Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ligi Kuu Bara 2026/27, kazi inaanza

LIGI KUU Pict

Muktasari:

  • Dodoma Jiji inakwenda kucheza na Pamba Jiji ikiwa na kumbukumbu ya kupokwa pointi tatu na kupewa mpinzani wake na mabao matatu katika mechi ya  msimu uliopita iliyopigwa Oktoba 25, 2026, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma ambapo kulitokea changamoto ya umeme kukatika na ilionekana kushindwa kushughulikia hilo na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ilitoa maamuzi ya kuipa Pamba ushindi.

PAZIA la Ligi Kuu Bara linafunguliwa rasmi leo Agosti 14, 2026 zikichezwa mechi tatu ambapo Pamba Jiji itakuwa mwenyeji wa Dodoma Jiji, mechi itakayopigwa saa 8:00 mchana kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Dodoma Jiji inakwenda kucheza na Pamba Jiji ikiwa na kumbukumbu ya kupokwa pointi tatu na kupewa mpinzani wake na mabao matatu katika mechi ya  msimu uliopita iliyopigwa Oktoba 25, 2026, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma ambapo kulitokea changamoto ya umeme kukatika na ilionekana kushindwa kushughulikia hilo na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ilitoa maamuzi ya kuipa Pamba ushindi.

Timu hizo zinapokutana zinakuwa na ushindani wa juu, zilipokutana raundi ya 21 mechi iliyopigwa Mei 10, 2026, Pamba ikiwa mwenyeji zilitoka suluhu.

KANU 01

Kocha wa Pamba Jiji, Francis Baraza aliyeiongoza timu hiyo kumaliza msimu uliopita ikiwa nafasi ya saba ikiwa na pointi 36, amesema: "Tumefanya mabadiliko makubwa, kuna wachezaji walioondoka na wapya, hivyo naamini tutakuwa na msimu mzuri na mashabiki waje waone maigizo mapya na watatoka na furaha baada ya dakika 90."

Kocha Vincent Mashami siyo mgeni Dodoma Jiji, msimu uliopita aliwekwa kando kutokana na kukosa vigezo, hivyo timu ilikuwa chini ya Amani Josiah ambaye kwa sasa yupo Mashujaa.

Mashami aliyewahi kuwa kocha wa timu ya taifa ya Rwanda, amesema mechi dhidi ya Pamba haitakuwa rahisi lakini wapo tayari kwa kuzipambania pointi tatu.

"Tunahitaji kuwa na muendelezo wa kiwango ambacho timu ilikionyesha msimu uliopita ambapo ilimaliza nafasi ya 9 angalau msimu huu tuwe katika top 5," amesema.

KANU 02

Mechi nyingine ni Mbeya City iliyomaliza nafasi ya 14 na pointi 30 msimu uliopita dhidi ya Geita Gold iliyopanda kucheza Ligi Kuu msimu huu, itapigwa saa 10:15 alasiri ambapo makocha wa timu hizo wamezungumzia namna ambavyo zitakuwa dakika 90 za ushindani wa juu.

Kocha wa Mbeya City, Salum Mayanga aliyeinusuru timu hiyo isishuke daraja msimu wa 2025-2026, amesema: "Itakuwa mechi ngumu lakini tumejipanga ili kufungua pazia la ligi ya msimu huu kwa ushindi tumesajili wachezaji wapya ambao watasaidiana na waliokuwepo na timu tunatambua Geita ina kocha mzoefu na wachezaji wazuri."

Kiungo wa Mbeya City, Hassan Dilunga, amesema: “Hatutaki presha ijirudie, tunaamini viongozi na benchi la ufundi waliona wapi tuliteleza, hivyo kila mchezo kwetu ulio mbele yetu ni vita ya pointi tatu ili kumaliza salama ligi.”

KANU 03

Kwa upande wa kocha wa Geita Gold, Zuber Katwila ambaye ndiye aliyeipandisha timu hiyo daraja, amesema: "Tumejipanga, tunafahamu msimu sio mwepesi lakini tumepanda na tupo tayari kupamba na kuona tunaanza kwa kuvuna pointi tatu dhidi ya Mbeya City.

“Lazima tuwe makini tucheze kwa tahadhari yasitukute kama Mtibwa Sugar, kupitia matokeo hayo na timu nyingine ni fundisho kwetu, hata Geita Gold ilipanda na kushuka na sasa tumerejea tena.

“Tunapaswa kucheza kwa kuwaheshimu wapinzani na ninaamini kwa maandalizi tuliyofanya na utayari wetu tutafanya vizuri, kimsingi ni kuendelea kupambana na ninashukuru kwa sapoti ya uongozi.”

KANU 04

Kwa upande wake straika wa Geita Gold, Yusuph Mhilu, amesema watajitahidi kufuata maelekezo ya benchi la ufundi kuhakikisha wanafanya vizuri akieleza kuwa mchezo wao dhidi ya Mbeya City pointi tatu ni muhimu.

“Tutacheza kwa kuwaheshimu kwakuwa tupo ugenini lakini mpira ni mchezo wa wazi, yeyote atakayeweza kutumia nafasi anaweza kupata matokeo mazuri, tunahitaji pointi tatu ili kuanza vyema Ligi,” amesema staa huyo.

Usiku saa 1:00, kuna mechi nyingine ambayo Singida Black Stars itaikaribisha Fountain Gate.

Katika mechi iliyopigwa Februari 11, 2026 msimu uliopita, Singida BS ilishinda bao 10 dhidi ya Fountain Gate.

Matokeo yanaonyesha timu hizo zinapokutana zinakuwa na ushindani wa juu kwani raundi ya 30 mechi ambayo ilipigwa Juni 30, 2026, Fountain Gate ikiwa mwenyeji wa mchezo ilishinda mabao 4-3.