Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Elon Musk atakapoinunua Liverpool

Muktasari:

  • Kinachoelezwa ni kwamba mwasisi huyo wa SpaceX anaweza kufungua pochi kuinunua Liverpool kwa mujibu wa baba yake bilionea huyo, Errol, akidai kwamba mwanaye ana mpango wa kuichukua timu hiyo. Hata hivyo, baba huyo alitoa angalizo kwamba, hiyo haina maana kwamba mwanaye atainunua Liverpool.

LIVERPOOL, ENGLAND: LIVERPOOL iko moto sana kwenye Ligi Kuu England - lakini tajiri Elon Musk anataka kuifikisha mbali zaidi klabu hiyo.

Kinachoelezwa ni kwamba mwasisi huyo wa SpaceX anaweza kufungua pochi kuinunua Liverpool kwa mujibu wa baba yake bilionea huyo, Errol, akidai kwamba mwanaye ana mpango wa kuichukua timu hiyo. Hata hivyo, baba huyo alitoa angalizo kwamba, hiyo haina maana kwamba mwanaye atainunua Liverpool.

Kinachoelezwa kampuni ya Fenway Sports Group inayoimiliki Liverpool kwa sasa haina mpango wa kuiuza klabu hiyo, ambayo kwa mujibu wa Forbes inathaminishwa kuwa na thamani ya Pauni 4.3 bilioni. Kwa maana hiyo, kama kuna mtu atahitaji kuinunua Liverpool, basi huyo atakuwa tajiri wa dunia.

Kocha mpya Arne Slot ametumia pesa kidogo sana kwenye usajili wa timu hiyo hadi sasa, lakini wala hilo halijaathiri matokeo yao ya uwanjani kwenye Ligi ya Kuu England na Ligi ya Mabingwa Ulaya. Makala haya yanahusu jeuri itakayoonyeshwa na Liverpool sokoni itakapochukuliwa na bilionea Musk.


Kylian Mbappe anang'oka Madrid

Real Madrid ilinasa huduma ya Kylian Mbappe bure kabisa kutoka PSG mwaka jana, lakini fowadi huyo Mfaransa hatakuwa na la kugomea endapo kama Musk atatua Liverpool na kumtaka mkali huyo akakipige Anfield. Mkataba wa Mbappe huko Real Madrid utakoma 2029, huku mshahara wake akilipwa Pauni 250,000 kwa wiki baada ya makato ya kodi. Kiasi hicho cha pesa ni kidogo sana ukilinganisha na Liverpool inavyowalipa wachezaji wake, ambapo supastaa Mohamed Salah anapokea mkwanja wa maana. Mbappe, 26, aliwahi kufichua pia anamfuatilia staa wa mpira wa kikapu, LeBron James, ambaye pia anamiliki hisa chache kwenye kampuni ya FSG inayoimiliki klabu ya Liverpool.

Na ukweli ni kwamba Liverpool haitasubiri Mbappe amalize mkataba wake huko Real Madrid kwa sababu itakapofika wakati huo mkali huyo atakuwa na umri wa miaka 31, hivyo Musk akichukua klabu hiyo, Mbappe atanaswa fasta kikosini kwa sababu timu itakuwa na pesa ya kutosha.


Alexander Isak anatua Anfield

Liverpool inafahamu wazi ubora wa straika Alexander Isak msimu huu. Fowadi huyo wa Sweden amefunga mara moja na kuasisti mara moja kwenye mechi dhidi yao wakati Newcastle ilipotoka sare ya 3-3  na Liverpool, Desemba na kuifanya miamba hiyo ya St James' Park kuwa miongoni mwa timu mbili ambazo zimepata pointi kutoka kwa kikosi hicho cha Arne Slot. Timu nyingine ni Arsenal. Supastaa wa Manchester City, Erling Haaland anawezekana kuwa mshambuliaji bora kabisa duniani kwa sasa, lakini shughuli ya Isak ni balaa zito na ni mchezaji ambaye anaweza kufiti kabisa Liverpool.

Ana uwezo wa kutengeneza nafasi na kuwasumbua mabeki wa timu pinzani. Newcastle United inataja bei yake kuwa ni Pauni 150 milioni, kitu ambacho hakitakuwa tatizo kwa Liverpool endapo kama itakuwa chini ya bilionea Musk. Kutokana na mshambuliaji Darwin Nunez kushindwa kuonyesha ubora mkubwa sana jambo ambalo linaweza kuisukuma miamba hiyo ya Anfield kwenda kwa Isak.


William Saliba anapewa mkoba

Kwa muda mrefu msimu huu gumzo kubwa kwenye kikosi cha Liverpool ni kutofahamika kwa hatima ya beki wa kati Virgil van Dijk, ambaye mkataba wake utafika tamati Juni mwaka huu. Mdachi huyo anajiandaa kufikisha umri wa miaka 34 wakati wa dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi na ndio maana Liverpool sasa inapaswa kujiandaa kutafuta mtu wa kuja kuchukua mikoba yake tena mwenye kiwango bora kabisa kwenye Ligi Kuu England.

Kwenye hilo, kwenye kikosi cha Arsenal yupo beki wa kati matata kabisa, William Saliba, ambaye Liverpool inaweza kwenda kunasa huduma yake na kuwa kwenye mikono salama kabisa, huku Mfaransa huyo umri wake ukiwa miaka 23 tu. Saliba ni beki mwenye uwezo mkubwa, hivyo Liverpool itakuwa kwenye mikono salama endapo kama itafanikiwa kunasa huduma yake wakati itakapochukuliwa na mtu mwenye pesa nyingi duniani, bilionea Musk.


Lamine Yamal kupewa wingi moja

Katika mapengo ambayo Liverpool italazimika kuyaziba basi moja wapo ni la winga Mo Salah. Staa huyo wa Misri anahusishwa na mpango wa kutimkia huko Saudi Arabia, huvyo atakapoondoka Anfield ataacha pengo litakalohitajika kuzibwa. Na kama hilo litatokea na Liverpool wakati huo watakuwa na pesa za kutosha, basi bila shaka itakwenda Nou Camp kwenda kunasa huduma ya winga matata kabisa wa Kihispaniola, Lamine Yamal.

Wakati sasa Salah akitajwa kuwa winga bora kabisa duniani, basi Yamal kwenye umri wa miaka 17 tu alionyesha moto wake. Tangu alipoanza kuibukia kwenye kikosi cha kwanza cha Barcelona mwaka 2023, kinda huyo amefunga mabao 15 na kuasisti mara 21 kwenye mechi 74 na sasa anaonekana kupevuka zaidi. Kwa sasa, staa huyo tayari amehusika kwenye mabao 20 katika mechi 23 alizochezea Barcelona msimu huu, akifunga mabao manane na kuasisti 12. Mkataba wake una kipengele kinachohitaji ilipwe Pauni 866 milioni kwa timu itakayohitaji kuvunja mkataba wake.