Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kombe la Dunia la mikeka

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa makadirio ya kampuni ya huduma za kifedha ya Macquarie Group, wadau wa kamari wanatarajiwa kuweka dau la wastani wa dola500 milioni kwa kila mechi ya mashindano hayo.

NEW YORK, MAREKANI: Kombe la Dunia la FIFA linatarajiwa kuwa tukio kubwa zaidi la kamari katika historia, huku zaidi ya dola 50 bilioni za Marekani zikitarajiwa kuwekwa kwenye dau duniani kote.

Kwa mujibu wa makadirio ya kampuni ya huduma za kifedha ya Macquarie Group, wadau wa kamari wanatarajiwa kuweka dau la wastani wa dola500 milioni kwa kila mechi ya mashindano hayo.

Jumla hiyo ya dola50 bilioni ni ongezeko kubwa ikilinganishwa na dola35 bilioni  zilizowekwa kama dau wakati wa Kombe la Dunia la 2022 lililofanyika nchini Qatar.

Makundi yanayojihusisha na uhamasishaji kuhusu madhara ya kamari yameonya kuwa watu wengi wanaocheza kamari hupoteza fedha kwa muda mrefu, na kwamba wale watakaoshiriki kamari wakati wa Kombe la Dunia wanaweza kushawishiwa kujaribu aina nyingine za kamari zenye hatari kubwa zaidi ya uraibu.

Mchambuzi wa Macquarie, Chad Benyon, amesema ongezeko hilo linachangiwa zaidi na kuongezeka kwa idadi ya timu zinazoshiriki mashindano hayo mwaka huu kutoka 32 hadi 48.

Kutokana na mabadiliko hayo, kutakuwa na zaidi ya mechi 100 katika kipindi cha wiki sita za mashindano, ikilinganishwa na mechi 64 zilizochezwa Qatar mwaka 2022.

Benyon pia alieleza kuwa tofauti za saa zinazofaa kwa watazamaji duniani, kutokana na mashindano kuandaliwa na Marekani, Canada na Mexico, zitasaidia kuongeza watazamaji duniani kote na hivyo kuongeza hamasa ya kubashiri matokeo ya mechi, hasa barani Ulaya, Amerika Kusini na Afrika.

Sababu nyingine inayochochea ukuaji huo ni kupanuka kwa soko la kamari za michezo nchini Marekani. Kwa sasa, takribani asilimia 65 ya wananchi wa Marekani wanaweza kisheria kushiriki kamari za michezo, ikilinganishwa na asilimia 40 mwaka 2022.

Hata hivyo, wataalamu wa masuala ya kamari wanaendelea kusisitiza kuwa kamari inapaswa kufanywa kwa tahadhari kubwa, kwa kuwa kwa muda mrefu watu wengi hupoteza fedha zaidi kuliko wanavyoshinda.

Hii inamaanisha kuwa Kombe la Dunia la 2026 ndilo la kwanza ambapo zaidi ya nusu ya wakazi wa Marekani wanaweza kisheria kuweka dau kwenye mechi za mashindano hayo.

Hata hivyo, mchambuzi wa Macquarie Group, Chad Benyon, ameonya kwamba mashindano hayo yanaweza kuwa faida ya muda mfupi kwa kampuni kubwa za kamari ikiwa hazitaweza kuwageuza wachezaji wa mara moja kuwa wateja wa kudumu wanaobashiri michezo mbalimbali.

Aliongeza kuwa kampuni zenye huduma za kasino mtandaoni ndani ya majukwaa yao zinaweza kufaidika zaidi kutokana na ongezeko la watumiaji wanaovutiwa na kamari wakati wa Kombe la Dunia.

Kwa upande wake, Les Bernal, mkurugenzi wa kitaifa wa Stop Predatory Gambling, ameonya kuwa:

"Mamia ya maelfu ya watu duniani kote, hasa wanaume vijana, watakumbwa na madeni makubwa na matatizo ya kifedha yatakayobadilisha maisha yao kutokana na kamari zinazohusiana na Kombe la Dunia."

Bernal alidai kwamba: "Watu 99 kati ya 100 wanaobashiri michezo hupoteza fedha kwa muda mrefu. Mfumo wa biashara wa kampuni za kamari za michezo unategemea kwa kiwango kikubwa watu wanaogeuzwa kuwa waraibu wa kamari, uraibu ambao unaweza kuwa na madhara makubwa sana."

Pia alitoa wito kwa wanasiasa duniani kuchukua hatua za kudhibiti aina za kamari zinazoweza kusababisha uraibu na kulinda watumiaji dhidi ya kupoteza fedha nyingi wakati wa Kombe la Dunia.

Naye mwanaharakati wa mageuzi ya kamari kutoka Uingereza, Matt Zarb-Cousin, alisema kuwa watu wanaobashiri mechi za Kombe la Dunia wanaweza kushawishiwa kujaribu michezo ya kasino mtandaoni, ambayo mara nyingi huonekana kuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kusababisha uraibu.

Ripoti ya National Centre for Social Research ilibaini kwamba nchini Uingereza, asilimia 79 ya mapato ya kampuni za kamari yalitokana na asilimia 10 tu ya wachezaji waliotumia fedha nyingi zaidi. Kundi hilo lilijumuisha watu walioweka dau la angalau pauni 5,639 kwa mwaka.