Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hapa Amorim atawaua nyie

Muktasari:

  • Man United imeingia kwenye dirisha hili la usajili wa majira ya kiangazi ikiwa na mpango mkubwa wa kukifumua na kukifuma upya kikosi hicho baada ya msimu wa hovyo uliopita, lakini jambo hilo linakwenda taratibu sana.

MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER United imetua Marekani kwa ajili ya mazoezi ya pre-season huku kikosi hicho kikiwa kimefanyiwa maboresho nusu, hakijakamilika kwa asilimia 100.

Man United imeingia kwenye dirisha hili la usajili wa majira ya kiangazi ikiwa na mpango mkubwa wa kukifumua na kukifuma upya kikosi hicho baada ya msimu wa hovyo uliopita, lakini jambo hilo linakwenda taratibu sana.

Kichapo kwenye fainali ya Europa League na baada ya timu kumaliza katika nafasi ya 15 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England hilo liliibua maswali mengi sana katika kambi ya timu hiyo. Na kilichoelezwa ni kwamba kocha Ruben Amorim atalazimika kuungwa mkono kwenye dirisha hili la usajili ili kunasa mastaa wa maana wa kuja kuinusuru timu.

Usajili wa mapema wa Matheus Cunha, aliyenaswa kwa Pauni 62.5 milioni kutoka Wolves, ilionekana kama timu imepania, lakini kisha zikapita wiki sita kabla ya usajili wa pili wa mchezaji Bryan Mbeumo, aliyesajiliwa kwa Pauni 71 milioni kutoka Brentford.

Cunha na Mbeumo ni usajili mkubwa wa Man United hadi sasa kwenye dirisha hili, ikifanikiwa kuwanasa wachezaji waliofanya vizuri sana kwenye Ligi Kuu England msimu uliopita. Lakini, Man United kuna kazi ya ziada inayopaswa kufanywa kabla ya dirisha la usajili kufungwa Septemba 1.

Kwanza, timu hiyo inahitaji kupata timu za kuwapeleka mastaa wake watano – Marcus Rashford, Jadon Sancho, Alejandro Garnacho, Antony na Tyrell Malacia. Rashford anakwenda Barcelona kwa mkopo na Sancho anajiunga na Juventus, lakini wachezaji wengine watatu bado haijafahamika na wanapaswa kuondoka.

Sambamba na hilo, Man United itahitaji kuongeza mastaa wengine kwenye timu. Eneo moja muhimu ni la golikipa, huku anayetajwa kusakwa na wakali hao wa Old Trafford katika nafasi hiyo ni kipa wa Aston Villa, Emi Martinez.

Andre Onana alifanya makosa mengi sana msimu uliopita na namba mbili wake, Altay Bayindir alipoingia hakuwa suluhisho bora, hivyo Emi Martinez anatazamwa kama mtu mwafaka wa kwenda kumaliza tatizo la Man United kwenye eneo hilo.

Kipa wa Royal Antwerp, Senne Lammens naye yupo kwenye rada za Man United, ambaye saini yake inaweza kupatikana kwa ada ya Pauni 17 milioni.

Eneo jingine la kufanyia maboresho ni la kiungo wa chini, ambako Casemiro umri umeshaanza kumtupa mkono, Manuel Ugarte amekuwa na kiwango chenye kupanda na kushuka na Kobbie Mainoo – ni kama alivyokuwa Scott McTominay anakuwa bora zaidi anapocheza mbele kuliko kwenye kiungo ya chini.

Kwenye kumaliza tatizo hilo, Man United inahusishwa na kiungo wa Atalanta, Ederson – ambapo Mbrazili huyo anaonekana kama mchezaji atakayekwenda kufiti vyema. Juventus na Inter Milan nazo zimekuwa zikihusishwa na kiungo Ederson, ambaye Atalanta inamthaminisha kuwa na thamani ya Euro 60 milioni, lakini Man United imekuwa na uhusiano mzuri na klabu hiyo ya Italia baada ya kufanya biashara za mastaa Rasmus Hojlund na Amad.

Ujio wa Ederson kwenye kiungo ya chini, utamfanya kocha Amorim kumtumia nahodha wake Bruno Fernandes kwenye eneo moja kati ya nafasi mbili za kiungo wa kati, ambapo wakali wapya Mbeumo na Cunha watacheza kama pacha kwenye Namba 10.

Staa wa Sporting Lisbon, Morten Hjulmand, ambaye Amorim anamfahamu vyema ni chaguo jingine mbadala kwenye kiungo ya chini endapo kama Ederson atakosekana.

Kwenye fowadi, Man United ilijaribu kuwafukuzia mastraika kadhaa. Ilimtaka Hugo Ekitike, ambaye sasa anakaribia kujiunga na Liverpool na Viktor Gyokeres, ambaye yupo kwenye hatua za mwisho kukamilisha dili la kutua Arsenal, wakati sasa orodha ya mastraika inaowataka yumo pia Nicolas Jackson, Ollie Watkins na Benjamin Sesko.

Kwenye eneo hilo, Man United itahitaji kumuuza Rasmus Hojlund ili kutoa nafasi, ambapo straika huyo anasakwa na timu za Italia baada ya kufunga mabao 10 kwenye mechi 52 alizocheza msimu uliopita. Na hilo likifanyika, dhamira ya Man United ni kunasa saini ya Sesko, ambaye anahitaji kutua kwenye Ligi Kuu England dirisha hili.

Sesko ana thaminishwa kuwa na thamani ya Euro 70 milioni na klabu yake ya RB Leipzig na Man United inamtaka kwa mkopo, huku akiminika atakwenda kufiti vyema kwenye mtindo wa soka la kocha Amorim.

Kikosi cha ndoto cha Man United: E Martinez; Yoro, De Ligt, L Martinez; Dalot, Ederson, Fernandes, Dorgu; Mbeumo, Cunha, Sesko