Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Georgina afunguka uhusiano wake na Cristiano Jr

JOJINA Pict

Muktasari:

  • Ingawa Georgina si mama mzazi wa Cristiano Jr mwenye umri wa miaka 16, amekuwa akimlea kama mtoto wake tangu aanze uhusiano na Ronaldo mwaka 2016.

LISBON, URENO: MCHUMBA wa nyota wa Al-Nassr na Ureno, Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez, ameeleza jinsi anavyothamini muda anaoutumia na Ronaldo pamoja na mtoto wake wa kwanza, Cristiano Jr, akisema likizo yao ya kila mwaka imekuwa sehemu ya kumbukumbu maalumu kwa familia yao.

Georgina aliweka picha mbalimbali kupitia ukurasa wake wa Instagram zikimuonyesha akiwa na Ronaldo na Cristiano Jr wakifurahia maisha katika kisiwa cha Mallorca, Hispania, wakila vyakula vya kifahari, kutembelea maeneo ya pwani na kuendesha jet ski.

Ingawa Georgina si mama mzazi wa Cristiano Jr mwenye umri wa miaka 16, amekuwa akimlea kama mtoto wake tangu aanze uhusiano na Ronaldo mwaka 2016.

JOJI 01

Katika ujumbe wake wa hisia, Georgina amesema safari hiyo imekuwa desturi maalumu kwa familia yao kwa miaka mingi.

"Ilikuwa ndoto yangu kuoga kwenye maporomoko ya maji. Junior ni msanii na ana kipaji katika kila jambo analolifanya. Tangu akiwa mdogo, safari hii imekuwa muda wetu maalumu; baba, mama na yeye, pamoja baharini kila majira ya kiangazi," aliandika.

Pia, alimwelezea Ronaldo kama mtu anayependa kugundua maeneo mapya, huku akifichua kuwa safari ya mwaka huu iliwapa nafasi ya kutembelea fukwe nyingi za kuvutia.

"Mwaka huu tumegundua maeneo mengi mazuri ya pwani. Chakula ninachokipenda zaidi ni nyama ya ng'ombe iliyochomwa kwenye jiwe la moto," ameongeza.

JOJI 02

Hadi sasa, utambulisho wa mama mzazi wa Cristiano Jr umeendelea kubaki siri, huku Ronaldo akiwa na haki zote za malezi ya mtoto huyo.

Katika mahojiano ya awali, mshindi huyo mara tano wa Ballon d'Or amesema atamweleza mwanawe ukweli kuhusu mama yake wakati utakapofika.

"Kuna mambo binafsi ambayo watu wanapaswa kuyaheshimu. Cristiano akikua nitamweleza ukweli kwa sababu anastahili kuujua, lakini si kwa sababu watu wanataka nijibu," amesema Ronaldo.

Cristiano Jr anafuata nyayo za baba yake katika soka na kwa sasa anacheza katika timu za vijana za Al-Nassr nchini Saudi Arabia.

Wakati huohuo, Ronaldo na Georgina wanatarajiwa kufunga ndoa mwishoni mwa wiki hii katika kanisa kuu la Funchal, kwenye kisiwa cha Madeira, kabla ya kufanya sherehe kubwa katika Hoteli ya nyota tano ya Savoy Palace.

JOJI 03

Kwa pamoja, wawili hao wanalea watoto watano wa Ronaldo kama familia moja. Watoto Eva Maria na Mateo walizaliwa kwa njia ya mama wa kubeba ujauzito mwaka 2017, huku Georgina na Ronaldo wakimpata binti yao wa kwanza pamoja, Alana Martina, baadaye mwaka huo.

Mwaka 2022 walipata mtoto wao wa pili, Bella Esmeralda, huku pacha wake Angel akifariki dunia wakati wa kujifungua.

Ronaldo na Georgina walikutana mwaka 2016 wakati Georgina alipokuwa akifanya kazi kama mhudumu wa mauzo katika duka la bidhaa za kifahari la Gucci.