Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gyokeres, Havertz wampa mzuka Arteta

Muktasari:

  • Arteta alimwanzisha straika wake mpya aliyemnasa kwa Pauni 64 milioni kwenye dirisha hili, Gyokeres na alifunga bao lake la kwanza kwa kichwa matata.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta anaamini Viktor Gyokeres na Kai Havertz wanaweza kucheza pamoja baada ya wote kufunga mabao kwenye ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Athletic Bilbao katika mchezo wao wa mwisho wa kirafiki.

Arteta alimwanzisha straika wake mpya aliyemnasa kwa Pauni 64 milioni kwenye dirisha hili, Gyokeres na alifunga bao lake la kwanza kwa kichwa matata.

Havertz, aliyeanzia kwenye benchi katika mechi hiyo na kuingiza dakika 71 aliifungia Arsenal bao la tatu la mwisho katike mechi hiyo baada ya pasi kali ya kupenyeza ya Bukayo Saka.

Kulikuwa na maswali Havertz atawezaje kupata nafasi kwenye timu baada ya ujio wa straika Gyokeres na ilidhaniwa Mjerumani huyo ataanza kuwekwa benchi msimu huu.

Lakini, baada ya mechi, kocha Arteta alisema washambuliaji hao wanaweza kucheza pamoja na kutengenezeana nafasi, huku akidai Havertz anaweza kucheza kwenye kiungo pia.

"Wanaweza kucheza pamoja au Kai akacheza kwenye nafasi tofauti," alisema Arteta na kuongeza. "Hiyo inaelezea viwango kwenye kikosi, machaguo ambayo tunayo na uwezo wa kuwaweka wapinzani kwenye matatizo.

Arteta alisema kuwa na machaguo mengi kwenye safu ya ushambuliaji ni kitu kizuri kitakachompa wakati mgumu msimu huu, tofauti na msimu uliopita na hakuwa na Namba 9 sahihi.

Alisema: "Ni kitu kizuri kuwaona wote wakifunga na wote wakicheza kwenye viwango bora kabisa. Hili ni tatizo zuri kuwa nalo."

Kocha Arteta anafahamu wazi kwenye kikosi chake kutakuwa na ushindani mkali wa namba baada ya ujio wa wachezaji wengine kikosini kama Martin Zubimendi na Noni Madueke, walionaswa kwa Pauni 55 milioni kila mmoja