Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dili 15 moto EPL ndani ya siku 7

DILI Pict

Muktasari:

  • Liverpool bado iko kwenye harakati za kutafuta mbadala wa Mohamed Salah, wakati Manchester United iko kwenye uhitaji mkubwa wa beki wa pembeni.

LONDON, ENGLAND: MSIMU wa Ligi Kuu England umeshaanza, lakini bado kuna dili mbalimbali zinazoweza kufanyika katika soko la usajili, huku zikiwa zimesalia siku saba pekee kabla ya dirisha kufungwa. Bado kuna dili kubwa zinazohitaji kukamilishwa, hasa baada ya baadhi ya udhaifu wa timu kuonekana katika wikiendi ya ufunguzi wa ligi hiyo.

Liverpool bado iko kwenye harakati za kutafuta mbadala wa Mohamed Salah, wakati Manchester United iko kwenye uhitaji mkubwa wa beki wa pembeni.

Manchester City kwa upande wake inaweza kutumia fedha nyingi, huku uwanja wake wa Etihad ukionekana kuwa kama kituo cha kupishana kwa wachezaji kutokana na nyota kadhaa wanaotarajiwa kuondoka. Na Daily Star Sport imeangalia dili 15 zinazoweza kukamilika kabla ya muda wa mwisho wa usajili.

DIL 01

Arsenal ilionekana kuwa imara katika mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu England dhidi ya Coventry, lakini kocha Mikel Arteta anavutiwa na huduma ya straika wa Atletico Madrid, Julian Alvarez, 26, anayeuzwa Pauni 85 milioni. Hata hivyo, Muargentina huyo anayetaka kuondoka klabuni kwake haonekani kuwa na shauku kubwa ya kujiunga na Arsenal.

Victor Osimhen, 29, ni chaguo jingine kwa Arteta katika safu ya ushambuliaji, lakini nyota huyo wa Galatasaray ambaye amewekewa bei ya karibu Pauni 55 milioni anaonekana kuwa chaguo la gharama nafuu ukilinganisha na Alvarez.

DIL 02

Kwa upande wa Liverpool, kocha Andoni Iraola anatafuta mbadala wa Salah, huku nyota wa PSG, Bradley Barcola akionekana kuwa kinara katika orodha ambapo Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 23 atakuwa na gharama kubwa, kwani PSG inadaiwa kutaka kati ya Pauni 111 milioni na milioni 128.

Liverpool pia inadaiwa kumlenga kinda mwingine wa PSG, Ibrahim Mbaye. Kama ilivyo kwa Barcola, Mbaye, 18, hayupo katika mipango ya PSG na anaweza kuondoka Paris kwenda Anfield kwa ada ya karibu Pauni 50 milioni.

DIL 03

The Reds wanaonekana kuweka wazi machaguo yao katika eneo la pembeni, huku pia wakimtaka nyota wa Brighton, Yankuba Minteh, 22.

Ripoti za hivi karibuni zinaeleza kuwa ofa ya tatu inaweza kutumwa, huku Brighton ikihitaji Pauni 60 milioni kama bei yake.

Maadui wakubwa wa Liverpool, Manchester United, wanaonekana hatimaye kufanikiwa kumnasa Carlos Baleba kutoka Brighton, wakitarajia kutangaza usajili wa kiungo katika dili lenye thamani ya awali ya Pauni 65 milioni na Pauni 5 milioni za nyongeza kutegemea kiwango chake.

DIL 04

Kocha Michael Carrick pia bado anahitaji beki wa kushoto, na United inahusishwa kwa kiasi kikubwa na Lewis Hall, 21, ambaye amekuwa akivutia akiwa Newcastle United. Hata hivyo, Hall hatakuwa nafuu kwa United kwani inaweza kulazimika kulipa zaidi ya Pauni 70 milioni.

Straika Ollie Watkins anaonekana kuwa njiani kuondoka Aston Villa baada ya kocha wake Unai Emery kutojibu alipoulizwa kuhusu kutokuwapo kwake kwenye kikosi Jumapili, ambapo anakwenda Al-Hilal ya Saudia. Na Watkins anaweza kuungana Al-Hilal na Gabriel Martinelli, 25.

DIL 05

Huku nyuma Nicolas Jackson, 25, anatafuta njia ya kuondoka Chelsea baada ya kutumia msimu uliopita kwa mkopo Bayern Munich na  inaaminika kuwa Chelsea imeshusha bei yake hadi Pauni 65 milioni, huku Aston Villa ikimfuatilia kama mbadala wa Watkins.

Katika kikosi cha Man City, kocha Enzo Maresca alilazimika kubadili mfumo katika kikosi chake alipokabiliana na Bournemouth kwa kumtumia  beki wa kati, Marc Guehi kwenye eneo la chini la kiungo kutokana na kutokuwapo kwa viungo mahiri walioondoka Rodri na Bernardo Silva waliotimkia Barcelona na Real Madrid mtawalia.

Na sasa Manchester City inaonekana kuchukua hatua haraka katika soko la usajili kwa kukubaliana na Lille kuhusu dili la Pauni 86 milioni kwa ajili ya Ayyoub Bouaddi mwenye miaka 18. Hata hivyo, huenda Maresca hajamaliza shughuli yake. City imekuwa ikihusishwa na Enzo Fernandez kipindi chote cha majira ya joto.

Ikiwa Muitaliano huyo anataka kuungana tena na Fernandez, 25, itailazimu City kutumia kiasi cha Pauni 120 milioni ili kumvuta kutoka Chelsea.

City pia itakuwa ikiwaaga baadhi ya wachezaji kabla ya muda wa mwisho wa usajili, huku Savinho, 22, akionekana atakayeuzwa kwa bei kubwa  baada ya kukubaliana kujiunga na Tottenham Hotspur katika dili la Pauni 85 milioni.

Na Mbrazili huyo ataungana na Omar Marmoush, 27, ambaye pia ataondoka Etihad na kuhamia Spurs msimu huu kwa mkopo, huku kukiwa na kipengele cha lazima cha kumnunua kwa Pauni 50 milioni msimu ujao.

Pia Nico Gonzalez anaonekana kuwa njiani kuondoka Etihad kutokana na  kupata wakati mgumu kuonyesha kiwango tangu alipohamia akitokea Porto, na ripoti zinaeleza kuwa anaweza kuhamia Newcastle United kwa Pauni 50 milioni.