Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gary Neville amchana Milos Kerkez, afichua udhaifu wa Liverpool

Muktasari:

  • Kerkez alipewa jukumu la kuanza kwenye mechi hiyo lakini hakufanya vizuri kipindi cha dakika 55 alichokaa uwanjani, huku Liverpool ikipata kipigo cha tatu mfululizo. 

Gwiji wa soka nchini England, Gary Neville ametoa tathmini kuhusu mlinzi wa Liverpool, Milos Kerkez, baada ya kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Chelsea kwenye Uwanja wa Stamford Bridge jana Jumamosi Oktoba 04, 2025. 

Kerkez alipewa jukumu la kuanza kwenye mechi hiyo lakini hakufanya vizuri kipindi cha dakika 55 alichokaa uwanjani, huku Liverpool ikipata kipigo cha tatu mfululizo. 

Neville ametoa tathmini yake kuhusu uchezaji wa mchezaji huyo raia wa Hungary, akiamini hawezi kukidhi kiwango cha Ligi ya EPL.

Neville ameiambia Sky Sports kwamba: "Milos Kerkez anaonekana kama mchezaji wa timu ya vijana, najua ni mchezaji mzuri, lakini anaoneka kama anacheza kwa timu ya chini ya umri wa miaka 21. Anaonekana ana ujinga mwingi, ambao hauwezi kuisaidia Liverpool inayotetea ubingwa wa EPL. Alipoteza mipira 50-50 dhidi ya Pedro Neto. Si kwamba anatoka nchi tofauti, ameshacheza michezo mingi katika Premier League."

NEV 02

Neville amesisitiza kwamba Kerkez anapaswa kujifunza mambo mengi katika uwanja wa mazoezi ili kuwa makini katika mechi za EPL, lakini badala yake amedhihirisha kuwa na changamoto ya uelewa kwenye michezo mikubwa kama hii. 

Ameongeza: "Nilitarajia angeweza kupata uzoefu kutoka kwa wachezaji wenzake ambao wana ubora, hasa ukizingatia anamzunguka Virgil van Dijk, ambaye ni kati ya mabeki bora duniani, lakini ameshindwa kudhihirisha hilo kwa vitendo."

Neville amebainisha kuwa alianza kumfuatilia Kerkez wakati wa mechi dhidi ya Bournemouth mwezi wa Agosti, na aligundua ana tatizo kubwa katika uchezaji wake.

NEV 01

Kuhusu beki zingine za pembeni za Liverpool, Neville pia ameonya kuhusu Jeremie Frimpong, Conor Bradley, na Andy Robertson kwa kusema wote hao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali.

Pia, Neville hakusita kuzungumzia wachezaji wa safu ya ushambuliaji ya Liverpool, akidai kwamba wana uwezo na ubunifu, lakini kwenye mechi ya jana dhidi ya Chelsea walipoteza nafasi nyingi hali mbayo imeigharimu The Reds.

Neville amemtaja Mohamed Salah kwa kusema ni mchezaji mahiri wa Liverpool, lakini alishindwa kufanya maajabu kwenye mechi hiyo, ingawa ni mchezaji wa kipekee kwa kipindi cha miaka mingi. 

Amesema: "Salah ni bora sana, hawezi kuhukumiwa kwa ubora wake, lakini maamuzi yake na udhaifu wake katika dakika za mwisho viliweza kuigharimu kwa kiasi kikubwa Liverpool."

NEV 03

Kupoteza kwa Liverpool mbele ya Chelsea, kumeifanya timu hiyo ya Anfield kushuka hadi nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi ya EPL ikiwa na pointi 15, huku Arsenal ikipanda kileleni kwa kufikisha pointi 16.

Arsenal ilishinda mechi yake wa jana Jumamosi, Oktoba 4, 2025 dhidi ya West ham United kwa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Emirates.

Matokeo ya mechi zingine za EPL zilizochezwa jana ni Leeds United 1-2 Tottenham Hotspur na Manchester United 2-0 Sunderland.