Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jadon Sancho, Juventus ni suala la muda

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Ripoti zinaeleza Sancho atasaini mkataba wa miaka minne ambao utamwezesha kulipwa mshahara wa Euro 6 milioni kwa mwaka ambacho ni kiasi kidogo ukilinganisha na kile ambacho anakipokea kwa sasa akiwa na Man United.

JUVENTUS imekubali kutoa Euro 25 milioni kwenda Manchester United kuipata saini ya winga wa timu hiyo, Jadon Sancho.

Ripoti zinaeleza Sancho atasaini mkataba wa miaka minne ambao utamwezesha kulipwa mshahara wa Euro 6 milioni kwa mwaka ambacho ni kiasi kidogo ukilinganisha na kile ambacho anakipokea kwa sasa akiwa na Man United.

Inaelezwa wakala wa staa huyu alisafiri kwenda Italia wiki iliyopita kwa ajili ya mazungumzo zaidi na dili linatarajiwa kukamilika kabla ya Alhamisi ya wiki hii.

Kocha wa Juventus, Igor Tudor amewaambia mabosi wa timu hiyo anahitaji asafiri na Sancho kwenda Ujerumani kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya.

Mbali ya Juventus, saini ya Sancho pia ilihitajika na baadhi ya timu za Saudi Arabia pamoja na Lazio na AS Roma.

Awali pia ilionekana huenda angesaini mkataba wa kudumu na Chelsea aliyoichezea kwa mkopo msimu uliopita lakini timu hiyo iliamua kuachana na mpano huo.

Mkataba wa Sancho ambaye msimu uliopita alicheza mechi 42 za michuano yote na kufunga mabao matano, unatarajiwa kumalizika mwaka 2026.


Adam Wharton

LIVERPOOL inaongoza vita ya kumsajili kiungo wa kati wa Crystal Palace na England, Adam Wharton, 21,dirisha hili lakini inakumbana na kikwazo kutoka kwa mchezaji mwenyewe ambaye ameomba kuendelea kusalia kwa mwaka mmoja zaidi katika kikosi cha Palace. Mbali ya Liverpool, saini yake pia inawindwa sana na Tottenham. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2029. Msimu uliopita alicheza mechi 27 za michuano yote.


Randal Kolo Muani

MANCHESTER United na Newcastle zipo katika vita kali ya kuiwanai saini ya mshambuliaji wa Paris St-Germain na timu ya taifa ya  Ufaransa, Randal Kolo Muani, 26. Timu zote hizi zinatamani sana kumsajili Muani dirisha hili la majira ya kiangazi baada ya kuvutiwa na kiwango alichokionyesha akiwa na Juventus msimu uliopita alipokuwa akicheza kwa mkopo. Muani ambaye mkataba wake wa sasa unamalizika mwaka 2028.


Jordan Pickford

KIPA wa  Everton, Jordan Pickford, 31, yuko karibu kusaini mkataba mpya wa miaka minne na klabu hiyo ya Merseyside wakati ule wa sasa ukitarajiwa kumalizika mwaka 2027. Kabla ya kufikia makubaliano hayo, Pickford alikuwa akitajwa anaweza kujiunga na timu kadhaa ikiwemo Man United. Katika mkataba wake mpya, kuna ongezeko la mshahara kutoka Pauni 125,000 hadi 150,000 kwa wiki.


Pervis Estupinan

AC Milan inapambana kuipata saini ya beki kisiki wa  Brighton, Pervis Estupinan, 27, ili akawe mbadala wa beki wao wa kimataifa wa Ufaransa, Theo Hernandez, 27, aliyesajiliwa na Al-Hilal dirisha hili. Benchi la ufundi la Milan limevutiwa sana na kiwango cha Estupinan alichoonyesha msimu uliopita ambapo alicheza mechi 36 za michuano yote. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2027.


Luis Diaz

BAYERN  Munich inaendelea na juhudi zao kuhakikisha inamsajili mshambuliaji wa Liverpool, Luis Diaz, baada ya ofa mbili ilizowasilisha  kukataliwa. Kwa mujibu wa ripoti kutoka tovuti ya Bild, viongozi wa timu hizi mbili wanatarajiwa kukutana hivi karibuni kufanya mazungumzo zaidi juu ya Luiz. Staa huyu, 28 awali alikuwa akihusishwa na Barcelona lakini imeshindikana kutokana na kiasi cha pesa kinachohitajika na Liverpool.


Evan Ferguson

ROMA imefikia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji wa Brighton, Evan Ferguson kwa mkopo wa msimu mmoja ambao utakuwa na kipengele cha kumnunua mazima kwa Euro 40 milioni ikiwa itavutiwa na kiwango chake Ferguson ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2029, msimu uliopita alicheza mechi 23 za michuano yote.


Milan Skriniar

FENERBAHCE imeripotiwa kufikia makubaliano na Paris St-Germai kuwasajili beki wa klabu hiyo na timu ya taifa ya Slovakia, Milan Skriniar, 30,pamoja na kiungo mshambuliaji wa  timu hiyo na Hispania Marco Asensio, 29, katika dirisha hili. Asensio na Skriniar ni miongoni mwa wachezaji ambao hawapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza cha PSG.

Mkataba wa Asensio unatarajiwa kumalizika mwakani wakati wa Skiriniar ukimalizika mwaka 2028.