anthony Gordon na mkali wa Real Madrid, Rodrygo wapo kwenye orodha ya wakati anawataka watue Emirates.

Kwenye hilo hilo, Arsenal imerudi tena kuonyesha dhamira yao ya kunasa huduma ya kiraka wa Crystal Palace, Eberechi Eze, jambo vita yake itakuwa kali kwa sababu Bayern Munich inamtaka pia.

Kama wanavyokuja mastaa wapya, Arsenal itaachana na wakali waliopo kwenye kikosi chake na wachezaji Jorginho, Kieran Tierney, Thomas Partey na Takehiro Tomiyasu wote wameshaondoka bure, huku mastaa wengine kama Jakub Kiwior, Oleksandr Zinchenko, Reiss Nelson, Leandro Trossard, Fabio Vieira, Albert Sambi Lokonga na Karl Hein nao watafunguliwa mlango wa kutokea.