Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Juventus yakwama kumsajili Martinez

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Martinez, 33, ambaye ni kipa wa kimataifa wa Argentina na mshindi wa Kombe la Dunia, amekuwa akihusishwa na uwezekano wa kuondoka Aston Villa katika misimu miwili iliyopita.

TURIN, ITALIA. Mpango wa Juventus kumnasa kipa wa Aston Villa, Emiliano Martinez umeanguka licha ya klabu hiyo ya Ligi Kuu England kuwa tayari imeanza kutafuta mrithi wake.

Martinez, 33, ambaye ni kipa wa kimataifa wa Argentina na mshindi wa Kombe la Dunia, amekuwa akihusishwa na uwezekano wa kuondoka Aston Villa katika misimu miwili iliyopita.

Hata hivyo, Juventus ilionekana kuwa katika nafasi nzuri ya kumsajili msimu huu baada ya kuwasilisha ofa kadhaa kwa Aston Villa kwa ajili ya kipa huyo.

Licha ya jitihada hizo, mpango huo sasa umefikia tamati baada ya Juventus kushindwa kufikia makubaliano na Aston Villa kuhusu ada ya uhamisho.

Kwa mujibu wa taarifa za The Athletic, mabingwa hao wa zamani wa Italia wameamua kuachana na harakati za kumsajili Martinez na sasa wameelekeza nguvu zao kwa makipa wengine wanaowalenga katika dirisha hili la usajili.

Hatua hiyo imekuja wakati Aston Villa tayari ikiwa imeanza kupanga maisha bila Martinez, ikiwa imeanza kutafuta kipa mwingine wa kuchukua nafasi yake endapo ataondoka Villa Park.


Jadon Sancho

WINGA Jadon Sancho anaelekea kuendelea na maisha ya soka nje ya England licha ya kupokea ofa za mikataba kutoka kwa klabu kadhaa za Ligi Kuu England.

Sancho, 26, kwa sasa anapima chaguo mbalimbali kuhusu hatua inayofuata ya maisha yake ya soka baada ya kuachana na Manchester United mwishoni mwa Juni, alipomalizika mkataba wake na klabu hiyo.


Darwin Guagua

BRENTFORD imethibitisha kumsajili kiungo chipukizi wa Ecuador, Darwin Guagua, kutoka Independiente del Valle, klabu iliyomlea nyota wa zamani wa Brighton, Moises Caicedo.

Guagua, mwenye umri wa miaka 18, amesaini mkataba wa miaka mitano na Brentford, ukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka mmoja.


Arne Engels

WEST HAM United imemsajili kiungo wa Celtic, Arne Engels, kwa ada ya pauni milioni 22, ikiwa ni rekodi mpya ya usajili katika Championship.

Engels, 22, amesaini mkataba wa awali wa miaka mitano na West Ham, huku klabu hiyo ikiwa na chaguo la kuongeza mwaka mmoja zaidi kwenye mkataba wake.


Josh Acheampong

COVENTRY City imeingia kwenye mbio za kumsajili beki wa Chelsea, Josh Acheampong, huku mabingwa hao wa England sasa wakionekana kuwa tayari kusikiliza ofa kwa ajili ya mchezaji huyo.

Awali, Chelsea ilikataa ofa kadhaa za kumsajili Acheampong, 20, ikisisitiza kuwa beki huyo aliyelelewa kwenye akademi ya klabu hiyo hayuko kwenye orodha ya wachezaji wanaouzwa.


Louis Page

MANCHESTER United imepata matumaini zaidi katika harakati zake za kumsajili kinda wa Leicester City, Louis Page, baada ya mchezaji huyo kuachwa nje ya kikosi kilichokutana na Notts County.

Page hakujumuishwa kwenye kikosi hicho licha ya kuwa fiti, hali inayozua zaidi maswali kuhusu mustakabali wake ndani ya Leicester.


Jamie Gittens

FENERBAHCE imekanusha taarifa zinazodai kuwa inataka kumsajili winga wa Chelsea, Jamie Gittens, ikieleza kuwa tetesi hizo hazina msingi na ni sehemu ya jitihada za kuipotosha klabu.

Klabu hiyo ya Ligi Kuu Uturuki imetoa taarifa rasmi ikisema haina nia ya kumsajili Gittens, huku ikizitaja taarifa zinazoendelea kusambaa kuwa “hazina msingi” na ni “majaribio ya kuendesha klabu kwa maslahi binafsi.”


Dayann Methalie

SUNDERLAND imefikia makubaliano ya kumsajili beki wa kushoto wa Toulouse, Dayann Methalie, kwa ada ya jumla ya pauni milioni 25.6, sawa na takribani Sh68 bilioni.


Klabu hizo zimefikia makubaliano ya awali ya pauni milioni 23.9, huku pauni nyingine milioni 1.7 zikitarajiwa kulipwa kama bonasi kulingana na utendaji wa mchezaji na masharti ya mkataba.


Nestory Irankunda

MSHAMBULIAJI wa Watford, Nestory Irankunda, ameondoka klabuni hapo baada ya msimu mmoja na kujiunga na vigogo wa Ureno, Sporting Lisbon, kwa uhamisho wa moja kwa moja.

Irankunda, mwenye umri wa miaka 20, alijiunga na Watford Julai 2025 akitokea Bayern Munich, lakini ameshindwa kudumu kwa muda mrefu Vicarage Road.


Arne Engels

WEST HAM United imeweka rekodi mpya ya usajili katika ligi za EFL baada ya kumsajili kiungo Arne Engels kutoka Celtic kwa ada ya pauni milioni 22.

Engels, 22, ambaye ni raia wa Ubelgiji, amesaini mkataba wa miaka mitano na West Ham, ambao msimu huu utashiriki Championship baada ya kushuka daraja kutoka Ligi Kuu England.