Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Knicks yaweka rekodi NBA

Muktasari:

  • Knicks walikuwa nyuma kwa pointi 29 katika kipindi cha mchezo kabla ya kufanya ‘comeback’ ya kihistoria na hatimaye kushinda kupitia kikapu cha mwisho cha OG Anunoby aliyedaka mpira uliokosa wa jaribio la pointi tatu la Jalen Brunson huku kukiwa na sekunde 1.2 pekee kabla ya mchezo kumalizika.

NEW YORK, MAREKANI: TIMU ya New York Knicks imebakiza ushindi mmoja tu kutwaa ubingwa wa NBA kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1973 baada ya kufanya moja ya marejeo makubwa zaidi katika historia ya Fainali za NBA na kuibuka na ushindi wa pointi 107-106 dhidi ya San Antonio Spurs katika mchezo wa nne wa fainali uliofanyika usiku wa jana Jumatano.

Knicks walikuwa nyuma kwa pointi 29 katika kipindi cha mchezo kabla ya kufanya ‘comeback’ ya kihistoria na hatimaye kushinda kupitia kikapu cha mwisho cha OG Anunoby aliyedaka mpira uliokosa wa jaribio la pointi tatu la Jalen Brunson huku kukiwa na sekunde 1.2 pekee kabla ya mchezo kumalizika.

Ushindi huo umeifanya Knicks kuongoza mfululizo wa fainali kwa michezo 3-1, hivyo kupewa nafasi tatu za kutwaa ubingwa.

Awali, Spurs walionekana kuwa njiani kuelekea ushindi rahisi baada ya kumaliza kipindi cha kwanza wakiwa mbele kwa pointi 27. Hata hivyo, Brunson aliiongoza Knicks katika kurejea kwa kufunga pointi 36, huku Anunoby akiongeza pointi 33 na kuwa shujaa wa mwisho wa mchezo.

Kocha wa Knicks, Mike Brown, alimpongeza Anunoby kwa mchango wake mkubwa.

“Nilimwambia OG kwamba kwa ukubwa wake, nguvu zake na uwezo wake wa kimichezo, anatakiwa kuwa tishio kwenye mipira ya kushambulia. Sijui kama kuna mchezo mkubwa zaidi katika historia ya Knicks kuliko ule alioufanya leo,” alisema Brown.


REKODI YA KIHISTORIA

Kabla ya ushindi huo, hakuna timu iliyowahi kurejea kutoka nyuma kwa zaidi ya pointi 24 katika mchezo wa fainali tangu NBA ianze kuhifadhi takwimu za kina mwaka 1997. Rekodi ya awali ilikuwa ya Boston Celtics waliorejea kutoka nyuma kwa pointi 24 dhidi ya Los Angeles Lakers mwaka 2008.

Katika hatua zote za mchujo, comeback kubwa zaidi bado ni ya pointi 31 iliyofanywa na Los Angeles Clippers dhidi ya Golden State Warriors mwaka 2019.

Spurs waliongoza kwa pointi 81-52 katika robo ya tatu, lakini walipoteza kabisa makali yao katika kipindi cha pili cha mchezo. Baada ya kufunga mashuti 11 kati ya 16 ya pointi tatu mwanzoni, walifanikiwa kuingiza mashuti matatu tu kati ya 17 katika kipindi cha pili huku Knicks wakiwashinda kwa pointi 58-30.

Kocha wa Spurs, Mitch Johnson, alikiri kukatishwa tamaa na kilichotokea.

“Tulianza kupoteza kujiamini na tukakosa mashuti mengi. Ni jambo la kusikitisha sana,” alisema.

Wembanyama aangukia pua

Nyota wa Spurs, Victor Wembanyama, alifunga pointi 24 na kudaka rebound 13 lakini hakupata ufanisi mkubwa wa mashuti baada ya kuingiza 9 kati ya 25 alizopiga.

Aidha, atajilaumu kwa kukosa ‘free throw’ mbili muhimu zikiwa zimesalia dakika 1:47 huku Spurs wakiongoza kwa pointi 104-103.

Dylan Harper alifunga pointi 21 kwa Spurs, wakati De’Aaron Fox na Devin Vassell wakiongeza pointi 18 kila mmoja.


MASHABIKI WASHANGILIA KWA KISHINDO

Ndani ya Madison Square Garden, mashabiki wa Knicks walishangilia kwa furaha kubwa baada ya kushuhudia moja ya michezo ya kusisimua zaidi katika historia ya klabu hiyo.

Knicks walianza safari yao ya kurejea kwa kuizuia Spurs kufunga zaidi ya pointi 14 katika robo ya tatu na kupunguza pengo hadi pointi 15 kabla ya kuingia robo ya mwisho.

Hata baada ya Spurs kurejesha uongozi wao katika dakika za mwisho, Knicks hawakukata tamaa na walifanikiwa kupata ushindi kupitia mchezo wa mwisho wa Anunoby.

Spurs watalazimika kujipanga upya wakitarajia kushinda mchezo wa tano ili kuurejesha mfululizo huo New York.