Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kombe la dunia la klabu, Marekani kumenoga

KUMENOGA Pict

Muktasari:

  • Leo tumekuletea picha kamili juu ya kile ambacho kimeandaliwa nchini humo kwa ajili ya kuhakikisha michuano inafanyika na kumalizika bila ya shida.

NEW YORL, MAREKANI: IKIWA zimebakia siku tisa kabla ya kuanza kwa michuano ya Kombe la Dunia la klabu itakayopigwa kule Marekani, maandalizi ndani ya nchi yanaripotiwa kuwa yameshamilika na sasa kinachosubiriwa ni muda rasmi tu wa michuano hiyo kuanza.

Maandalizi hayo ni pamoja na marekebisho ya viwanja, ulinzi na mapokezi kwa mashabiki.

Leo tumekuletea picha kamili juu ya kile ambacho kimeandaliwa nchini humo kwa ajili ya kuhakikisha michuano inafanyika na kumalizika bila ya shida.

KUME 06

MAPOKEZI YA MASHABIKI

Takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya mashabiki milioni 1.5 wanatarajiwa kusafiri kushuhudia mashindano haya moja kwa moja.

Sekta ya utalii inatarajiwa kufaidika pakubwa, ambapo Shirikisho la Utalii la Marekani linakadiria mapato ya zaidi ya dola 3 bilioni kutokana na wageni watakaokwenda.

 Serikali za majimbo zinashirikiana na mashirika binafsi kuimarisha usafiri wa umma, hoteli, huduma za afya na usalama ili kuweza kuendana na ongezeko la watu.

KUME 02

ULINZI WA MAENEO

Katika eneo hili kutakuw ana ushirikiano wa FBI ambayo itahusika na kuratibu taarifa za kijasusi, tahadhari za ugaidi, na ulinzi wa wageni wa hadhi ya juu.

Pia DHS (Department of Homeland Security) itaongeza nguvu zaidi katika kuratibu usalama wa mipaka, viwanja vya ndege, na maeneo ya mikusanyiko mikubwa.

Interpol itashirikiana na FBI na polisi wa mataifa mengine kwa ajili ya utambuzi wa wageni hatarishi.

Polisi za Majimbo na Jiji  kama NYPD (New York), LAPD (Los Angeles), na HPD (Houston) wataimarisha doria na uwepo wa polisi maeneo ya viwanja na hoteli.

Vilevile kamera za kisasa za CCTV  zitafungwa kwenye viwanja vyote, vituo vya usafiri, na maeneo ya burudani.

Mfumo wa AI kwa utambuzi wa uso (facial recognition) utatumika kudhibiti watu waliopigwa marufuku na kufuatilia mienendo isiyo ya kawaida.

Drones zitafanya doria angani ili kuchunguza mikusanyiko isiyo rasmi au matishio ya usalama.

KUME 01

ULINZI WA VIWANJANI

Kila kiwanja kitakuwa na vikosi maalum vya kupambana na ghasia (riot police) na vikundi vya usalama wa kibinafsi (private security).

Mashabiki wote watapitia ukaguzi mkali: scanner za mwili, vipimo vya vifaa vya chuma na ukaguzi wa mizigo wanayoingia nayo viwanjani.

Viwanja vyote pia vina  maeneo maalum ya kujificha wakati wa dharura na njia za haraka za kuondoka (emergency exits).

Maofisa wa afya ya dharura, zimamoto, na vikosi vya huduma za haraka (EMS) watakuwepo kila mechi.

Mafunzo ya kujitayarisha na kushughulikia milipuko mikubwa na mashambulizi ya silaha, au moto, tayari yameanza kwenye miji mwenyeji.

Mfumo wa Onyo wa Haraka (Emergency Alert System) utaunganishwa na simu za mashabiki kwa taarifa za usalama kwa wakati halisi.

Kwa kuwa mashindano haya yatategemea sana mifumo ya kidigitali katika masuala ya (matangazo, tiketi, huduma za malipo), timu za usalama wa kimtandao zimewekwa kuhakikisha hakuna mashambulizi ya mtandaoni au wizi wa taarifa za mashabiki unazuiliwa.

KUME 05

MABORESHO YA VIWANJA

Taarifa zinaeleza jumla ya dola 2 bilioni zimetengwa kwa ajili ya maboresho ya viwanja vitakavyotumika kwa ajili ya michuano hii na taarifa zinaeleza hadi sasa yameshafanyika.


1. MetLife Stadium -East Rutherford, New Jersey

Uwezo: 82,500

Matumizi: Fainali na mechi nyingine za hatua za mtoano.

Maboresho: Uboreshaji wa mfumo wa taa za LED, uboreshaji wa vyumba vya kubadilishia nguo, na maeneo ya wageni wa VIP.


2. Mercedes-Benz Stadium -Atlanta, Georgia

Uwezo: 75,000

Matumizi: Mechi za hatua ya makundi na hatua ya mtoano.

Maboresho: Mfumo wa paa linalofunguka, skrini ya video ya 360°, na uboreshaji wa maeneo ya mashabiki.


3. Bank of America Stadium -Charlotte, North Carolina

Uwezo: 74,867

Matumizi: Mechi za hatua ya makundi na hatua ya mtoano.

Maboresho: Uboreshaji wa vyumba vya waandishi wa habari, maeneo ya wageni wa VIP, na mfumo wa sauti.


4. TQL Stadium - Cincinnati, Ohio

Uwezo: 26,000

Matumizi: Mechi za hatua ya makundi.

Maboresho: Teknolojia ya kisasa ya VAR, nyasi za mseto, na maeneo ya mashabiki wa familia.


5. Rose Bowl Stadium -Pasadena, California

Uwezo: 88,500

Matumizi: Mechi za hatua ya makundi.

Maboresho: Uboreshaji wa taa, vyumba vya kubadilishia nguo, na maeneo ya waandishi wa habari.


6. Hard Rock Stadium - Miami Gardens, Florida

Uwezo: 65,000

Matumizi: Mechi za hatua ya makundi na hatua ya mtoano.

Maboresho: Uboreshaji wa mfumo wa sauti, maeneo ya wageni wa VIP, na teknolojia ya ulinzi.


7. GEODIS Park -Nashville, Tennessee

Uwezo: 30,000

Matumizi: Mechi za hatua ya makundi.

Maboresho: Uboreshaji wa maeneo ya mashabiki, vyumba vya waandishi wa habari, na mfumo wa taa.


8. Camping World Stadium - Orlando, Florida

Uwezo: 65,000

Matumizi: Mechi za hatua ya makundi na hatua ya mtoano.

Maboresho: Uboreshaji wa vyumba vya kubadilishia nguo, maeneo ya mashabiki, na teknolojia ya usalama.


9. Inter&Co Stadium - Orlando, Florida

Uwezo: 25,000

Matumizi: Mechi za hatua ya makundi.

Maboresho: Uboreshaji wa nyasi za mseto, mfumo wa taa, na maeneo ya mashabiki wa familia.


10. Lincoln Financial Field - Philadelphia, Pennsylvania

Uwezo: 69,000

Matumizi: Mechi za hatua ya makundi na hatua ya mtoano.

Maboresho: Uboreshaji wa mfumo wa sauti, vyumba vya waandishi wa habari, na maeneo ya wageni wa VIP.


11. Lumen Field - Seattle, Washington

Uwezo: 69,000

Matumizi: Mechi za hatua ya makundi.

Maboresho: Uboreshaji wa nyasi za mseto, mfumo wa taa, na maeneo ya mashabiki.


12. Audi Field – Washington, D.C.

Uwezo: 20,000

Matumizi: Mechi za hatua ya makundi.

Maboresho: Uboreshaji wa vyumba vya kubadilishia nguo, maeneo ya mashabiki, na teknolojia ya usalama

KUME 03

INA MAANA GANI KWA MAREKANI

Kwa FIFA, mashindano haya ni jaribio la mfumo mpya wenye timu 32 ambayo ni idadi sawa na ile ya Kombe la Dunia la mataifa.

Mfumo huu unatarajiwa kuongeza mapato ya matangazo, udhamini na haki za matangazo kwa zaidi ya dola 1.2 bilioni tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

Kwa Marekani, mashindano haya ni sehemu ya maandalizi ya kuwa mwenyeji mwenza wa Kombe la Dunia 2026 ambapo itashirikiana na  Canada na Mexico, michuano hii itawapa viongozi wa michezo uzoefu wa kitaalamu katika kuratibu mashindano makubwa.