Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Happy Birthday Lamine Yamal

YAMAL Pict

Muktasari:

  • Nyota huyo wa Barcelona na timu ya taifa ya Hispania alizaliwa Julai 13, 2007 na hadi sasa tayari ana mataji kadhaa kwa ngazi ya klabu na timu ya taifa.

BARCELONA, HISPANIA: LEO Lamine Yamal anasherehekea siku yake ya kuzaliwa akitimiza umri wa  miaka 18, lakini tayari amefanikisha mambo makubwa katika taaluma yake ambayo Lionel Messi na Cristiano Ronaldo hawakuwahi kuyafanikisha walipokuwa na umri kama wake.

Nyota huyo wa Barcelona na timu ya taifa ya Hispania alizaliwa Julai 13, 2007 na hadi sasa tayari ana mataji kadhaa kwa ngazi ya klabu na timu ya taifa.

Yamal alicheza mechi yake ya kwanza katika kikosi cha wakubwa cha Barcelona mwaka 2023 akiwa na umri wa miaka 15, na tangu wakati huo amefunga mabao 25 katika mechi 106 kwenye mashindano yote.

Winga huyo ameshinda mataji mawili ya La Liga, Copa del Rey na Supercopa de Espana akiwa na Barcelona.

Mwaka huo huo pia aliitwa timu ya taifa ya Hispania, ambapo alicheza mechi yake ya kwanza katika kikosi cha wakubwa.

Yamal ameifungia Hispania mabao sita katika mechi 20 na alikuwa sehemu ya kikosi kilichotwaa ubingwa wa Euro 2024, akisaidia kuishinda England mabao 2-1 katika fainali.

Akiwa na miaka 17, alikuwa mchezaji mdogo zaidi kuwahi kuteuliwa kugombea tuzo ya Ballon d’Or mwaka jana ambapo alimaliza katika nafasi ya 8.

Yamal alipitia katika ngazi za vijana za Barcelona kama alivyofanya Lionel Messi lakini kijana huyu wa Kihispania analinganishwaje na Messi na Cristiano Ronaldo walipokuwa na umri wa miaka 18?

Messi alicheza mechi yake ya ushindani ya kwanza na Barcelona akiwa na miaka 17, Oktoba 2004, akiwa mkubwa kidogo kuliko Yamal alipoanza.

Vilevile, Messi alitimiza miaka 18, Juni 2005, na kufikia wakati huo alikuwa tayari ameshinda taji la La Liga na Barcelona, lakini alikuwa amecheza mechi tisa tu na kufunga bao moja pekee.

Messi alilazimika kusubiri hadi baada ya kutimiza miaka 18 ili acheze mechi yake ya kwanza na timu ya wakubwa ya Argentina, dhidi ya Hungary Agosti 2005.

Kwa upande wa Ronaldo, alianza kuchezea Sporting Lisbon akiwa na miaka 17, Agosti 2002.

Alipofikisha umri wa  miaka 18, Februari 5, 2003, alikuwa tayari amefunga mabao matano katika mechi 19 akiwa na timu hiyo ya Ureno, na baadaye mwaka huo alihamia Manchester United hatua iliyofungua milango zaidi ya  maisha yake ya soka.

Kwa upande wa timu ya taifa ya Ureno, Ronaldo alisubiri hadi alipotimiza miaka 18 ndipo acheze mechi yake ya kwanza katika kikosi cha wakubwa, aliyochezwa Agosti, 2003 dhidi ya Kazakhstan akitokea benchi.

Kimsingi Yamal bado ana safari ndefu sana kufikia mafanikio yao lakini kwa ulinganisho Messi na Ronaldo hawakuwa na wamefikia mafanikio yake ya sasa walipokuwa na umri kama wake.