Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hawa hapa kumrithi Rodri Man City

RODRI Pict

Muktasari:

  • Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 30, ambaye alitwaa tuzo ya Ballon d’Or mwaka 2024, anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka minne na Barcelona, huku uhamisho huo ukitarajiwa kukamilika ndani ya siku chache zijazo.

BARCELONA, HISPANIA: Mabingwa wa La Liga, Barcelona wamefikia makubaliano ya kumsajili nahodha wa timu ya taifa ya Hispania, Rodri, kutoka Manchester City kwa ada inayokadiriwa kufikia pauni milioni 65.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 30, ambaye alitwaa tuzo ya Ballon d’Or mwaka 2024, anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka minne na Barcelona, huku uhamisho huo ukitarajiwa kukamilika ndani ya siku chache zijazo.

Rodri anaondoka Manchester City baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa misimu saba yenye mafanikio makubwa, akicheza jumla ya mechi 298 tangu alipojiunga nayo akitokea Atletico Madrid mwaka 2019 kwa ada iliyokuwa rekodi ya klabu hiyo ya pauni milioni 62.8.

Hata hivyo, safari yake ya mwisho akiwa City ilikumbwa na majeraha. Alikosa sehemu kubwa ya msimu wa 2024/25 baada ya kupata jeraha kubwa la goti, huku msimu uliopita pia akitatizwa na tatizo la misuli ya nyuma ya paja.

Licha ya changamoto hizo, Rodri alirejea katika kiwango chake bora kwenye Kombe la Dunia lililofanyika majira ya kiangazi, akiongoza Hispania kutwaa ubingwa wao wa pili wa dunia na kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa michuano hiyo.

Kwa jumla, Rodri anaondoka Etihad akiwa ameshinda mataji 12 makubwa, yakiwemo manne ya Ligi Kuu England, mawili ya FA Cup, matatu ya EFL Cup na Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2022/23.

RODR 05

Real Madrid yashindwa, Barca yafanya kweli

Wiki iliyopita, Manchester City ilikataa ofa ya kwanza ya Barcelona ya pauni milioni 38.5 kwa ajili ya Rodri, ambaye alikuwa akielekea kuingia mwaka wa mwisho wa mkataba wake na klabu hiyo.

Awali, Real Madrid ilionekana kuwa kwenye nafasi nzuri zaidi ya kumnasa kiungo huyo, lakini Barcelona iliongeza nguvu katika harakati zake siku za hivi karibuni na sasa imefanikiwa kufikia makubaliano ya kumsajili.

Kocha mpya wa Manchester City, Enzo Maresca, alikiri umuhimu wa Rodri baada ya timu yake kufungwa na Arsenal katika Community Shield Jumapili.

“Rodri ni mchezaji ambaye ameshinda Kombe la Dunia na Ballon d’Or. Ni mchezaji wa kiwango cha juu. Kila timu inamhitaji mchezaji kama Rodri, hivyo suala si kama tutamkosa Rodri au la,” alisema Maresca.


RODR 04

Bouaddi kuchukua nafasi ya Rodri?

Manchester City imekuwa ikihusishwa kwa muda wote wa majira haya ya usajili na kiungo wa Lille mwenye umri wa miaka 18, Ayyoub Bouaddi, ambaye anaripotiwa kuwa chaguo moja la kuchukua nafasi ya Rodri.

City tayari inadaiwa kufanya mazungumzo na mchezaji huyo raia wa Morocco, ambaye thamani yake inakadiriwa kufikia pauni milioni 85, huku Bouaddi akielezwa kuwa tayari kuhamia Etihad.

Bouaddi alivutia kwenye Kombe la Dunia la majira haya ya kiangazi, baada ya awali kuanza kujijengea jina katika soka la Ulaya kufuatia kiwango chake bora katika ushindi wa Lille dhidi ya Real Madrid katika Ligi ya Mabingwa mwaka 2024.

Kiungo huyo anacheza zaidi kama kiungo wa chini anayesimamia ujenzi wa mashambulizi, jukumu linalofanana kwa kiasi kikubwa na lile la Rodri.

Uwepo wake unaweza pia kwenda sambamba na usajili mpya wa City, Elliot Anderson, ambaye ana sifa zaidi za kiungo anayepanda na kushuka katika eneo lote la uwanja.

City pia inahitaji kuziba pengo lililoachwa na Bernardo Silva na Tijjani Reijnders, hivyo Bouaddi anaweza kuwa sehemu ya mpango mpana wa kuunda upya safu ya kiungo.

Licha ya umri wake mdogo, Bouaddi ana uzoefu wa kutosha baada ya kucheza mechi 30 za Ligue 1 msimu uliopita.


RODR 01

Fernandez bado kwenye rada

Manchester City pia haijaficha nia yake ya kumsajili kiungo wa Chelsea, Enzo Fernandez, licha ya kutowasilisha ofa kabla ya muda wa mwisho uliowekwa na klabu hiyo ya London Ijumaa iliyopita.

Chelsea iliwaambia klabu zilizokuwa zikimhitaji Fernandez kwamba zilipaswa kuwasilisha ofa kabla ya saa 17:00 kwa saa za Uingereza, huku ikimtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 alipwe pauni milioni 120.

Hakuna ofa iliyowasilishwa na sasa Chelsea inatarajia kumbakiza makamu wake wa nahodha.

Hata hivyo, Manchester City bado haijaondoa uwezekano wa kumsajili Fernandez, huku ikiamini Chelsea inaweza kubadili msimamo wake na kukubali kufanya biashara hiyo.

Maresca ni shabiki mkubwa wa Fernandez, ambaye alimpa unahodha wa Chelsea wakati Reece James alipokuwa majeruhi.

Katika mechi 92 ambazo Maresca aliongoza Chelsea, alimtumia Fernandez katika 79.

Ingawa kwa asili Fernandez ni kiungo mkabaji, Maresca mara nyingi alimtumia mbele zaidi msimu uliopita wakati Cole Palmer alipokuwa majeruhi, jambo lililomsaidia kufunga mabao 15, rekodi yake bora kwa msimu mmoja.

Hivyo, Fernandez anaweza kucheza katika nafasi kadhaa kwenye kikosi cha Maresca iwapo City itafanikiwa kumnasa.


RODR 02

Alex Scott naye kwenye rada

Manchester City pia imechunguza uwezekano wa kumsajili kiungo wa Bournemouth, Alex Scott.

Mchezaji huyo wa England mwenye umri wa miaka 22 amekataa ofa kadhaa za mkataba kutoka Bournemouth kutokana na kuvutiwa na klabu nyingine za Ligi Kuu, ingawa mkataba wake wa sasa unaendelea hadi mwaka 2028.

Bournemouth imeweka wazi kuwa inataka kumbakiza Scott na tayari ilikataa ofa ya pauni milioni 64 kutoka Chelsea mwezi uliopita.

Arsenal nayo imewahi kujaribu kumnasa kiungo huyo, lakini jitihada zake ziligonga mwamba.

Nguvu, uwezo wa kubeba mpira na namna Scott anavyoshiriki katika mchezo wa kujenga mashambulizi vinaendana na falsafa ya Maresca inayosisitiza umiliki wa mpira.

Uwezo wake wa kupiga pasi za hatari ndani ya boksi pamoja na kushinda mipambano ya ana kwa ana pia unamfanya kuwa chaguo linalovutia.


RODR 03

Mac Allister pia avutia

Kiungo wa Liverpool, Alexis Mac Allister, ni mchezaji mwingine anayemvutia Maresca.

Raia huyo wa Argentina amebakiza miaka miwili kwenye mkataba wake na Liverpool na amekuwa mhimili muhimu katika safu ya kiungo ya timu hiyo tangu alipojiunga nayo.

Hata hivyo, kiwango chake kilishuka katika msimu wa 2025/26 uliokuwa na changamoto kwa Liverpool.

Mac Allister, ambaye tayari ana uzoefu wa kushinda Ligi Kuu England, angekuwa chaguo lililo tayari kuingia moja kwa moja katika kikosi cha Manchester City na kuongeza uzoefu katika safu yake ya kiungo.