Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Konate awagomea Waarabu, Madrid yakoleza moto

Muktasari:

  • Kinachoripotiwa ni kwamba mabosi wa Real Madrid wameshaanza mazungumzo na mawakala wa beki huyo wa kati ili kutazama uwezekano wa kunasa huduma yake.

BEKI wa kati wa Liverpool na timu ya taifa ya Ufaransa, Ibrahima Konate, 26, amekataa ofa nono kutoka timu ya Saudi Pro League jambo linalowapa Real Madrid nguvu na mzuka mkubwa katika kufukuzia saini yake kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi.

Kinachoripotiwa ni kwamba mabosi wa Real Madrid wameshaanza mazungumzo na mawakala wa beki huyo wa kati ili kutazama uwezekano wa kunasa huduma yake.

Bado haijawekwa bayana kama Liverpool itakuwa tayari kumwachia beki huyo, licha ya kuwapo kwa ripoti zinadai miamba hiyo ya Anfield itahitaji ada ya Pauni 43.5 milioni endapo kama itafanya uamuzi wa kumpiga bei.

Mkataba wa Konate utamalizika Juni 2026 na hadi sasa bado hajafikia makubaliano ya kusaini dili jipya la kumfanya aendelee kubaki Anfield.

Na kama Konate hatakuwa amesaini dili jipya hadi kufikia Januari, basi Liverpool italazimika kumuuza kwenye dirisha hilo la majira ya baridi ili kupata pesa kuliko kubaki naye hadi mwisho wa msimu ambapo ataondoka bure.

Ripoti zinafichua, Konate yupo tayari kwenda kukipiga kwenye kikosi cha Los Blancos, lakini hawezi kulazimisha dili hilo kutokea endapo kama Liverpool itagoma kumuuza. Kinachoelezwa ni kwamba Real Madrid imemwekea Konate mkataba wa mshahara unaokaribia Pauni 300,000 kwa wiki ili akakipige Bernabeu.


Christopher Nkunku

CHELSEA inataka kupiga panga la maana katika kikosi chao katika dirisha hili la majira ya kiangazi na miongoni mwa mastaa ambao watapitiwa ni mshambuliaji wao wa kimataifa wa Ureno, Joao Felix, 25, ambaye yupo kwenye mazungumzo ya kusaini mkataba wa kudumu na Benfica, pia mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa Christopher Nkunku, 27, ambaye anahitaji na timu mbalimbali za ndani na nje ya England. Nkunku alihusishwa na timu kadhaa kwenye dirisha hili ikiwamo Manchester United inayohitaji mshambuliaji wa kati.


Daniel Muno

LICHA ya kusaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia katika kikosi cha kwanza cha Crystal Palace hadi 2028, beki Daniel Munoz, 29, yupo tayari kuondoka katika kikosi hicho katika dirisha hili ikiwa ofa nono itawekwa mezani kutoka kwa timu yoyote inayomhitaji. Mkataba wake una kipengele kinachoiwezesha Palace kuurefusha kwa mwaka mmoja zaidi ikiwa itahitaji kufanya hivyo.


Andrea Pinamonti

MSHAMBULIAJI wa Sassuolo, Andrea Pinamonti ameingia katika rada za West Ham inayohitaji huduma yake katika dirisha hili kwa ajili ya kuboresha eneo lao la ushambuliaji ambalo lina mapengo kadhaa hususani baada ya kuuzwa kwa washambuliaji kadhaa.

Mbali ya West Ham, timu nyingine kutoka jiji la London, Brentford, pia inataka kumsajili staa huyu mwenye umri wa miaka 26 na tayari imeshawasiliana na wawakilishi wake kujua ikiwa inaweza kumpata.


Gonzalo Garcia

LEEDS United inataka kumsajili  mshambuliaji wa Real Madrid, Gonzalo Garcia, 21, kwa mkopo katika dirisha hili.

Staa huyu wa kimataifa wa Hispania amekuwa akitamani kuondoka Madrid tangu dirisha la majira ya baridi mwaka huu kwa sababu hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza.

Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika 2027, katika michuano ya Kombe la Dunia la Klabu alicheza mechi sita na kufunga mabao manne.


Jacob Ramsey

NOTTINGHAM Forest imemweka kiungo wa Aston Villa na timu ya taifa ya vijana ya England chini ya miaka 21, Jacob Ramsey, katika orodha ya mastaa ambao ingependa kuwasajili katika dirisha hili.

Ramsey ni mmoja kati ya wachezaji walioonyesha kiwango bora msimu uliopita ambapo alicheza mechi 46 za michuano yote na kufunga mabao manne.

Mkataba wa sasa wa staa huyu unatarajiwa kumalizika 2027.


Cristhian Mosquera

BEKI kisiki wa Valencia, Cristhian Mosquera yupo katika hatua za mwisho za kujiunga na Arsenal katika dirisha hili la majira ya kiangazi baada ya kufikia makubaliano binafsi na washika mitutu hao.

Mosquera mwenye umri wa miaka 21, anasajiliwa kwa ajili ya kuongeza nguvu na kuwapa changamoto mabeki wa sasa Gabriel Magalhaes and William Saliba.

Arsenal ipo tayari kutoa karibia Euro 25 milioni kama ada yake ya uhamisho na mchezaji mwenyewe ameweka wazi kuwa anaihitaji Arsenal tu.


John Victor

BOTAFOGO ya Brazil ambayo ilishiriki michuano ya Kombe la Dunia la Klabu iliyofanyika Marekani hivi karibuni imeingia sokoni kutafuta kipa mpya baada ya Manchester United kuwatumia ofa ya kutaka kumsajili kipa wao raia wa Brazil, John Victor mwenye umri wa miaka 29.

Kwa mujibu wa tovuti ya The Sun, Botafogo ipo tayari kumuuza kipa huyo ingawa mazungumzo bado yanaendelea.

Man United imeingia sokoni kusajili kipa mpya baada ya kuumia kwa Andre Onana.