Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Financial Fair Play ilivyookoa klabu za England, Hispania - 2

JANA tuliona dhamira kuu ya uanzishwaji wa Financial Fair Play kwenye soka la Ulaya ambapo lengo kuu lilikuwa kuweka udhibiti kwenye matumizi ya pesa ili kuzilinda klabu zisifanye matumaini makubwa kuzidi mapato wanayokusanya kwa lengo la kuzifanya kuwa na maendeleo endelevu.

Tumeona pia msukumo mkubwa uliosababisha hilo kutokana na klabu nyingi hasa kwenye Ligi Kuu England, Serie A na La Liga, ambapo kulikuwa na klabu nyingi zilizokuwa na madeni makubwa kiasi cha kutishia uwezekano wa kuendelea kujiendesha kutokana na kufanya matumizi makubwa kuzidi mapato yao. Je, hali ilikuwaje kwenye ligi za nchi hizo na FFP ilikuwa na malengo gani thabiti kwenye maeneo hayo.

Ligi Kuu England
Ripoti ya Deloitte ilifichua kwamba jumla ya deni lote la klabu 20 za Ligi Kuu England kwa mwaka 2008–09 lilikuwa Pauni 3.1 bilioni.

Katika kipindi ambacho FFP inatambulishwa, klabu kadhaa za Ligi Kuu England zilikuwa na matumizi makubwa kuliko mapato yao. Kwa mfano, kati ya 2005 na 2010, West Ham United ilirekodi hasara ya pesa taslimu Pauni 90.2 milioni.
Wakati huo, Everton, ambayo kocha wao wa zamani David Moyes alikuwa akipewa sifa kwa kuifanya klabu hiyo kucheza kwa kiwango bora kwenye Ligi Kuu England bila ya kuwa na bajeti kubwa ya usajili, yenyewe ilitangaza hasara ya Pauni 3.1 milioni kwenye akaunti zake.

Hali mbaya zaidi ilikuwa kwenye vitabu vya fedha vya Portsmouth, ambayo ilirekodi hasara ya Pauni 59,458,603 hadi kufikia Februari 2010 baada ya kutoa thamani ya mali zake, baada ya kuwekeza kwa kiwango kikubwa kwenye kikosi chao misimu kadhaa iliyopita na hasara hiyo ilifidiwa na mfanyabiashara, Alexandre Gaydamak.

Portsmouth ilishika namba mbili kwenye Kombe la FA msimu wa 2010, lakini hali yao ya kiuchumi ilikuwa mbaya ikishindwa kulipa mishahara wachezaji wake na klabu ikawekwa chini ya utawala kuogopa isishuke daraja.
Kutokana na kushindwa kujiendeesha yenyewe na kuwekwa chini ya utawala, klabu hiyo ilipokwa pointi tisa kwenye Ligi Kuu England na matokeo yake ikashuka daraja. Jambo kama hil liliitokea pia Leeds United.

Suala la kuwa na madeni halikuwa likionekana tatizo kwa klabu za ngazi ya juu, ambapo kwa mfano timu za ligi ya pili kwa ukubwa England, Championship zilikuwa zikiwekeza pesa nyingi kwenye vikosi vyao kwa ajili ya kujaribu kupanda daraja ili zicheze Ligi Kuu England.

Katika ripoti ya mwaka 2010–2012 ya bunge, ilifichua kwamba timu nyingi za England hasa zile za ligi za chini zilikuwa zikitumia pesa nyingi kwenye kuwekeza katika vikosi vyao kwa ajili ya kupanda daraja wacheze Ligi Kuu England, ambako kulikuwa na fursa nyingi za kupiga pesa.
Kwa sababu waliamini madeni yote wanayokusanya kutoka kwenye ligi za chini yatakwenda kujilipa yenyewe wakati watakapopanda Ligi Kuu England kutokana na mapato yake kuwa makubwa. Matokeo yake, timu zikatengeneza madeni makubwa kuliko mapato yao.

Serie A
Kwenye ligi ya Serie A huko Italia, klabu nyingi zilirekodi hasara kwenye mapato yao kwa misimu iliyotangulia. Milan ilitangaza hasara ya Euro 69.751 milioni hadi Desemba 2010; Genoa hasara ya Euro 16,964,706 hadi Desemba 31 2010; Fiorentina Euro 9,604,353, Bologna Euro 4,166,419 kufika Juni 30. 2011; na Chievo ilitangaza hasara ya Euro 527,661, Juni 30 2011 kwa kuzitaja tu kwa uchache kwa klabu za Italia.

Kulikuwa na timu chache sana za Italia zilizopata faida na hiyo ilikuwa pamoja na Udinese, Catania, Napoli (Euro 4,197,829 – Juni 30, 2011) na Lazio (Euro 9,982,408 kwenye akaunti zao kufikia Juni 30, 2011. Kuna baadhi ya klabu za Italia zilipoteza pesa nyingi sana, ikiwamo Inter Milan iliyopoteza jumla ya Euro 1.3 bilioni kwa miaka 16 iliyopita, wakati Mei 20, 2005, Lazio ilikubali kulipa deni la Euro 140 milioni kwa miaka 23. Klabu zilijikuta kwenye hatari kubwa kwa kuweka rehani mali zao. Kutokana na hilo, ilifanya klabu nyingi hasa zile zilizokuwa na wamiliki binafsi, mabilionea kutumia pesa zao za nje ya soka kujaribu kuweka mambo sawa. Kitu hicho ndicho kilichoonekana na Uefa si sahihi na kutaka pesa inayopatikana kwenye mpira ndiyo hiyo hiyo ifanye kazi za kimpira. Timu nyingi zilikumbwa na jambo la namna hiyo huko Italia ikiwamo AS Roma.

La Liga
Licha ya ripoti kuonyesha ongezekano la asilimia 8 la mapato kwenye La Liga, ikiwa ni kubwa kwa kulinganisha na ligi nyingine za Ulaya, lakini sehemu kubwa ya pesa hiyo ilikuwa kwa klabu mbili kubwa, Real Madrid na Barcelona, ambazo zenyewe kimsingi zilikuwa na uwezo wa kuingia mikataba ya pesa nyingi ya haki za televisheni. Zenyewe zilikuwa zikiingia dili tofauti za haki za televisheni kwa kulingana na klabu nyingine kwenye ligi hiyo ya Hispania. Kwa mfano, majira ya kiangazi 2009, Real Madrid ililipa ada iliyovunja rekodi ya dunia ya Pauni 80 milioni kunasa saini ya Cristiano Ronaldo. Kwa kutangazwa kuwa klabu taji duniani kwa mujibu wa Forbes, Real Madrid ilitumia pesa nyingi pia kwa wakali wengine wawili, Kaka na Karim Benzema, huku ikiwalipa pia mishahara mikubwa, jambo hilo likazidisha mara tatu madeni ya Los Blancos kutoka Euro 130 milioni, Juni 30, 2008 hadi Euro 326.7 milioni, Juni 30, 2009, baada ya usajili wao wa Raul Albiol, Benzema, Kaka, Ronaldo, Alvaro Negredo na wengineo. Real Madrid iliongeza usajili mwingine wa mchezaji mwenye jina kubwa, Xabi Alonso kutoka Liverpool, Agosti 2009.

Lakini, Juni 30, 2010 deni lao lilishuka kutoka Euro 326.7 milioni hadi Euro 244.6 milioni, hata hivyo liliendelea kuwa kubwa kwa misimu minane iliyotangulia. Hali haikuwa tofauti kwa Barcelona pia, nao walikuwa na matumizi makubwa na walilazimika kupunguza sana baada ya sheria ya udhibiti kuanza.

Kwa ujumla, deni la La Liga lilikisiwa kuwa Pauni 2.5 bilioni na hapo iliwafanya wamiliki wengi wa klabu hizo kwa siku za nyuma, kutumia pesa zao za mfukoni kuzieendesha klabu.
Mwaka 2010, Villarreal ilishindwa kuwalipa wachezaji wake mishahara ambapo mmiliki wao Fernando Roig alitumia pesa hadi amefikia ukomo. Mwishoni mwa mwaka huo, Deportivo de La Coruna ilikuwa na deni la Euro 120 milioni, Atletico Madrid ilidaiwa zaidi ya Euro 300 milioni, wakati Valencia kwa wakati fulani mwaka 2009 deni lake liliripotiwa kufikia Euro 547 milioni.

Hilo lilitokea baada ya uamuzi wa mwaka 2007 wa Valencia kujenga uwanja wenye uwezo wa kuingiza watazamaji 70,000 wakilenga kupata mapato kwenye viingilio vya mashabiki. Ukajengwa Mestalla. Lakini, mradi huo haikuleta matunda makubwa na makovu ya madeni hayo ndiyo yaliyoishusha ubora Valencia na sasa kuonekana kuwa kama timu ya kawaida kwenye soka la Italia.

Kupunguza makali ya uchumi, Valencia ililazimika kuuza wachezaji wake mahiri kama David Silva, David Villa na Juan Mata baada ya awali kufanya matumizi makubwa kuzidi kipato chao na hivyo ikaanza kutaabika kwenye kujiendeesha.
Kwenye ligi za chini huko Hispania, timu zisizopungua sita wakiwamo Real Sociedad, Celta de Vigo na Levante, ziliwekwa chini ya utawala baada ya hali yao ya uchumi kuw ambaya. Julai 2008, serikali ya Hispania ilifichua kwamba klabu hizo zilikuwa na deni la pamoja la Pauni 507 milioni kwenye mamlaka ya kodi peke yake. Je, hali ilikuwaje kwenye ligi nyingine za Ulaya kabla ya utambulisho wa FFP uliokuja kuziokoa klabu kwenye hatari ya kufilisika. Itaendelea kesho.