Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Juventus yaja kivingine kwa Jadon Sancho

TETESI Pict

Muktasari:

  • Awali, Sancho alionekana kuwa na nafasi kubwa ya kuendelea kusalia katika kikosi cha Chelsea alichocheza kwa mkopo msimu uliopita lakini ilishindikana baada ya matajiri hao kuamua kutomsainisha mkataba wa kudumu.

JUVENTUS inaongeza juhudi kwa ajili ya kumsajili winga wa Manchester United na timu ya taifa ya  England, Jadon Sancho, mwenye umri wa miaka 25, na inaweza kumtoa mchezaji wake kiungo kutoka Brazil Douglas Luiz, 27, kama sehemu ya mabadilishano.

Awali, Sancho alionekana kuwa na nafasi kubwa ya kuendelea kusalia katika kikosi cha Chelsea alichocheza kwa mkopo msimu uliopita lakini ilishindikana baada ya matajiri hao kuamua kutomsainisha mkataba wa kudumu.

Staa huyu anataka kuondoka kwa sababu inaelezwa kocha Ruben Amorim hana mpango wa kumtumia katika kikosi chake na ameshatoa ruhusa ya kuuzwa kwake.

Katika msimu uliopita Sancho alicheza mechi 42 za michuano yote na kufunga mabao matano. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwakani.

Gazeti la Corriere dello Sport (CdS) limeripoti kuwa Juventus wanamchukulia Douglas Luiz kama mchezaji aliye “karibu kuondoka,” na kwamba “uwezekano wa kubadilishana kwa usawa (na Jadon Sancho) bado upo.”

Kinachoongeza moto kwenye tetesi hizi ni madai kuwa kocha mpya wa Manchester United, Ruben Amorim, “anamkubali sana” Douglas Luiz.

Hata hivyo, kusajili kiungo wa kati haionekani kuwa kipaumbele kwa Manchester United katika majira haya ya kiangazi kwani wanapanga kufanya mabadiliko makubwa katika safu ya ushambuliaji.


Yves Bissouma

KIUNGO wa Tottenham na timu ya taifa ya Mali, Yves Bissouma yupo katika rada za Juventus inayohitaji kumsajili katika dirisha hili la uhamisho la majira ya kiangazi.

Bissouma mwenyewe anaonekana kuwa tayari kujiunga na wababe hao wa Italia ingawa changamoto kubwa inaonekana kuwa ni makubaliano baina ya timu na timu kuhusiana na bei ya usajili.


Marcus Rashford

INAELEZWA mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford, 27, anauzwa kwa pauni 40 milioni katika dirisha hili jambo linalosababisha hadi sasa asipate timu kwani timu nyingi kati ya hizo zinaona kiasi hicho cha pesa ni kikubwa kwa mchezaji ambaye hajaweza kurejea katika makali yake ya juu kabisa.

Rashford mwenye umri wa miaka 27, mkataba wake na Man United unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.


Leonardo Balerdi

NEWCASTLE inaangalia uwezekano wa kumsajili beki wa kati wa Marseille na timu ya taifa ya Argentina, Leonardo Balerdi, mwenye umri wa miaka 26, ambaye pia anawindwa na  Juventus.

Balerdi ni miongoni mwa wachezaji tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Marseille na msimu uliopita alicheza mechi 29 za michuano yote. Mkataba wake unamalizika mwaka 2028.


Tolu Arokodare

BURNLEY inatafuta shambuliaji mpya kwa ajili kujiimarisha na staa wa KRC Genk na timu ya taifa ya Nigeria, Tolu Arokodare, mwenye umri wa miaka 24, ni miongoni mwa wale inaowahitaji.

Arokodare ni mmoja kati ya wachezaji tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Genk na msimu uliopita alicheza mechi 45 za michuano yote na kufunga mabao 23. Mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2027.


 Rodrygo

Al-Nassr imefanya mazungumzo ya awali na mshambuliaji wa Real Madrid, Rodrygo, 24, ambaye pia amekuwa akiwindwa na timu kadhaa za Ligi Kuu, England. Hivi karibuni Rodrygo alipewa nafasi ya kutafuta timu itakayokuwa tayari kumsajili baada yeye mwenyewe kuona kwamba hana nafasi ya katika kikosi cha timu hiyo chini ya kocha Xabi Alonso.


Mario Balotelli

MSHAMBULIAJI wa zamani wa timu ya taifa ya Italia, Mario Balotelli, 34, anawindwa na timu kadhaa za Ligi Kuu ya Marekani na Mexico baada ya kuondoka Genoa mwanzoni mwa mwezi huu.

Katika msimu uliopita Balotelli alicheza mechi sita za michuano yote na hakufunga hata bao moja huku umri ukimtupa mkono.