Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Garnacho akataa ofa ya waarabu, Napoli yajisogeza

TETESI Pict

Muktasari:

  • Inaelezwa Garnacho mwenye umri wa miaka 21, anatamani zaidi kuendelea kucheza soka England na ikishindikana atajiunga na timu nyingine  nje ya England lakini itakuwa ni barani Ulaya.

WINGA wa Manchester United, Alejandro Garnacho, amekataa ofa ya kujiunga na Al Nassr ya Ligi Kuu Saudi Arabia, katika dirisha hili la majira ya kiangazi.

Inaelezwa Garnacho mwenye umri wa miaka 21, anatamani zaidi kuendelea kucheza soka England na ikishindikana atajiunga na timu nyingine  nje ya England lakini itakuwa ni barani Ulaya.

Katika dirisha lililopita la majira ya baridi Napoli iliweka wazi inamhitaji na ikaweka mezani ofa ya Pauni 40 milioni lakini ilikataliwa na inaelezwa mabosi wa Man United wanahitaji kiasi kisichopungua Pauni 50 milioni ili kumuuza.

Garnacho ni miongoni mwa wachezaji ambao Man United imepanga kuwauza dirisha hili kwa ajili ya kupata pesa ambazo zitawawezesha kuboresha kikosi zaidi kwa sababu wao hawapo kwenye mipango ya kocha Ruben Amorim ambaye amewaambia kuwa watafute timu za kucheza kwa msimu ujao.

Fundi huyu wa kimataifa wa Argentina, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2028 na kwa timu za England, Aston Villa inaonekana kuhitaji huduma yake.

Msimu uliopita alicheza mechi 58 za michuano yote na kufunga mabao 11.

Kocha wa Man United, alisema kuwa staa huyu hafanyi vile ambavyo anamwelekeza ndiyo maana hajamweka katia mipango yake na pamoja na nyota wengine kadhaa wameambiwa watafute mahali pa kwenda ili kupisha sajili nyingine zitakazoendana na kasi ya Amorim.


Leandro Trossard

BAYERN Munich imepanga kuhamishia nguvu zao kwa mshambuliaji wa Arsenal na timu ya taifa ya Ubelgiji, Leandro Trossard, mwenye umri wa miaka 30, iwapo itashindwa kufikia makubaliano ya kumsajili winga wa Liverpool mwenye umri wa miaka 28, Luis Diaz katika dirisha hili. Mabosi wa Bayern wanapambana sana kuboresha eneo lao la ushambuliaji ili kuhakikisha inafanya vizuri zaidi kwa msimu ujao na kutetea taji lao la ligi.


Evan Ferguson

MSHAMBULIAJI wa Brighton, Evan Ferguson, amefanya makubaliano binafsi ya kujiunga na  AS Roma katika dirisha hili na sasa dili hilo limebakia upande wa timu juu ya ada ya uhamisho. Majadiliano baina ya timu zote mbili yanaendelea na kuna uwezekano Roma ikatoa ofa ya Euro 20 milioni kukamilisha dili la mshambuliaji huyo wa Jamhuri ya Ireland mwenye umri wa miaka 20. Mkataba wa sasa Ferguson unamalizika mwaka 2029.


El Hadji Malick Diouf

WEST Ham imefikia makubaliano ya kumsajili beki wa pembeni wa Slavia Prague, El Hadji Malick Diouf, mwenye umri wa miaka 20 kutoka Senegal. Diouf ni miongoni mwa wachezaji tegemeo katika kikosi cha Slavia Prague na timu nyingi kubwa barani Ulaya zimekuwa zikipambana sana kuipata saini yake katika dirisha hili. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.


Johan Bakayoko

NOTTINGHAM Forest inakumbana na ushindani wa kutosha kutoka kwa timu nyingine za Ulaya katika harakati za kumsajili winga wa PSV, Johan Bakayoko. Forest ambayo inahitaji kumsajili Bakayoko katika dirisha hili inamwangalia staa huyu kama mbadala sahihi wa Anthony Elanga ambaye ameuzwa kwenda Newcastle wiki iliyopita. Bakayoko mwenye umri wa miaka 22, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2026.


Neil El Aynaoui

EVERTON imeingia katika vita dhidi ya AS Roma kuiwania saini ya  kiungo wa RC Lens na timu ya taifa ya Morocco, Neil El Aynaoui mwenye umri wa miaka 24, katika dirisha hili. Hata hivyo, tovuti ya Teamtalk inafichua Roma imeshafikia makubaliano binafsi juu ya masilahi ya mchezaji na sasa inazungumza na Lens kuhusu ada ya uhamisho ili kumaliza dili. Mkataba wake unamalizika mwaka 2027.


Marco Bizot

KIPA wa Brest, Marco Bizot mwenye umri wa miaka 34, anatarajiwa kusaini mkataba na Aston Villa wiki hii na atasafiri kwenda England kwa ajili ya kumaliza kila kitu. Bizot anasajiliwa kama mbadala wa Emiliano Martinez ambaye kuna uwezekano mkubwa akaondoka dirisha hili ambapo timu vigogo barani Ulaya zinahusishwa naye.


Granit Xhaka

NEOM ya Saudi Arabia imewasilisha ofa nono kwenda Bayer Leverkusen kuipata huduma ya kiungo wa timu hiyo na Uswiss, Granit Xhaka katika dirisha hili. Mbali ya ofa ilyoiwasilisha kwenda kwa Leverkusen, matajiri hao pia wamewasilisha ofa nono ya mshahara kwa Xhaka inayoripotiwa kufikia Euro 25 milioni kwa mwaka.