Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Guehi aikataa Man City, Arsenal, Liverpool zatajwa

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Man City iliingia katika harakati za kumsajili staa huyu baada ya kuumia kwa mabeki wao Ruben Dias na Josko Gvardiol, ambao wanasumbuliwa na majeraha ya muda mrefu yanayoweza kuwaweka nje kwa muda mrefu.

BEKI wa Crystal Palace, Marc Guehi inadaiwa kukataa kujiunga na Manchester City na badala yake anataka kujiunga na Arsenal au Liverpool ambazo zimeonyesha nia ya kumsajili dirisha la majira ya baridi.

Man City iliingia katika harakati za kumsajili staa huyu baada ya kuumia kwa mabeki wao Ruben Dias na Josko Gvardiol, ambao wanasumbuliwa na majeraha ya muda mrefu yanayoweza kuwaweka nje kwa muda mrefu.

Dirisha lililopita Guehi alikuwa karibu kujiunga na Liverpool lakini dili lilifeli dakika za mwisho baada ya kocha kuzuia na kutishia kuondoka ikiwa fundi huyo angeuzwa.

Kwa sasa Palace inaonekana kutaka kumuuza dirisha hili kwa sababu Guehi amegoma kusaini mkataba mpya hivyo inahofia kuona akiondoka bure mwisho wa msimu huu mkataba wake utakapomalizika.

Tangu kuanza kwa msimu huu, beki huyu amecheza mechi 33 za michuano yote, amefunga mabao matatu na kutoa asisti nne.


Ben White

EVERTON imeonyesha nia ya kumsajili beki wa Arsenal, Ben White, 28, kwa ajili ya kutatua tatizo lao la muda mrefu la beki wa kulia.

White amekuwa hapati nafasi ya kutosha Arsenal tangu kuanza kwa msimu huu hali inayosababisha afikirie kutaka kuondoka ili kupata muda mwingi zaidi wa kucheza na kufufua matumaini ya kuitwa katika timu ya taifa ya England kuelekea michuano ijayo ya Kombe la Dunia.

Hata hivyo, uamuzi wa mwisho utategemea msimamo wa Arsenal pamoja na dhamira ya mchezaji mwenyewe.


Oscar Bobb

BORUSSIA Dortmund inaendelea kumfuatilia kwa karibu kiungo mshambuliaji wa Manchester City, Oscar Bobb, 22, ambaye anaweza kuruhusiwa kuondoka baada ya City kumsajili winga wa Bournemouth, Antoine Semenyo, 26.

Ujio wa Semenyo umeongeza ushindani mkubwa wa namba katika safu ya ushambuliaji wa Man City jambo lililomfanya Bobb kuanza kufikiria kuhusu kuondoka hata kwa mkopo.

Dortmund wanamwona Bobb kama chaguo sahihi la kuimarisha kikosi chao kuelekea msimu ujao.


Conor Gallagher

TOTTENHAM Hotspur bado inahitaji kumsajili kiungo wa Atletico Madrid, Conor Gallagher, 25, licha ya Aston Villa kuonekana kuwa mbele zaidi katika dili hilo.

Gallagher alikuwa akifanya vizuri Atletico tangu ajiunge nayo kutoka Chelsea, lakini hivi karibuni mambo yanaonekana kumwendea kombo.

Mabosi wa Atletico wanadaiwa kuhitaji zaidi ya Pauni 50 milioni ili kumuuza staa huyu na haina haraka sana kufanya hivyo kwa sababu bado inamhitaji.


William Osula

ASTON Villa imeingia vitani kumwania mshambuliaji wa Newcastle United, William Osula, 22, baada ya kukumbana na kikwazo katika harakati zao za kumsajili straika wa timu ya vijana ya Real Madrid, Gonzalo Garcia, 21.

Villa inataka kuongeza nguvu kwenye ushambuliaji na wanamwona Osula kama chaguo sahihi.

Newcastle bado haijaweka wazi kama iko tayari kumuachia mchezaji huyo, lakini mazungumzo yanatarajiwa kuanza hivi karibuni.


Jacobo Ramon

LIVERPOOL na Chelsea zimeonyesha kuvutiwa na beki wa kati wa Como, Jacobo Ramon, 21, kutokana  na kiwango alichoonyesha tangu msimu uliopita Serie A.

Ramon amekuwa akifuatiliwa pia na klabu nyingine za Ligi Kuu England ambazo zimekuwa zikituma maskauti wao kumtazama mara kwa mara.

Como inadaiwa kuhitaji zaidi ya Pauni 30 milioni ili kumuuza staa huyu na kuna uwezekano dau hilo likazidi kutokana na wingi wa timu zinazomhitaji.


Mathys Tel

PARIS FC ni miongoni mwa timu zilizoonyesha nia ya kumsajili winga wa Tottenham, Mathys Tel kwa mkopo dirisha hili.

Licha ya timu kuonyesha nia ya kumsajili, taarifa zinadai Tel anahitaji kuendelea kusalia Spurs na kupambania namba. Mkataba wa sasa wa staa huyu unatarajiwa kumalizika mwaka 2031. Msimu huu amecheza mechi 19 za michuano yote na kufunga mabao matatu.


Dayot Upamecano

BEKI wa Bayern Munich, Dayot Upamecano, 27, anatarajiwa kuendelea kusalia Allianz Arena hadi mwaka 2031 ikiwa ni baada ya kukataa ofa ya Real Madrid iliyokuwa inahitaji.

Msimu huu amecheza mechi 22 za michuano yote na kufunga bao moja. Awali pia alikuwa akihusishwa na Liverpool akawe mbadala wa Ibrahim Konate ambaye mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu.