Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Guardiola afichua alichowaambia wachezaji wake kuhusu Arsenal

PEP Pict

Muktasari:

  • Arsenal ililazimishwa sare ya 2-2 dhjidi ya Sunderland juzi Jumamosi, Novemba 8, 2025, matokeo ambayo yalitoa ahueni kwa Man City iliyokuwa bado haijacheza dhidi ya Liverpool katika Uwanja wa Etihad.

Meneja wa Manchester City, Pep Guardiola, amefichua kuwa aliwaambia wachezaji wake wasahau matokeo ya 2-2 ya Arsenal dhidi ya Sunderland, kabla ya mechi yao dhidi ya Liverpool jana Jumapili, Novemba 9, 2025.

Arsenal ililazimishwa sare ya 2-2 dhjidi ya Sunderland juzi Jumamosi, Novemba 8, 2025, matokeo ambayo yalitoa ahueni kwa Man City iliyokuwa bado haijacheza dhidi ya Liverpool katika Uwanja wa Etihad.

Matokeo hayo yalifungua nafasi kwa Manchester City au Liverpool kufuatilia nafasi ya juu katika jedwali la ligi.

Hata hivyo, Guardiola amefichua alichozungumza na wachezaji wake, baada ya mechi ya Liverpool ambayo ilikubali kichapo cha 3-0, na kuendelea kutoa mwanya kwa miamba hiyo ya Jiji la Manchester kuingia katika mbio za ubingwa sambamba na Arsenal.

PE 01

Guardiola amesema alitambua wachezaji wake walifurahishwa na matokeo ya Arsenal, lakini alichokifanya ni kuwarudisha katika mawazo ya mechi iliyokuwa inawakabili, ambayo pia ilitakiwa washinde ili kuingia kwenye mbio za ubingwa msimu huu.

“Sikutaka kabisa wachezaji wangu wajiingize kwenye matokeo ambayo hayatuhusu kabla ya mechi yetu na Liverpool, nilichukua jukumu la kuwatafuta na kuwahimiza jambo la kuhakikisha tunapambana na kupata matokeo mazuri dhidi ya Liverpool.

PE 02

“Ninashukuru tumeshinda mechi yetu na Liverpool, hivyo lengo letu limetimia. Tunajua matokeo ya Arsenal yalitupa mwanya wa kupambana na kujituma zaidi, lakini nilitaka tujikite zaidi katika jambo linalotuhusu na kuacha mengine ambayo hayakuwa na msaada kabla ya mechi yetu na Liverpool,” amesema Guardiola.

Kwa sasa, Arsenal inaongoza msimamo wa Ligi ya EPL kwa tofauti ya pointi nne na Manchester City inayoshika nafasi ya pili, kuelekea mapumziko ya mechi za kimataifa, na wanatarajiwa kurejea kwa nguvu kutafuta ushindi katika mchezo wao ujao wa ligi.