Luka Modrić kuiongoza Croatia Kombe la Dunia 2026
Muktasari:
- Licha ya umri wake wa miaka 40, kiungo huyo wa AC Milan anatarajiwa kuweka rekodi ya kucheza Kombe lake la Dunia la tano na la mwisho katika historia ya soka lake.
Nahodha na kiungo Luka Modrić amejumuishwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Croatia kitakachoshiriki michuano ya Kombe la Dunia 2026.
Licha ya umri wake wa miaka 40, kiungo huyo wa AC Milan anatarajiwa kuweka rekodi ya kucheza Kombe lake la Dunia la tano na la mwisho katika historia ya soka lake.
Modrić, ambaye alipata jeraha la kuvunjika mfupa wa shavu mwishoni mwa mwezi Aprili akiwa na klabu yake nchini Italia, amefanyiwa upasuaji na amerejea mazoezini akiwa amevaa barakoa maalumu ya usoni ili kuhakikisha anakuwa fiti kwa ajili ya mashindano haya makubwa.
Kocha wa Croatia, Zlatko Dalić, ameeleza kuwa na imani kubwa na nahodha huyo ambaye anatazamwa kama nguzo na kiongozi mkuu wa kikosi hicho kinacholenga kurudia au kuzidi mafanikio ya miaka ya nyuma.
Kikosi cha Croatia kilichotangazwa kwa ajili ya Kombe la Dunia:
Makipa: D. Livaković (Dinamo Zagreb), D. Kotarski (Copenhagen) na I. Pandur (Hull City).
Mabeki: J. Gvardiol (Man City), D. Ćaleta-Car (Real Sociedad), J. Šutalo (Ajax), J. Stanišić (Bayern Munich), M. Pongračić (Fiorentina), M. Erlić (Midtjylland), na L. Vušković (Spurs).
Viungo: L. Modrić (Milan), akisaidiana na M. Kovačić (Man City), M. Pašalić (Atalanta), N. Vlašić (Torino), L. Sučić (Real Sociedad), M. Baturina (Como), K. Jakić (Augsburg), P. Sučić (Inter), N. Moro (Bologna), na T. Fruk (Rijeka).
Washambuliaji: I. Perišić (PSV), A. Kramarić (Hoffenheim), A. Budimir (Osasuna), M. Pašalić (Orlando City), P. Musa (FC Dallas), na I. Matanović (Freiburg).