Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jamie Carragher: Inatosha sasa, Mo Salah awekwe benchi

SALAH Pict

Muktasari:

  • Katika mechi hiyo Liverpool ilipoteza nyumbani kwake Anfield kwa kufungwa 1-2, hii imekuwa mara ya nne mfululizo kwa timu hiyo kupoteza, hali ambayo imemuibua Carragher na kutoa maoni yake.

Gwiji wa Liverpool, Jamie Carragher amemshauri kocha mkuu wa klabu hiyo, Arne Slot kumuweka benchi mshambuliaji Mohamed Salah baada ya mambo kuwaendea hivyo kwenye mchezo wa jana Jumapili, Oktoba 19, 2025 dhidi ya Manchester United.

Katika mechi hiyo Liverpool ilipoteza nyumbani kwake Anfield kwa kufungwa 1-2, hii imekuwa mara ya nne mfululizo kwa timu hiyo kupoteza, hali ambayo imemuibua Carragher na kutoa maoni yake.

Gwiji huyo amemtaka kocha Arne Slot kumuweka benchi Salah, ambaye anadai kwa sasa amepoteza uwezo wa kupambana na safu za ulinzi za timu pinzani, hali ambayo inapelekea Liverpool kushindwa kupata matokeo mazuri kupitia kwa mshambuliaji huyo wa Misri.

Akizungumza kupitia Sky Sports, Carragher amezungumzia kuhusu kiwango cha Salah katika mechi hiyo, hasa tukio la kutolewa uwanjani kipindi cha pili. 

SAL 01

Amesema Salah sasa yuko katika hatua ya maisha ya soka ambayo hayampi nafasi ya kucheza mara kwa mara kama ilivyokuwa siku za nyuma, hivyo kocha Slot anapaswa kumpumzisha na kutoa nafasi kwa washambuliaji wengine ambao anaamini wana uwezo wa kuisaidia timu.

“Hii ni changamoto kubwa kwa kocha. Cha kuvutia ni kwamba alimtoa uwanjani. Jurgen Klopp aliwahi kumtoa mara kwa mara hapo awali, na hiyo ilionyesha hata akiwa na nguvu au makali fulani, bado angeweza kutolewa kama hakuwa kwenye kiwango bora. 

“Mo Salah hastahili kuwa kwenye kikosi cha kwanza. Haimaanishi sio bora, lakini kuna wakati unapaswa kumpumzisha mchezaji ili aweze kurejea kwenye kiwango chake cha kuisaidia timu,” amesema Carragher.

Katika hatua nyingine, Carragher ameenda mbali zaidi kwa kusisitiza kuwa, kwa sasa Salah hafai kuchezeshwa katika kila mechi, hasa zile ngumu za ugenini.

“Liverpool wana mechi mbili za ugenini, moja Ulaya na nyingine dhidi ya Brentford, sidhani kama anastahili kucheza zote mbili. Tumefikia hatua ambapo Salah hafai kuwa mchezaji anayeanza kila wiki.”

SAL 02

Kushuka kwa kiwango cha Salah
Baada ya msimu wa 2024-25 wa kuvutia ambapo Mohamed Salah aliongoza kwa ufungaji wa mabao na pasi za mwisho, na hatimaye kutangazwa kama Mchezaji Bora wa Mwaka, huku Liverpool ikitwaa ubingwa, msimu huu amekuwa na wakati mgumu kwenye mechi alizocheza hadi sasa.

Akiwa na umri wa miaka 33, Salah ameanza katika mechi nane mfululizo za ligi msimu huu, lakini amefunga mabao mawili tu. Liverpool pia imekuwa na kiwango cha kustaajabisha tofauti na msimu uliopita, na kwa sasa ina pointi nne nyuma ya vinara wa ligi Arsenal.

Katika mechi ya jana Jumapili, Oktoba 19, 2025 dhidi ya Manchester United, wakati Liverpool ilipokuwa ikihitaji bao la kusawazisha, kocha Arne Slot aliamua kumtoa Salah na kumuingiza Jeremie Frimpong, jambo ambalo wengi wameliona kama ishara ya kuporomoka kwa makali yake.