Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jamie Carragher aukubali mziki wa Arsenal

JAMIE Pict

Muktasari:

  • Carragher ametoa kauli hiyo baada ya kushuhudia ushindi wa Manchester City wa mabao 3–0 dhidi ya Liverpool jana Jumapili, Novemba 9, 2025. Ushindi huo uliiwezesha timu ya Pep Guardiola kupanda hadi nafasi ya pili, ikiishusha Chelsea, na kwa sasa iko nyuma ya Arsenal kwa pointi nne.

Gwiji wa Liverpool, Jamie Carragher, ameitaja Arsenal kuwa timu bora zaidi katika Ligi ya EPL msimu huu.

Carragher ametoa kauli hiyo baada ya kushuhudia ushindi wa Manchester City wa mabao 3–0 dhidi ya Liverpool jana Jumapili, Novemba 9, 2025. Ushindi huo uliiwezesha timu ya Pep Guardiola kupanda hadi nafasi ya pili, ikiishusha Chelsea, na kwa sasa iko nyuma ya Arsenal kwa pointi nne.

Licha ya kiwango bora kilichoonyeshwa na Manchester City, Carragher amesema hana shaka kwamba kikosi cha Mikel Arteta ndicho bora zaidi nchini England kwa sasa. 

Beki huyo wa zamani wa England amekiri kuwa Manchester City itaendelea kuiweka Arsenal chini ya shinikizo katika mbio za ubingwa, hasa ikizingatiwa kwamba Arsenal imewahi kupoteza mara mbili dhidi ya kikosi cha Guardiola katika misimu iliyopita.

JAMI 01

Carragher ameambia Sky Sports: “Mara mbili katika miaka mitatu iliyopita, wamekuja kutoka nyuma na kuipiku Arsenal. Liverpool ndio mabingwa, lakini City imewazidi. Wanaweza kuwa wanapata kumbukumbu za mara zilizopita walipokuwa na nafasi ya kuchukuwa ubingwa.

“Bado ninaamini Arsenal ndiyo timu bora zaidi niliyoshuhudia katika Ligi ya EPL msimu huu, bila shaka.” 

Kwa sasa, Arsenal inaongoza msimamo wa Ligi ya EPL kwa pointi 26, ikifuatiwa na Manchester City (22), kuelekea mapumziko ya mechi za kimataifa, na wanatarajiwa kurejea kwa nguvu kutafuta ushindi katika mchezo wao ujao wa ligi.

JAMI 02

MECHI TANO ZIJAZO ZA ARSENAL
Tottenham Hotspur – Novemba 23 2025, nyumbani
Chelsea – Novemba 30 2025, ugenini
Brentford – Novemba 03 2025, nyumbani 
Aston Villa – Desemba 06 2025, ugenini 
Everton – Desemba 21 2025, ugenini


MECHI TANO ZIJAZO ZA MANCHESTER CITY 
Manchester City – Novemba 22, 2025, ugenini
Leeds United – Novemba, 29 2025, nyumbani
Manchester City – Desemba 3, 2025, ugenini
Sunderland – Desemba 6, 2025, nyumbani