Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gyokeres ashinda tuzo ya ubora Ureno

GYOKERES Pict

Muktasari:

  • Straika huyo aliyewahi kuzichezea pia Brighton na Coventry alifanya mgomo huko Sporting kulazimisha uhamisho huo wa kutua Arsenal kwa ada ya Pauni 55 milioni dirisha la majira ya kiangazi.

LONDON, ENGLAND: STRAIKA mpya wa Arsenal, Viktor Gyokeres ameishukuru Sporting CP kwa kile alichofanya msimu uliopita licha ya miamba hiyo ya Ureno kumpiga faini ya Pauni 306,000 kutokana na kufanya mgomo wa kuhama.

Straika huyo aliyewahi kuzichezea pia Brighton na Coventry alifanya mgomo huko Sporting kulazimisha uhamisho huo wa kutua Arsenal kwa ada ya Pauni 55 milioni dirisha la majira ya kiangazi.

Gyokeres alikosa mechi za kujiandaa na msimu huko Sporting alipokuwa akigomea kujiunga na timu hiyo kulazimisha kwenda Arsenal.

Jambo hilo limemfanya straika huyo kupigwa faini na klabu yake, ambayo atailipa sasa akiwa kwenye timu nyingine kabisa huko Emirates.

Lakini, Gyokeres hakujali na badala yake amewashukuru Sporting pamoja na mashabiki wa timu hiyo baada ya kuchaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Primeira Liga kwa mwimu wa 2024/25. Alimaliza ligi ya Ureno akiwa kinara wa mabao.

“Nimefurahi sana kupokea tuzo hii,” alisema straika huyo wa kimataifa wa Sweden na kuongeza. “Bahati mbaya sikuwa mimi niyeipokea, lakini nawashukuru wachezaji wengi, benchi la ufundi na mashabiki wa Sporting kwa kufanikisha hili na sapoti waliyonipa kwa msimu mzima.

“Ulikuwa msimu wa kipekee, tulishinda Primeira Liga na Kombe la Ureno. Nawashukuru sana na hongera kwa washindi wengine. Nawashukuru wale walionipigia kura. Nawapenda nyote.”

Gyokeres alifunga mabao 97 katika mechi 102 alizochezea Sporting, huku mabao 54 alifunga katika mechi 52 alizocheza msimu uliopita.

Aliasisti mara 14 pia kwenye michuano yote aliyocheza msimu uliopita, huku kwenye kikosi cha Arsenal tayari ameshafanya mambo yake baada ya kufunga mara mbili kwenye Ligi Kuu England.