Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

IRON MAN: Mkono wa chuma unaingiza pesa, moyo unatoa kwa jamii

IRON Pict

Muktasari:

  • Ni mwigizaji wa Hollywood aliyejipatia jina kutokana na filamu zake maarufu ikiwamo ya Iron Man ambayo imempa jina hilo la utani.

CARLIFONIA, MAREKANI: UKITAJA waigizaji 50 wanaoingiza pesa nyingi duniani, huwezi kulikosa jina la Robert Downey Jr 'Iron Man'.

Ni mwigizaji wa Hollywood aliyejipatia jina kutokana na filamu zake maarufu ikiwamo ya Iron Man ambayo imempa jina hilo la utani.

Makala hiya yanakuchambulia namna nyota huyu anavyopata pesa, mali anazomiliki, maisha yake ya kifahari, familia yake, pamoja na moyo wake wa huruma kwa jamii.

IR 01

ANAPIGAJE PESA

Hadi kufikia mwaka 2025, utajiri wa Robert Downey Jr. unakadiriwa kuwa zaidi ya Dola 300 milioni (takriban Tsh780 bilioni). Kiasi hiki kinatokana na kiasi kikubwa anacholipwa filamu, hususan mfululizo wa Marvel Cinematic Universe na kwa filamu ya Avengers: Endgame pekee alilipwa zaidi ya Dola 75 milioni.

Downey Jr. amepata malipo makubwa kwenye filamu kama Iron Man, Sherlock Holmes, Dolittle na  Avengers.

Vilevile, anamikiki hisa katika kampuni ya Team Downey inayozalisha filamu na vipindi vya televisheni.

Pia amesaini mikataba ya udhamini na kampuni mbalimbali kama OnePlus, Audi na Dolce & Gabbana, ambazo zote kwa pamoja zinakadiriwa kumpa takribani Dola 20 milioni kwa mwaka.

Mwigizaji huyu pia amewekeza katika teknolojia na amenunua hisa katika kampuni mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kujiongezea kipato.

IR 02

NDINGA

Downey Jr. ni mpenzi mkubwa wa magari ya kifahari. Baadhi ya magari anayo miliki ni:

Audi R8 -Dola 150,000 ( TSh 390 milioni)

Bentley Continental GT - Dola 200,000 ( TSh 520 milioni)

Ferrari California T - Dola 230,000 (TSh 598 milioni)

Mercedes-Benz SL550 Coupe -Dola 115,000 (TSh 299 milioni)

1965 Chevrolet Corvette Stingray – Dola 100,000(Tsh 260 milioni)

IR 03

MIJENGO

Ana mjengo maeneo ya Malibu, California yenye thamani ya Dola 13.8 milioni (TSh 35.8 bilioni) ambayo ndani yake ina bwawa la kuogelea, ukumbi wa sinema na mandhari ya bahari, pia ana nyumba huko Hamptons yenye thamani ya Dola 11.9 milioni (Tsh 30.9 bilioni) na nyumba ya Los Angeles inayokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya Dola 4 milioni.


MSAADA KWA JAMII

Amekuwa akisaidia sana jamii kupitia miradi mbalimbali kama Footprint Coalition ambao una nia ya kupambana na uchafuzi wa mazingira na kuendeleza teknolojia ya kijani.

Pia amekuwa akitoa michango katika taasisi zinazosaidia wagonjwa wa saratani, watoto yatima na walemavu pamoja mashirika ya kutunza mazingira na kusaidia vijana wanaoishi mitaani Marekani.

IR 04

FAMILIA NA BATA

Downey Jr. yupo katika ndoa na Susan Downey, ambaye pia ni mtayarishaji wa filamu. Wana watoto wawili pamoja ambao ni Exton Elias Downey na Avri Roel Downey.

Pia ana mtoto mkubwa aitwaye Indio Falconer Downey aliyempata katika ndoa yake ya awali na Deborah Falconer.

Staa huyu hupendelea sana kusafiri na familia yake katika sehemu za kifahari kama Maldives, Bora Bora na Monte Carlo.